Askari Polisi kutoka Ukanda wa Mashariki mwa Afrika wametakiwa kujiweka imara katika kukabiliana na uhalifu

John Walter

Member
Aug 14, 2017
68
63
inbound2797349761755508610.jpg

Askari Polisi kutoka Ukanda wa Mashariki Mwa Afrika wametakiwa kujiweka imara katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza Aprili 17, 2024 wakati akifunga rasmi zoezi la utayari FTX USALAMA PAMOJA2024 lililofanyika katika Shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani Kilimanjaro Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb) amewataka kwenda kufanyia kazi yale yote waliyojifunza katika kipindi chote walichokuwa wakitekeleza mazoezi mbalimbali chuoni hapo.

"Nimejionea hapa mbinu mbalimbali mlizojifunza na kuelekezwa ambazo zitakuwa nyenzo nzuri katika kupambana na uhalifu pamoja na matukio mengine basi niwatake nyote kwenda kufanyia kazi yale yote mliyojifunza na kuelekezwa katika mazoezi yenu chuoni hapa ili yakawe chachu katika kuboresha utendaji wenu wa kila siku"

Aidha, Mhe. Sillo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Marais wote wa Nchi shiriki kwa kuwezesha kufanyika kwa zoezi hilo na kuwataka washiriki kwenda kufanya utalii wa ndani kama vile kutembelea Mbuga za Wanyama zilizopo Tanzania na kupanda mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura alisema kuwa, kufanyika kwa zoezi hilo la utayari kutachochea kuongeza hali na morali kwa Askari katika kukabiliana na makosa mbalimbali ya uhalifu.

Akizungumzia umuhimu wa zoezi hilo IGP Wambura alisema kuwa, litawezesha kupima utayari wa Askari, kuongeza maarifa pamoja na kuimarisha uhusiano na mashirikiano.

Vilevile Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Burundi Meja Jenerali Fredric Budomo alisema kuwa kufanyika kwa zoezi la utayari nchini Tanzania ni miongoni mwa mafanikio makubwa hasa katika eneo la kuongeza maarifa katika kuukabili uhalifu wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom