Askofu Bagonza: SHUKRANI na USALITI(Kusaliti, Kusalitiwa na Kusalitiana).

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
29,293
31,105
SHUKRANI na USALITI

Wapendwa marafiki wa ukurasa huu wa Kalikawe Lwakalinda Bagonza, napenda kuwashukuruni nyote kwa kuniombea na kunitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa (6 Desemba).

Salaam zenu na pongezi zenu kwa maelfu zilinitia moyo na kuongeza deni lisilolipika.

Kwa njia hii pokea shukrani zangu nyote. Endeleeni kuwa marafiki wema.
🙏🙏🙏🙏

KUSALITI, KUSALITIWA na KUSALITIANA.

1. Niligombea nikashindwa lakini nikatangazwa mshindi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

2. Niligombea nikashinda lakini mwingine akatangazwa mshindi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

3. Nilishinda sikutangazwa lakini nimeteuliwa na niliyemshinda nikakubali. Nani msaliti? Nani Msalitiwa?

4. Niwe Nilishindwa au kushinda anayejua ukweli ni aliyetangaza. Aliyetangazwa ana kosa gani? Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

5. Wananchi wanaamini kura ndiye mwamuzi. Sheria inatambua tangazo ndiye mwamuzi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

6. Mimi ni Mwalimu. Shida ninazo nyingi mpaka za ziada. Nimepewa amri au bahasha nikaachia sanduku linajisiwe. Nani msaliti? Nani msalitiwa?

7. Mimi ni mwalimu, baada ya kunogewa na bahasha au amri, nikiachia mtihani wa taifa unajisiwe, nani msaliti na nani msalitiwa?

Msaliti na Msalitiwa hawatenganishwi na ukuta bali kwa pazia. Tusalitiane ndipo tuaminiane au tuaminiane ndipo tusalitiane?

Baba wa Taifa alipozongwa na wapenda usuluhishi wakati wa vita ya Kagera aliwauliza, "Nani anamuamini Amin?' Hakupatikana.

Nijualo ni kuwa:

Unasalitiwa ili ujifunze kusaliti
Unasaliti kwa kuogopa usaliti
Ukimshawishi mtu afanye usaliti akakubali, unaishi naye kwa mashaka. Mazungumzo ya siri chumbani, sebuleni kicheko na masikhara.

Simuliwa na aliyeona siyo na aliyesikia. Ukikosa usingizi andika taarabu na mashairi.

Mbwa Koko aliye huru ni tajiri kuliko Mbwa wa tajiri anayeshinda kwenye mnyororo.

Mnaoteka uhuru wetu, Mungu akichelewa kujibu, tutawashtaki kwa shetani.
 
BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALITUTAJIA MAADUI.

1. UMASIKINI
2.UJINGA.
3. MARADHI.

Akasema Hawa ni maadui wa kweli kweli katika hili Taifa.

LEO 2024 BAADA YA MIAKA 60 TUMEKUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI.

2024 maadui wameongeseka Zaidi kuliko wale watatu wa 1961.

1.Umasikini na ufukara.
2.Ujinga na upumbavu.
3.Magonjwa na Maradhi.

4.Mmomonyoko wa Maadili.
ushoga, usagaji Kamali, sugar mamy, sugar Dady mashangazi
AJIRA.
5. Rushwa na Upendelo

6. USimba na u yanga.
7. Mitandao ya kijamii Tiktok, x, nk
8. Manabii wa uongo na Mashehe Uchwara.
9. Ajali nyingi mno.
10. Gharama kubwa za maisha, ujenzi holela nk

MAMBO NI MENGI SANA VIJANA WA KITANZANIA WANAWAZA MAMBO YA HOVYO SANA SIMBA NA YANGA ZINATAWALA MIKEKA NK.

OKOENI TAIFA LENU LEO.

IPO SIKU HILI TAIFA LITAZIDIWA NA SOMALIA KIUCHUMI.

MKIFIKA MBINGUNI MTAHOJIWA NA MUNGU MLILIFANYIA NINI TAIFA LENU NIMEMALIZA.
 
SHUKRANI na USALITI

Wapendwa marafiki wa ukurasa huu wa Kalikawe Lwakalinda Bagonza, napenda kuwashukuruni nyote kwa kuniombea na kunitakia heri katika siku yangu ya kuzaliwa (6 Desemba).

Salaam zenu na pongezi zenu kwa maelfu zilinitia moyo na kuongeza deni lisilolipika.

Kwa njia hii pokea shukrani zangu nyote. Endeleeni kuwa marafiki wema.
🙏🙏🙏🙏

KUSALITI, KUSALITIWA na KUSALITIANA.

1. Niligombea nikashindwa lakini nikatangazwa mshindi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

2. Niligombea nikashinda lakini mwingine akatangazwa mshindi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

3. Nilishinda sikutangazwa lakini nimeteuliwa na niliyemshinda nikakubali. Nani msaliti? Nani Msalitiwa?

4. Niwe Nilishindwa au kushinda anayejua ukweli ni aliyetangaza. Aliyetangazwa ana kosa gani? Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

5. Wananchi wanaamini kura ndiye mwamuzi. Sheria inatambua tangazo ndiye mwamuzi. Nani Msaliti? Nani Msalitiwa?

6. Mimi ni Mwalimu. Shida ninazo nyingi mpaka za ziada. Nimepewa amri au bahasha nikaachia sanduku linajisiwe. Nani msaliti? Nani msalitiwa?

7. Mimi ni mwalimu, baada ya kunogewa na bahasha au amri, nikiachia mtihani wa taifa unajisiwe, nani msaliti na nani msalitiwa?

Msaliti na Msalitiwa hawatenganishwi na ukuta bali kwa pazia. Tusalitiane ndipo tuaminiane au tuaminiane ndipo tusalitiane?

Baba wa Taifa alipozongwa na wapenda usuluhishi wakati wa vita ya Kagera aliwauliza, "Nani anamuamini Amin?' Hakupatikana.

Nijualo ni kuwa:

Unasalitiwa ili ujifunze kusaliti
Unasaliti kwa kuogopa usaliti
Ukimshawishi mtu afanye usaliti akakubali, unaishi naye kwa mashaka. Mazungumzo ya siri chumbani, sebuleni kicheko na masikhara.

Simuliwa na aliyeona siyo na aliyesikia. Ukikosa usingizi andika taarabu na mashairi.

Mbwa Koko aliye huru ni tajiri kuliko Mbwa wa tajiri anayeshinda kwenye mnyororo.

Mnaoteka uhuru wetu, Mungu akichelewa kujibu, tutawashtaki kwa shetani.
Aisee!
 
Back
Top Bottom