Askofu Bagonza, barua ya kumkaribisha Rais Magufuli Mkoani Kagera na tahakiki ya mjadala tunduizi

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,057
2,621
1610698451817.png


A. UTANGULIZI

Rais wa Tanzania, John Magufuli alikuwa Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi wilayani Karagwe na baadaye Wilayani Bukoba tangu tarehe 18 Januari 2020. Inaonekana kuwa, siku hiyo, Askofu Dr. Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza, aliandika barua tepe kwa ajili ya kumkaribisha Rais Magufuli Mkoani Kagera na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Nimeisoma barua husika na kuiweka mwishoni mwa andiko hili, li wasomaji wanaotaka kujisomea wenyewe waweze kufanya hivyo. Kwa maoni yangu, hoja ya sasa ya Dr. Bagonza, ambayo nakusudia kuiunga mkono kwa kuongezea ushahidi ninaoufahamu, inakusudia kutetea pendekezo lifuatalo:

Kwamba, kuna haja ya kuwawezesha watu wa Kagera kuendelea kuvaa kofia yao yenye nembo ya “Nshomile” kwa kufanya jambo mojawapo kati ya mawili: (1) Ama, kwa serikali kurejea maamuzi yake ili kuwaruhusu watu wa Kagera kufufua vyuo vyao haraka na kuviendeleza; (2) Au, kwa serikali yenyewe kubeba jukumu la kuanzisha chuo kikuu cha umma mkoani Kagera, ambacho chaweza kuwa tawi la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini kwa sasa au chuo kikuu kipya.

Ametaja sababu tatu kulitetea. Pia amebashiri pingamizi dhidi ya hoja yake na kulijibu.

Hii ni hoja nzuri na nzito, endapo itaboreshwa kama nitakavyopendekeza baada ya kuchambua kwa kina na kuhakiki hoja nzima.

Uhakiki rasmi unafuata hapa chini kwa kutumia mbinu za kuchambua na kuhakiki mijadala iliyosheheni hoja chokonozi (critical discourse analysis), yaani uchambuzi wa mijadala iliyobeba hoja tunduizi, kwa maneno mengine.


1610701193013.png

Jengo la Utawala, Chuo cha KARUCO, Karagwe

B. UCHAMBUZI WA HOJA YA BAGONZA

Dhamira kuu ya mwandishi, Dk. Bagonza, ilikuwa ni kusanifu na kutetea hoja ambayo, kianatomia, inazo sehemu kuu sita zifuatazo:

Kwenye pendekezo kuu (claim) inadaiwa kwamba, kuna haja ya kuwawezesha watu wa Kagera kuendelea kuvaa kofia yao yenye nembo ya “Nshomile” kwa kufanya jambo mojawapo kati ya mawili: (1) Ama, kwa serikali kurejea maamuzi yake ili kuwaruhusu watu wa Kagera kufufua vyuo vyao haraka na kuviendeleza; (2) Au, kwa serikali yenyewe kubeba jukumu la kuanzisha chuo kikuu cha umma mkoani Kagera, ambacho chaweza kuwa tawi la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini kwa sasa au chuo kikuu kipya.

Kwenye sababu ya kwanza (ground) inadaiwa kwamba, kwa sasa watu wa Kagera wanajiona wanyonge kwa kuwa hawana chuo kikuu hata kimoja, baada ya vyuo vikuu kadhaa vilivyoanzishwa mkoani humo “kufwariki” kwa sababu ya “tetemeko la ardhi” lililotokana na mawimbi ya maamuzi ya serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Magufuli;

Kwenye sababu ya pili (warrant) inadaiwa kwamba, kwa mujibu wa historia, umaarufu wa watu wa Kagera unatokana na uwepo wa taasisi za kielimu zilizowafanya wavae kofia ya “Nshomile,” yaani kofia ya usomi;

Kwenye sababu ya tatu (backing) inadaiwa kwamba ukosefu wa elimu ya chuo kikuu inayopatikana kwa urahisi na katika maeneo ya karibu na nyumbani kunasababisha watu kujiona “wanyonge” kielimu mbele ya majirani zao wanaozidi kupaa kwa sababu ya kupata unafuu kama huo.

Kwenye pingamizi tarajiwa (anticipated objection), mwandishi alibashiri uwezekano wa mtu kupinga pendekezo lake la serikali kuvifungua vyuo vikuu vya Kagera, kwa kutumia sababu kwamba, vyuo hivi vilifungwa kwa sababu ya “mdomo” mrefu wa wamiliki wa vyuo hivi dhidi ya serikali. Mwandishi amemtolea mfano “mdomo” wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe” ambaye amekuwa mkosoaji endelevu wa maamuzi kadhaa ya serikali.

Kwenye ubutuaji wa pingamizi tarajiwa (rebuttal), mwandishi alitumia maelezo kwamba, pingamizi hili nidhaifu kwani, mbali na “mdomo” wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe” anayemiliki chuo kikuu cha KARUCO kuna vyuo vingine vitatu vimefungwa wakati wamiliki wake hawana “mdomo” kama wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe.”


1610701301626.png

Jengo la utawala, CARUMCO, Muleba

C. UHAKIKI YA HOJA YA BAGONZA
Utetezi wa sababu ya kwanza umefanywa na mwandishi kwa kuorodhesha vyuo vikuu vinne vilivyoanzishwa mkoani humo na baadaye “kufwariki,” yaani: (1) University of Bukoba iliyoanzishwa na Profesa Teddy Maliyamkono na wenzake; (2) Josiah Kibira University College (JOKUCO) KKKT iliyoanzishwa na KKKT; (3) Cardinal Rugambwa University (CARUMCO) iliyoanzishwa na TEC; na (4) Karagwe University College (KARUCO) iliyoanzishwa na Dayosisi ya Karagwe (KKKT).

Nimeridhika na utetezi huu. Hata hivyo, sababu hii ingeweza kuimarishwa zaidi kwa kusisitiza kwamba, kitendo cha kufunga chuo kikuu chochote ni hatua ya kulizuia Taifa kufikia idadi mwafaka ya watu wenye kiwango cha elimu ya chuo kikuu (university education attainment level) inayoliwezesha Taifa kushindana kwa ufanisi katika ulimwengu wa soko la pamoja linaloambatana na siasa za utandawazi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za UNESCO, watu wenye elimu ambayo ni angalau kidato cha nne hapa Tanzania ni chini ya 10%; Kenya ni juu ya 25%; na Uganda ni juu ya 15%. Kwa hiyo, kuna haja ya kupanua udahili katika ngazi ya vyuo vikuu ili tuweze kushindana na majirani zetu.

Utetezi wa sababu ya pili umefanywa na mwandishi kwa kuzitaja shule kongwe za mkoa wa Kagera kwa kutumia neno la “BUIKANO” linalomaanisha shule ya Bukoba Seco, Ihungo, Kahororo, Nyakato na Omumwani. Nimeridhika na utetezi huu.

Utetezi wa sababu ya tatu haukufanwa na mwandishi. Lakini, hii ni sababu ambayo iko wazo, kiasi kwamba, ni watu wachache wanaweza kuipinga. Kuna tofauti za kiuchumi na kisaikolojia kati ya anayepata elimu mkoani mwake na mtu anayepata elimu katika maeneo ya mbali na mkoa wa nyumbani.

Pingamizi tarajiwa na ubutuzi wake uliofanywa na mwandishi vinakubalika kimantiki. Hata hivyo, mwandishi alipaswa kwenda mbali na kubaini mapingamizi ya ziada na kuyabutua ili kulinda zaidi hoja yake.

Kwa mfano, nayafahamu mapingamizi mengine matatu ambayo mwandishi hakuyabaini wala kuyabutua. Mapingamizi hayo ni haya:

  • Kwamba, vyuo vinashindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU);
  • Kwamba, vyuo vinashindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu;
  • Na kwamba, vyuo vinakiuka misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Pingamizi linalohusu vyuo kushindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) linakigusa chuo kikuu cha KARUCO pekee. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii.

Nilipokuwa nakwenda Rwanda kumsalimia mjomba wangu, nilipita kwenye Chuo Kikuu cha KARUCO Karagwe ili kumtafutia nafasi mdogo wangu aliyekuwa anasoma Rugambwa.

Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Katabaro, aliniambia kwamba kwa sasa wameruhusiwa kutoa mafunzo kwa kutumia mitaala ya NACTE na wamenyimwa usajili wa chuo kikuu, japo miundombinu waliyonayo inawaruhusu kufanyakazi kama Chuo Kikuu.

Katika maelezo yake aliniambia kuwa, kigezo kigumu katika kutafuta usajili wa chuo kikuu ni sharti la kuwa na walimu walioajiriwa kwa mkataba wasiopungua idadi kadhaa. Walimu hao wanapaswa wasiwe wameajiriwa chuo kingine chochote. Na TCU inazo kanzidata ya kusajili walimu wa vyuo vikuu ili kuweza kufuatilia mikataba yao.

Dk. Katabaro aliniambia kuwa, ili kupata fedha za kuwaajiri walimu wa chuo kikuu watano inabidi ama chuo kiwe na vyanzo vyake vya mapato au kisajili wanafunzi na walipe karo. Kusudi upate wanafunzi walioidhinishwa na TCU inabidi kwanza usajiliwe na TCU kama Chuo Kikuuu! Kwa hiyo, njia hii haiwezekani. Na mpaka siku ile naongea na Dk. Katabaro, chuo cha KARUCO kilikuwa kimeshindwa kupitia njia mbadala ya kupata fedha za kuajili walimu ambao ni sharti muhimu kwa ajili ya usajili.

Kuhusu pingamizi hili, nilimtarajia Dr. Gagonza aseme jambo akieleza ni kwa vipi amepambana na changamoto husika, na kuhakikisha kwamba, mkwamo wa usajili hauanzii kwenye upande wake yeye kama mmiliki wa chuo cha KARUCO. Ni kwa njia hiyo, angekuwa amefungua mlango wa kujadili ni kwa vipi mkwamo wa usajili wa KARUCO unaanzia kwenye upande wa serikali.

Ni baada ya hapo, Profesa Ndalichako angelazimika kutoa maelezo juu ya mkwamo huo na kushauriwa ipasavyo na wanazuoni. Bila Dr. Bagonza kujipambanua katika jambo hili, pendekezo lake kwamba chuo cha KARUCO kinapaswa kusajiliwa kama Chuo Kikuu linabaki likining’inia hewani.

Pingamizi linalohusu vyuo kushindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu linavigusa vyuo vikuu baki vitatu, yaani, University of Bukoba, JOKUCO, na CARUMCO. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii pia.

Hata hivyo, siku nilipoongea na Dr. Katabaro wa chuo cha KARUCO, nilifahamishwa kwamba, hata vyuo hivi jirani yake vinayo matatizo na serikali kwa sababu mbili.

Sababu ya kwanza ni kwamba, kuna sera ya serikali ya kuitaka TCU kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu katika namna ambayo inatoa kipaumbele kwa vyuo vya serikali. Kwa mujibu wa sera hii, kama wanafunzi wenye sifa wakigawiwa kwenye vyuo vya serikali na kuisha, basi vyuo binafsi vinabaki mikono mitupu.

Na sababu ya pili niliyoambiwa na Dr. Katabaro ni kwamba, kuna sera ya serikali ya kutoa mikopo ya elimu ya juu ambayo inatoa kipaumbele kwa masomo maalum, kama vile masomo ya sayansi. Kwa sababu hii, vyuo binafsi vinavyotoa elimu kwa kufundisha kozi ambazo hazifadhiliwi na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu vinakufa kwa sababu ya kukosa wanafunzi wanaoweza kujilipia ada na mahitaji mengine yan kielimu.

Na pingamizi linalohusu vyuo kukiuka misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) linavigusa vyuo vikuu vyote vilivyoko sekta binafsi, kama vile University of Bukoba, JOKUCO, CARUMCO, SAUT, TUMAINI, na kadhalika. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii vile vile.

Nililibaini pingamizi hili mwenyewe wakati namsomesha mdogo wangu mmoja chuo cha TUMAINI. Wakati ule wanafunzi wa TUMAINI walilalamika sana juu ya ukubwa wa karo na huduma duni.

Askofu Dr. Malasusa alipokuja kuongea nao aliwambia kauli fupi sana: “asiyetaka kulipa karo hiyo na kusoma hapa aondoke.”

Baadaye ilibainika kuwa mhasibu wa TUMAIN DAR CAMPUS alikuwa na maagizo ya kupeleka 30% ya makusanyo yote ya jimboni kabla ya miamala mingine yote ya chuo kufanyika.

Kwa sababu hii, bajeti ya chuo ilikuwa inakata miezi mitatu kabla ya mwaka kuisha. Tangu hapo utawala wa chuo unaanza kuendesha chuo kwa kubahatisha.

Hii maana yake ni kwamba sehemu ya fedha ya serikali iliyotoka HESLB ilikuwa inatumika kuendesha Kanisa. Hii sio tuhuma ndogo.

Na katika mazingira haya, serikali ilianza kuvituhumu vyuo vikuu binafsi kadhaa kutumia fursa ya uwepo wa fedha za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kufanya biashara kwa kutoza ada kubwa. Jambo hili, kwa maoni ya serikali, linapingana na msingi wa kuanzishwa kwa HESLB.

Dr. Bagonza yuko Kanisa moja na Dr. Malasusa. Hivyo, huenda anayafahamu mamalalamiko haya kupitia kwa Askofu mwenzake. Hivyo, angeweza, na alipaswa, kulinda pendekezo lake la kuitaka serikali “kufungua” vyuo vikuu vya Kagera, kwa kusema jambo dhidi ya tuhuma hizi.


1610701427780.png

Jengo la utawala, Chuo cha JOKUCO, Bukoba

D. MATUMIZI YA LUGHA NA TASWIRA
Mdadisi wa mambo, kama vile Askofu Dk. Bagonza, anapoandika “mjadala tunduizi” (critical discourse) ulio katika muundo wa shairi, dayalogia, riwaya, makala au barua hutumia lugha ya picha aliyoichagua yeye ili kujenga taswira maalum inayofafanua na kuweka mkazo juu ya sababu, athari na utatuzi wa matatizo ya jumuiya kama vile uonevu, ubaguzi, ukabila, udini, ukanda, upotoshaji wa ukweli na unyonyaji kama yanavyojitokeza kati ya matabaka mbalimbali ya kijamii kwenye sekta za maisha kama vile afya, elimu, ofisi za utawala wa kisiasa, uchumi na media.

Kwa hiyo, wanazuoni wanapofanya “tahakiki ya mjadala tunduizi” (critical discourse analysis) wanatakiwa kubainisha, kuhakiki, kufafanua kuthibitisha au kukanusha uwepo wa sababu, athari na utatuzi wa matatizo ya jumuiya yaliyoibuliwa na mtunzi wa mjadala.

Kwa kuangalia lugha inayotumiwa na mtunzi, tunaweza kubaini aina kuu tano za taswira zinazoweza kutumikwa na mtunzi kusanifu mijadala ili kuitaka jamii kuingilia kati kumaliza tatizo.

Taswira hizo ni hizi: taswira inayoonyesha uwepo wa mgongano wa kitabaka (conflict frame); taswira inayoonyesha uwepo wa hisia kali (human interest frame); taswira inayoonyesha uwepo wa madhara hasi/chanya ya kiuchumi na kijamii (socio-economic consequences frame); taswira inayoonyesha uwepo wa ukiukwaji wa kanuni za maadili ya jamii (morality frame); na taswira inayoonyesha uwepo wa uwajibikaji au ukosefu wa uwajibikaji kwa wahusika (attribution of responsibility frame) (Semetko and Valkenburg 2002).

Kwa kuzingatia haya, “tahakiki ya mjadala tunduizi” uliomo katika “barua ya wazi kwa Rais,” kama ilivyoandikwa na Askofu Dk. Benson Kalikawe Bagonza na kusambazwa katika mitandao ya kijamii tangu asubuhi ya tarehe 18 Januari 2020, inaonyesha yafuatayo:

Mwandishi ametumia mbinu tatu kusanifu hoja yake. Kwanza, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa mgongano wa kitabaka (conflict frame) kati ya serikali na “Nshomile.” Ametoa ushahidi wa vyuo vilivyofungwa na serikali kinyume cha matakwa ya wamiliki.

Pili, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa hisia kali (human interest frame) za kina “Nshomile” kupoteza kofia yao ya usomi kwa sababu ya kukosa udahili kwenye vyuo vikuu vya karibu na nyumbani kwao. Uamuzi wake wa kutumia neon “kufwariki” kama ambavyo “Nshomile” hutamka neno “kufariki” ni ushahidi muhimu hapa.

Na tatu, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa madhara hasi ya kiuchumi na kijamii (socio-economic consequences frame) kwa sababu kuikosa elimu ya chuo kikuu ni sawa na kugeuka “mnyonge” kwa sababu ya kuukosa ufunguo wa maisha bora.


1610701778237.png

Makao Makuu, NACTE, Dar es Salaam

E. HITIMISHO, MUHTASARI NA MAPENDEKEZO
Barua ya Dr. Bagonza imeibua hoja nzuri yenye umuhimu na uharaka. Nina mapendekezo mahsusi kwa serikali na kwa Bagonza mwenyewe.

Kwanza ni kwa serikali: mahitaji ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni makubwa kuliko uwezo wa HESLB. Bosi wa HESLB apewe mamlaka ya kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ya bodi. Mgao toka serikalini hautoshi.

Lakini pia naye ajiongeze kwa kufanya reorganisation. Mfano, vision ya HESLB ya sasa haina focus wala clarity. Ni hii:

"To be a reliable and sustainable revolving fund in financing eligible Tanzanian Students for Higher and Tertiary Education."

Basi, Bosi wa HESLB, Abdul Razack, afikirie vision kama hii hapa:

"HESLB envisions to become a reliable and sustainable revolving fund that assists the nation to become the best East African candidate of quality university education attainment level through global fundraising toward broader and comprehensive education loan services to students".

Dira kama hii itaipa HESLB sababu yeye mwenye exposure ya kimataifa kuchakarika ipasavyo.


1611374558961.png

Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Abdul Razak

Kwa upande wa Bagonza, nashauri isiishie kuandika na kusambaza "nyaraka" kama Mtume Paul na kuzisambaza mitandaoni. Nashauri matatu.
  • Mosi, Dr. Bagonza ajielekeze kwenye kutafiti na kujibu mapingamizi yote yanayoweza kudhoofisha mapendekezo yake. Yaani, tuhuma kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU); kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu; na kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi matakwa ya misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
  • Pili, Dr. Bagonza apeleke majibu ya utafiti wake kwenye mamlaka husika za kiserikali, hasa, kwa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako.
  • Na tatu, Dr. Bagonza akae na mamlaka husika za kiserikali wayajenge kwa hoja kuhusu umuhimu na uharaka wa kufufua vyuo vya Kagera, na sio kuhusu kuanzisha chuo kipya cha umma. Hakuna haja ya kuanzia kwenye zero wakati tayari kuna kianzio kikubwa kuliko zero.
Lakini, yafaa Dr. Bagonza akakumbuka kuwa, Chuo Kikuu cha KARUCO kinao upekee dhidi ya vyuo vitatu baki alivyovitaja.

Kwanza KARUCO kinapanga kufundisha mitaala ya sayansi ya kilimo. Kwa hiyo wanafunzi wake wanaweza kupata mikopo baada ya KARUCO kusajiliwa kama Chuo Kikuu.

Kujenga hoja serikalini kwamba kozi zilizo katika mitaala hiyo zinapaswa kuingizwa katika oridha ya kozi zinazofadhiliwa na HESLB ni hoja inayowezekana kutetewa hadi kukubalika. Dr. Bagonza anaonekana ni bingwa wa advocacy and lobying.

Pili, sharti la kuajiri wahadhiri linajadilika kwa sababu ya uwezekano wa wanafunzi wake kupata ufadhili kutoka HESLB.

Kwa mfano, kuomba serikali iweke sera ya usajili wa muda itakayoiruhusu KARUCO kupata uhalali wa kudahili wanafunzi kupitia TCU sio hoja ngumu kujengwa.

Kwa hiyo, kuhusu KARUCO, natoa wito kwa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako, kuwa na sikio sikivu.

Kwa vile, akiwa jukwaani, leo Rais Magufuli ameomba na kupewa URAIA katika kabila la WANYAMBO wa KARAGWE kwa kina Bagonza, natarajia atatia neno hapo.

Kila la heri kwa Askofu Dr. Benson Kalikawe Lwalinda Bagonza, askofu wa Karagwe mwenye “mdomo.”

Nimalizie tahakiki yangu kwa kutoa angalizo. Dr. Bagonza anapaswa kupunguza “mdomo” kwa kujitenga na vilema vya habari vinne (“four information disorders”) ambavyo mara nyingi vimekuwa vikiambatana na maandiko yake kadhaa. Vilema hivyo ni:

  • Kusambaza taarifa potofu kwa kujua na kwa nia ovu ya kutafuta faida ya kiuchumi, kisiasa au kijamii (disinformation);
  • Kusambaza taarifa potofu bila nia ovu na bila kujua kwa imani kwamba usambazaji huo utamnufaisha mpokeaji (misinformation); na
  • Kusambaza taarifa za watu binafsi lakini ambazo ni za kweli kwa watu wasiohusika na kwa nia ovu ya kuwachafua watu wengine wasiokubaliana naye (malinformation).
  • Kuwapotosha watu kwa kusambaza taarifa zenye ukweli nusu nusu kwa makusudi ili kutafuta maslahi binafsi (deception by omission). (Wardle and Derakshan 2018:5)
1610703060160.png

Makao Makuu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Mwenge, Dar es Salaam

F. KIAMBATANISHO CHA BARUA ILIYOANDIKWA NA ASKOFU BAGONZA

Mheshimiwa Rais JPM,
Karibu Sana Bukoba.

Bukoba ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Zamani uliitwa [Mkoa wa] Ziwa Magharibi. Huu ni mkoa wenye historia ya mambo mengi. Kitaifa [Mkoa wa Kagera] ni nyumbani kwa [watu wanajitambua na kujitambulisha kama wasomi kwa kutumia neno maarufu la] "Nshomile". Hii ndiyo sababu ya makaribisho yangu [kwako Mheshimiwa Rais JPM].

Shule ya Ihungo inayopokelewa leo [na Rais Magufuli kutoka kwa mkandarasi] inapendeza. Lakini pia shule hiyo imebeba historia tukufu ya Mkoa huu [wa Kagera]. Wasomi wengi wamepita hapa. Ikiwa ni sehemu ya BUIKANO (Bukoba Seco, Ihungo, Kahororo, Nyakato na Omumwani), shule [hii] … pamoja na ile ya wasichana ya Rugambwa [vilikuwa vitovu vya] kuandaa wasomi wa Taifa hili kabla na baada ya Uhuru.

Mpendwa Rais, shule za sekondari tunazo za kutosha [mkoani Kagera] lakini hatuna chuo kikuu. [Unaweza kudhani kwamba, vyuo vikuu vya mkoa wa Kagera vilisambaratishwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea katika miaka ya hivi karibuni].

Mkoa huu una idadi kubwa ya [watu wapatao 3,000,000 na orofha ndefu ya] maprofesa lakini hauna Chuo Kikuu hata kimoja [japo kuna jitihada kubwa ambazo zinafanywa ili kujenga vyuo vikuu mkoani humu]. [Kwa mfano,] akina Profesa Teddy Maliyamkono na wenzake walianzisha University of Bukoba [lakini] "ikafwariki baadaye".

KKKT ikaanzisha Josiah Kibira University College (JOKUCO) ikafungwa [na serikali] baadaye. TEC ikaanzisha Cardinal Rugambwa University (CARUMCO) ikafungwa [na serikali] na kuacha maumivu. Dayosisi ya Karagwe (KKKT) ikajenga Karagwe University College (KARUCO) [lakini] haijasajiliwa mpaka leo.

[Kuna] wazushi wanadai [kwamba KARUCO] haijasajiliwa kwa sababu Askofu [Bagonza ambaye ni mwanzilishi wa KARUCO] ana mdomo [mrefu]. Hawa ni waongo. Kwani wale Maaskofu waliofungiwa vyuo kule Bukoba nao wana mdomo [mrefu] kama Askofu [Bagonza] wa Karagwe? [Jawabu ni hapana. Kwa hiyo,] wazushi hawa watafute sababu nyingine.

[Basi, nimalizie kwa kusema kuwa,] hata kama vyuo [vya Kagera] vilivyofungwa vinaweza kufunguliwa baadaye [kama serikali itaona yafaa vifunguliwe haraka kama mimi ninavyopendekeza], bado tunahitaji chuo kikuu cha umma [mkoani Kagera kwa sasa]. Chaweza kuwa tawi (constituent college) la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini [kama vile] UDSM, SUA, MZUMBE, MUHAS, nk.

Sababu [zinazokwepeka] zaweza kuwa […] zipo lakini iko [angalau sababu] moja isiyokwepeka. Mkoa huu [wa Kagera] ni [ukanda] wa "Nshomile". Bila chuo kikuu [Nshomile] tunakuwa wanyonge [kielimu wakati majirani zetu ndani na nje ya Tanzania wanazidi kupaa].

[Kuhusu hoja hii] naweza kupingwa [na] hata wana Kagera wenyewe. [Lakini haya] ni mawazo yangu nao wana [mawazo] yao. [Mawazo] ya kwangu yakikubalika, [tukalikumbuke] Tetemeko la Ardhi [lililotokea Kagera hivi karibuni] kupitia [jina la] chuo hiki [ninachokipendekeza].

[Napendekeza kwamba, chuo hiki] kinaweza kuitwa "Tetemeko University of Bukoba" na kiwe na Idara ya Jiolojia (Geology) ili mtani wangu Prof. Muhongo akimaliza ubunge aje kufundisha pale na kutuonyesha Tetemeko jingine linakuja lini.

NYEGERA WAITU OMUKUNILWA,
[KARIBU NDUGU MHESHIMIWA]
KALIKAWE LWAKALINDA BAGONZA.

1611072667126.png

Baadhi ya Kozi zinazofundishwa kwa sasa katika chuo cha KARUCO, Karagwe
 

Attachments

  • 1611069313914.png
    1611069313914.png
    96.8 KB · Views: 5
makala ya kisomi zaidi

Walengwa wakuu wa bandiko hili ni wasomi ambao ni wasomaji wa mtandaoni, hasa wenye average concentration capacity ya kusoma andiko la maneno 2000.

Tatizo linalojadiliwa hapa, yaani uanzishwaji na uendeshwaji wa vyuo vikuu, ni ajenda ya kisomi zaidi.

Lakini, kila msomaji anayetaka anakaribishwa kusoma.

JF inaruhusu andiko lenye maneno hadi 10,000.

Tatizo liko wapi?
 
Tatizo Kagera matapeli wanatapeliana hata wao.

Kagera ina retired professors wengi mno kuanzisha university bora hata kuliko UDSM kwao wala sio issue.

Nimuulize Askofu Bagonza wazo na pesa za kuanzisha Bukoba university watu walizochanga viliishia wapi tuanzie hapo.

Wana kagera walikuwa committed wa ndani na nje ya nchi wazaliwa kagera hasa kuanzisha private university bora Africa Mashariki yaliishia wapi hadi leo alilie serikali? Tunaomba mrejesho wa Bukoba University.
 
Walengwa wasomi, na tatizo ni la kisomi.
Inafanywa tu ya kisomi bure. Haya ni mambo ya kawaida. Tatizo la wasomi wetu akiwemo mleta bandiko neno la kiingereza uliita la kitaalamu. Waraka umeandikwa na msomi ambaye sina shaka naye. Hakuwaandikia wasomi bali wasomaji. Tena wasomaji wa mitandaoni.

Kuanzisha chuo kikuu si suala la kisomi. Huo usomi unapatikana ndani ya hicho chuo. Tena kwa Tanzania ndio kabisa. Musukuma kwa hela yake anaweza kuanzisha chuo kikuu bila kokoro. Akaajiri maprofesa kutoka popote duniani. Lakini thubutu yake Teddy. Atakutana na vikwazo hadi kusalimu amri.

Mleta bandiko amenitisha sana. Anaandika kama mhadhiri mkuda anajadili paper ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Hivyo wawezaona tofauti. Mwenye waraka msomi akiandika waraka mwepesi kwa wasomaji wa mitandaoni. Mleta bandiko akichambua kisomi kwa kulenga wasomi. Uncalled for. Na kwa ushauri wake kwa Bagonza wa kufunga mdomo kuna kitu. Kama sio superiority complex itakuwa ni malinformation au disinformation au yote mawili.

Ningefurahi kama Bagonza mwenyewe angemjibu kwa chanda chake. Akifanya hivyo nitalala usingizi mwanana. Alamsiki!

Walengwa wasomi, na tatizo ni la kisomi.
 
Inafanywa tu ya kisomi bure. Haya ni mambo ya kawaida. Tatizo la wasomi wetu akiwemo mleta bandiko neno la kiingereza uliita la kitaalamu. Waraka umeandikwa na msomi ambaye sina shaka naye. Hakuwaandikia wasomi bali wasomaji. Tena wasomaji wa mitandaoni.

Kuanzisha chuo kikuu si suala la kisomi. Huo usomi unapatikana ndani ya hicho chuo. Tena kwa Tanzania ndio kabisa. Musukuma kwa hela yake anaweza kuanzisha chuo kikuu bila kokoro. Akaajiri maprofesa kutoka popote duniani. Lakini thubutu yake Teddy. Atakutana na vikwazo hadi kusalimu amri.

Mleta bandiko amenitisha sana. Anaandika kama mhadhiri mkuda anajadili paper ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Hivyo wawezaona tofauti. Mwenye waraka msomi akiandika waraka mwepesi kwa wasomaji wa mitandaoni. Mleta bandiko akichambua kisomi kwa kulenga wasomi. Uncalled for. Na kwa ushauri wake kwa Bagonza wa kufunga mdomo kuna kitu. Kama sio superiority complex itakuwa ni malinformation au disinformation au yote mawili.

Ningefurahi kama Bagonza mwenyewe angemjibu kwa chanda chake. Akifanya hivyo nitalala usingizi mwanana. Alamsiki!

Mleta bandiko amejikita katika mahitaji ya barua ya Bagonza, ambayo sehemu yake inasomeka hivi:

[Kuna] wazushi wanadai [kwamba KARUCO] haijasajiliwa kwa sababu Askofu [Bagonza ambaye ni mwanzilishi wa KARUCO] "ana mdomo" [mrefu]. Hawa ni waongo. Kwani wale Maaskofu waliofungiwa vyuo kule Bukoba nao wana mdomo [mrefu] kama Askofu [Bagonza] wa Karagwe? [Jawabu ni hapana. Kwa hiyo,] wazushi hawa watafute sababu nyingine.

Sababu nyingine alizoziomba Bagonza sasa zimeonyeshwa, isipokuwa kama Bagonza ataonyesha kuwa sio za kweli.

Kwa hiyo, maneno yako kwamba IT IS UNCALLED FOR sio sahihi. Ukweli ni kwamba this response is called for.

Pia, hoja za mleta bandiko zinasomeka, hata kama msomaji ni darasa la saba, ilimradi awe na average concentration capacity.

Usije kufikiri kuwa wasomaji wa mtandaoni ni mbumbumbu saaaan.

Ukitofautisha mleta hoja na hoja utakuwa huru zaidi kuuona msingi wa hoja ya mleta bandiko.
 
Hakuwaandikia wasomi bali wasomaji. Tena wasomaji wa mitandaoni. Kuanzisha chuo kikuu si suala la kisomi. Huo usomi unapatikana ndani ya hicho chuo. Tena kwa Tanzania ndio kabisa. Musukuma kwa hela yake anaweza kuanzisha chuo kikuu bila kokoro. Akaajiri maprofesa kutoka popote duniani. Lakini thubutu yake Teddy. Atakutana na vikwazo hadi kusalimu amri.

Zingatia haya:

1. Hadhira ya bandiko hili ni wasomaji wasomi wa mitandaoni zaidi wenye average concentration capacity

2. Kauli unayoitetea na ninayoipinga ni hii: Kuanzisha chuo kikuu si suala la kisomi. Uandishi wa mpango kazi wa kuanzisha na kuendesha chuo haufanywi na Msukuma wa madongokuinama. Usomi unahitajika tangu mwanzo, ama kupitia kichwa cha mwekezaji au kichwa cha mtaalam mshauri.

3. Kuhusu vikwazo alivyokutana navyo Teddy sijatafiti. Nahimiza utafiti ufanyike ili ukweli ujulikane, lakini hiyo sio sehemu ya mada ya bandiko hili
 
Mleta bandiko amenitisha sana. Anaandika kama mhadhiri mkuda anajadili paper ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. Hivyo wawezaona tofauti. Mwenye waraka msomi akiandika waraka mwepesi kwa wasomaji wa mitandaoni. Mleta bandiko akichambua kisomi kwa kulenga wasomi. Uncalled for.

Nakataa dhana yako.

Ni kweli mwandishi wa waraka ni msomi aliyewaandikia waraka mwepesi wasomaji wa mtandaoni

Lakini sio kweli kuwa wasomaji wa mitandaoni ni mbumbumbu au kwamba wanastahili kulishwa half baked arguments.

Ni kweli, mleta bandiko amechambua kisomi kwa kuwalenga wasomi ambao ni wasomaji wa mtandaoni.

Lakini, andiko haliwabagui wasomaji wa kawaida wenye uwezo wa kusoma maneno 2000 na kuelewa hoja.

Lakini Kwa nini mleta bandiko amejielekeza zaidi kwa hadhira ya wasomi ambao ni wasomaji wa mtandaoni?

Jawabu:

Mwandishi wa waraka aliamua kwa makusudi kuacha taarifa muhimu kwapani mwake, kiasi cha kuwafanya wasomaji wake wapotoke bila kujua kwamba wamepotoshwa kwa kunyimwa taarifa muhimu.

Mapingamizi matatu aliyoacha bila kuyajibu, ni vigumu kugunduliwa na wasomaji wa kawaida, na hasa:

-- wasiojua kanuni za kuchambua na kutathmini hoja (argument analysis and evaluation) zilizotumiwa na mleta bandiko.

-- wasiojua masharti ya usajili wa vyuo vikuu kupitia TCU

-- wasiojua masharti ya kutoa mikopo ya elimu kupitia HESLB

--wasiojua masharti ya kudahiliwa kwa wanafunzi wa vyuo kupitia TCU

-- wasiojua masharti ya ajira za walimu wa vyuo vikuu chini ya usimamizi wa TCU

Kwa kuibua mapingamizi haya bandiko hili limeonyesha matobo ya kweli yanayopaswa kuzibwa na mwandishi wa waraka.

Tena, bandiko limeandikwa kwa nia njema, kama msomaji akitofautisha mwandishi na maandiko.

Hivyo, mwandishi wa waraka akiyafanyia kazi mapendekezo atafaidika na kina Nshomile wake, japo nasikia yeye sio Nshomile.

Soma tena hoja za bandiko.
 
Mleta bandiko amenisaidia zaidi kuielewa barua ya Bagonza labda bila mleta bandiko ingeniwia vigumu kujua hila za hali ya juu walizotumia serikali kusababisha vyuo vingi kufwa
 
Mleta bandiko amejikita katika mahitaji ya barua ya Bagonza, ambayo sehemu yake inasomeka hivi:

Pia, hoja za mleta bandiko zinasomeka, hata kama msomaji ni darasa la saba.
Ukitofautisha mleta hoja na hoja utakuwa huru zaidi kuuona msingi wa hoja ya mleta bandiko.
Nashukuru kwa kukubaliana na mimi. Hakuna cha walengwa wasomi wala suala la kisomi. Ushauri wako wa kutofautisha mleta hoja na hoja naukubali. Msikilize mlevi pia kuna siku anatapika mantiki badala ya mataputapu. Na saa mbovu kuna wakati ikaonyesha majira sahihi!

Lakini kuna wakati inasaidia sana kumwelewa mleta hoja ili uelewe hoja. Kwa bandiko hili mleta hoja amekuwa akijisaliti mwenyewe. Kiasi nikakumbuka bandiko lake jingine kuhusu wale covid-19 wa Chadema. Usomi mashaallah. Pia wapo sycophantic intellectuals. Tanzania ya leo tunao idadi ya kutisha. Bwashee asema: Asha tu!
 
kuna wakati inasaidia sana kumwelewa mleta hoja ili uelewe hoja.

Tangu enzi za Galileo kanuni za makabiliano ya kimantiki (rules of intellectual engagement) haziruhusu jambo hilo tena, labda kama mtu bado anaishi zama za mawe

Kutofautisha hoja na mleta hoja kunatusaidia kupinga hoja za mfalme, papa, kardinali, askofu, padre, baba, mama, lakini bila kumpinga yeyote kati ya hawa.
 
Mleta bandiko amenitisha sana. Anaandika kama mhadhiri mkuda anajadili paper ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza.

Alichofanya mleta bandiko ndivyo CRITICAL DISCOURSE ANALYSIS inafanyika.

Unashauriwa kuanza kuizoea.

Jielimishe kidogo juu ya haya:

- argument structure analysis

- argument evaluation/critique

- conceptual framing

- semiotic analysis

etc etc
 

Elimu ya makaratasi ni bure kabisa,
Kujiona unshomile ndio umewaponza,mji uko duni wametanguliza much knowing kila mtu
Siku moja tumekaa kijiweni watu watano. Tunaongea hili na lile. Mmoja wetu akasema: Mnajua mimi sikusoma lakini mambo yangu supa. Nilishangaa sana. Supa anaongelea chumba kimoja na bodaboda boxer. Aliuza shokora alilopewa na marehemu babu yake.

Mexicana ana elimu ya mavyuma. Hakusoma. Elimu haijamponza. Yupo yupo kama hayupo. Mji wake supa. Mipango miji ni watoto wa chekechea!

Siwezi endelea. Naishia hapa. Kichefuchefu. Huyu naye great thinker!
 
Back
Top Bottom