ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 59,064
- 69,741
Habari zenu ndugu,
Kutoka Dar, askari wa JWTZ apandishwa Kizimbani Kwa Kukaidi Amri Halali ya Askari Trafiki wakati akitekeleza Wajibu wake.
Hii safi sana, lazima ieleweke kwamba utii wa Sheria bila shurti ni Kwa Kila raia bila kujali hadhi wala vyeo.
Askari Jeshi hasa JKT mara nyingi Huwa wanapiga raia hivyo na kujifanya wao wako Juu ya Sheria na Wana Haki sana kuliko raia wengine.
Kazi iendelee
==============
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kukataa amri halali ya askari wa usalama barabarani.
Imedaiwa Mahakamani leo, kuwa MT 89487 CPL Hamis Ramadhan alishindwa kusimamisha gari yake katika kivuko cha watembea kwa miguu eneo la Mlimani City, barabara ya Survey.
Wakili wa Serikali, Vailet Kyendesa ameiambia Mahakama kuwa Ramadhani akiwa akiiendesha gari binafsi T 433 ALB Nissan Patrol alikaidi amri ya kusimamisha gari na kujaribu kumsukuma askari wa usalama barabarani kwa gari lake.
Mshitakiwa amekana mashitaka na upande wa mashitaka umedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
#HabarileoUPDATES