Pre GE2025 Askofu Bagonza: Naogopa kuamini ahadi za uchaguzi za Rais Samia sababu hazina misingi ya kisheria na kikatiba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,304
4,793
Na Askofu Bagonza

RAIS SAMIA HALAZIMIKI KUFUATA NJIA YA JPM KUHUSU CHAGUZI ZETU:

Ndiyo. Rais Samia anatoka chama kile kile alichoongoza hayati JPM.

Ndiyo. Rais Samia alikuwa Makamu wa JPM, lakini HALAZIMIKI kurithi misimamo ya JPM kuhusu chaguzi zetu na mahusiano mabaya na vyama vya upinzani.

Misimamo hiyo, ilivunja katiba, ilivunja haki za binadamu na iliifunga nchi.
Ndiyo maana Rais Samia aliamua kuondoa mazuio yaliyovunja katiba, akatamka hadharani kufungua nchi na kuzindua falsafa ya 4R ili kuliepusha taifa na sifa mbaya ya kuvunja haki za binadamu na kukosa utawala bora.

Kuhusu chaguzi zetu, yeye binafsi na pia wasaidizi wake walitamka hadharani kuwa yaliyotokea 2019 na 2020 hayatajitokeza tena. Niliwahi kueleza kuwa mimi “ninaogopa” kuamini ahadi hizo kwa kuwa hazina misingi ya kisheria na kikatiba. Lakini kwa kuwa zilitolewa na viongozi walioapa kwa misahafu, niliamua kuishi kwa imani.

Swali: KWA NINI TUSIKUBALI UCHAGUZI KUFANYIKA KABLA YA MAREKEBISHO YA MAENEO MUHIMU YA KATIBA (Minimum Reforms).

Kufuatia kuapishwa kuwa Rais baada ya uchaguzi wa 2015, JPM alitoa amri ya mdomo ya kukataza shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani.
Amri hiyo ilikiuka Katiba ya JMT hususan Ibara za 12 hadi 21.

Kwa bahati mbaya watu na taasisi waliotegemewa kupinga au hata kukemea ukiukwaji huo wa Katiba ya JMT, walikaa kimya kana kwamba jambo hilo haliwahusu.

Wafuatao walipaswa angalau KUNUNA kwa ukiukwaji huo:

1. CCM na UONGOZI WA JUMUIYA ZAKE.

Kwa kuwa CCM haina baraza la Wazee, wale wazee wachache waliofunua midomo yao na kunong'ona, JPM aliwatisha kuwa wakome "kuwashwa washwa".

2.Bunge la JMT lenye mamlaka ya kuishauri na kuisimamia Serikali nalo liliufyata na kuanza kuimba masifu na mapambio kwa JPM.

3.Mwanasheria mkuu wa Serikali.

4.Msajili wa Vyama vya siasa.

5.Viongozi wa Asasi mbali mbali zinazohusika na utetezi wa HAKI
ZA BINADAMU.

Mtu pekee aliyejitokeza kupinga ukiukwaji huo wa Katiba kwa njia ya UJASIRI na UWAZI ni TUNDU ANTIPAS LISSU ambaye alikuwa Rais wa TLS wakati huo. Matokeo yake alishambuliwa kwa risasi nyingi. Ni Rais Samia pekee aliyejitoa mhanga akiwa Makamu wa Rais aliyefika Nairobi kumjulia hali Tundu Lisu.

Ilipofika 2019, JPM alitoa tamko jingine la kuvunja KATIBA pale alipowaagiza Wakurugenzi (DED) kutowatangaza wapinzani kama Washindi kwenye chaguzi za Serikali za mitaa na mwaka uliofuata,2020 uchaguzi mkuu.

Amri hiyo ya JPM ilikiuka Katiba kwa uwazi kabisa.

Na, kama ilivyokuwa kwa amri ya awali ya katazo la shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani, WOOTE WALIOPASWA KUIPINGA walinyamaza kimya.

Baada ya kifo cha JPM, Rais SSH, hatimaye alitengua katazo la shughuli za kisiasa lakini BILA SHAKA KWA MAKUSUDI hakusema kitu juu ya Amri ya pili ya mtangulizi wake.

Matokeo yake uliotegemewa kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2024 umechukua sura ile ile ya uchaguzi wa 2019. NI KUTOANDIKISHA WAPIGA KURA KWENYE NGOME ZA WAPINZANI, KUWAENGUA WAGOMBEA WAO WENGI, KUTOWARUHUSU MAWAKALA WA VYAMA VYA UPINZANI na KUTOWATANGAZA WAPINZANI hata pale walipoonekana kushinda. Hili ni donda ndugu linalochafua “Legitimacy” ya viongozi wetu wa vitongoji.

Kama ilivyokuwa 2019 na 2020, mchakato wote wa Uchaguzi wa 2024 umekiuka Katiba ya JMT, sheria zoote husika na MISINGI ya kuendesha Uchaguzi KWA JAMII INAYOJIESHIMU.

MILA ZETU ZA KIAFRIKA ZINASISITIZA KWAMBA KUNA KIWANGO CHA CHINI KABISA CHA MTU AU JAMII KUJIHESHIMU, ISIPOKUWA KAMA MTU NI PUNGUANI.

Swali: NINI KITATOKEA ENDAPO TUTAENDA KWENYE UCHAGUZI WA 2025 BILA MAREKEBISHO?

Kwanza,Rais SSH bado hajatengua amri ya JPM ya KUWAKATAZA ma DED kuwatangaza WAPINZANI kama washindi wa Ubunge na Udiwani.

Pili,Tume ya Uchaguzi iliyobatizwa jina la HURU bado ni ileile kuanzia uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu wake na wajumbe wengine. Ni hivyo hivyo kwa Mkurugenzi na Sekretarieti ya Tume.
 
1739388788187.jpg
 
Ahhh that same old script ya you v ccm na chawa wake
Wakishindwa kutoa hoja kimbilio lao ni hilo hilo. ; Huyu sio raia wa nchi yetu au Huyu anatumiwa na mabeberu !! Kesho yake Samia yuko kwa hao hao mabeberu anatembeza bakuli.
 
Back
Top Bottom