Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
29,488
31,528
KKKT Ina MKUU MMOJA TU

Naona KKKT imepamba moto kutokana na matamshi ya mmoja wa Maaskofu wake. Kwa kimbelembele nilicho nacho naomba umma wa watanzania uelewe yafuatayo:

1. KKKT ina Mkuu mmoja tu. Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja.

2. KKKT hakuna cheo kinaitwa “Mkuu wa Kanisa Mstaafu”. Tunaweza kuwa na cheo cha “Aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa”. Hivi sasa tuna “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” ambaye amechaguliwa tena Mkuu wa Kanisa. Kama angekuwa Mstaafu asingechaguliwa. Inawezekana “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” akachaguliwa kuwa Mkuu tena. Sitashangaa aliyepita hivi karibuni, kuchaguliwa tena.

3. Kama kuna mstaafu, ASTAAFU. Si lazima kuhudhuria; si lazima kusema. Ukipenda, usipende kwa niaba. Ukichukia, usichukie kwa niaba. Kila ulimi una uwezo wa kuonja wenyewe,

4. KKKT ni shirikisho, siyo kanisa moja. Ukitaka kusema kwa niaba ya shirikisho, unashawishi siyo kuburuza, Hatujashawishika na hatujakaa.

5. Nampenda rais Samia, lakini sijatumwa na kanisa. Naweza kumpenda na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Hayo nitayasemea Karagwe siyo penginepo. Na nikiyasema, ni yangu na tumbo langu; siyo ya Wanyambo wala Walutheri walio wenye vyama vyao. Wanyambo haturuhusu mgeni kupiga mluzi katika nyumba ya mwenyeji.

6. Kanisa lina wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama. Chadema msitutolee macho na CCM msishangilie. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa.

7. Rais Samia ana uwezo wa kujiharibia. Tusimharibie. CCM ina uwezo kujiharibia; haijaomba msaada wa kuisaidia kuharibu. Lipo kundi linalodhani linamsaidia rais Samia, wakati linamharibia. Lipo linalodhani linamharibia lakini linamjenga. Anayesimama na HAKI anamsaidia rais Samia.

8. Tuna tatizo kitaifa: Kuna watu wanatumia dini kueneza siasa. Na kuna watu wanatumia siasa kueneza dini. Mimi si mmoja wa hao wawili. Mimi natumia ujinga kueneza dini na siasa. Wajinga tu, ndio wananisikiliza na kunifuata. Wewe mjuaji kaa pembeni tuendelee na safari.

9. Nikisema jambo mkanishangilia, mnanipa kiburi cha kusema bila kufikiri.
Nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari; si kuhemuka. Mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana.

10. Mungu analipenda Taifa hili kuliko mtu au chama chochote kinavyoweza kudai kulipenda. Usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili taifa. Ina gharama nzito kushuhudia Mungu anavyolipenda hili taifa.

Hata anayerudi nyuma ana mbele anakoelekea. Ukisifiwa kuwa na mbio, jihadhari usipitilize nyumbani kwenu.

Source: FB page yake

Pia soma
 
Huyo Askofu Shoo naye kaongea tu kama m Tanzania yeyote anavyoweza kuongea, pia siyo lazima ukubaliane na maneno yake.

1 Timotheo 5 : 1 Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;

Ni nini kinafanya hawa wachunga kondoo wa Bwana kufuatiliana?

Ile amri ya Upendo kwao haipo.

Yohana 13 : 34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom