The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,032
- 1,675
TAWALA ZA AFRIKA NA BIASHARA YA NISHATI
Tutanunua umeme kutoka Ethiopia kwa ajili ya mikoa ya Kaskazini. Mikoa hiyo ina barabara nzuri, nyama choma nyingi na watalii wengi lakini haina uhakika wa umeme.
Kenya itatumika kama posta. Itapokea kifurushi toka Ethiopia na kukikabidhi Tanzania. Hakuna kukichokonoa kama posta zetu. Tozo zote zitalipwa na “cha juu” pia. Sasa tutafakari;
1. Uganda ilikuwa inatuuzia umeme ili kuchimba Tini kule Kyerwa miaka ya 1970. Umeme ulizalishwa eneo la Kikagati-Murongo katika mto Kagera. Akaja Idd Amin, akasitisha na kubomoa. Sasa tumejenga upya. Akija Gen. Muhoozi Kainerugaba, hatabomoa tena? Besigye akikimbilia Tanzania, mkataba utapona?
2. Kagera tunapokea umeme kutoka Jinja. Ukifika Kyaka, tunasema ni wa Tanesco. Siku wakorofi wa TZ wakitoboa bomba la mafuta, Uganda haitazima Tanesco Kagera?
3. Hivi DRC ingekuwa inauza umeme Rwanda; M23 ikashindwa kuiteka Kinshasa, mgogoro ungekuwaje? Je M23 inayoongoza Goma, yaweza kuiuzia Tanesco-Kigoma? Tshekedi akirejesha Goma mikononi mwake, mkataba wa Kigoma utapona?
4. Urusi ilikuwa inaiuzia Ujerumani gesi nyingi. Katika vita ya Ukraine, Ujerumani akamuunga mkono Ukraine. Urusi akaziba bomba la gesi. Bei ikapanda Ujerumani. Kura za serikali zikashuka. Wafuasi wa Hitler sasa ni wa pili kwa wingi bungeni. Hakuna chama cha kuunda serikali peke yake. Mikataba ya kuuziana nishati iende sambamba na kununua mitambo ya kutengeneza kura bandia! Msicheke, naandika nikiwa nimesinzia.
5.Tatizo la kuvunja kwa umeme si jipya. Kila kitu kinavuja nchi hii. Siri zinavunja, nyumba zinavuja, mitihani inavuja, imani inavuja, maji yanavuja, damu inavuja na hata kura zinavunja! Taifa letu ni kubwa. Mchawi wetu ni KUHODHI KILA KITU KITOVUNI (Centralization). Hili nitalizungumzia siku nyingine.
Tujiulize:
a) Hivi ni lazima tuwe na shirika moja la umeme? Shirika moja la ndege? Shirika moja la reli? Wahenga wa Kinyambo wanasema “Mtoto wa pekee hamalizi ugumba wa wazazi”.
b) Inavyoonekana, nishati ni roho ya tawala zetu. Twaweza kujizuia kuichokonoa roho yetu? Nishati ni usalama, ni diplomasia, ni demokrasia, ni sheria, ni imani, ni elimu. Je kuna uendelevu wa nishati nje ya utawala bora?
c) Tumezungukwa na nchi ambazo hazijatulia: Rwanda, Burundi, Uganda, DRC, Msumbiji, Malawi, hata Kenya. Hizi biashara na mikataba ya kufanya na “Marais” wa mpito au waliokalia viti kwa tako moja ina uhakika gani?
Hatujachelewa. Tuondoe hodhi (monopoly). Kampuni za simu wanatupiga kwenye vifurushi kwa sababu ya uroho wa watu wetu wanaokula bila kunawa, lakini makampuni yanashindana kutupatia huduma. Tanesco deko linaiua.
Ikikisa umeme ni taabu. Ikipata wa ziada ni taabu. Hata ukiigawia nguzo bure, magaro bure, mishahara bure - italia na wasiolipa bill ambao ni serikali. Sasa inalalamika umene unavuja. Kweli?
Tanesco ndiyo inavuja kwa deko.