Askari polisi Arusha wadaiwa kukamatwa na Mirungi waliyopewa rushwa. Wapo Lokapu wakisota. RPC adai hana taarifa

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
93
288
ASKARI Polisi Wawili wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Wanashikiliwa katika mahabusu ya polisi jijini hapa kwa zaidi ya wiki tatu rumande kwa madai ya kupokea rushwa ya shilingi milioni 4 kutoka kwa Wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya Mirungi waliokuwa wakiingiza bidhaa hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 kutoka Nchi jirani ya Kenya.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi la Polisi zilidai kuwa askari hao baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao wakiwa na kiasi hicho cha Mirungi licga ya kupokea kitita cha sh,milioni 4 za rushwa pia waliwapokonya dawa gizo za kulevya na kuondoka nazo.

Inadaiwa kuwa askari hao bila kuwa na woga waliamua kwenda kuuza dawa hizo wenyewe kwenye vijiwe mbalimbali vya wala mirungi ndani ya Jiji la Arusha.

Polisi hao{majina tunahifadhi kwa sasa} walikamata Mirungi katika barabara ya Namanga –Arusha eneo la Ngaramtoni februali 3 mwaka huu majira ya saa 7 mchana na waliomba kiasi cha rushwa ya shilingi milioni 4 ili kuachia bidhaa hiyo haramu.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya jeshi la polisi vilisema kuwa Askari mmoja ambaye kituo chake cha kazi ni wilayani Arumeru na mwingine kituo chake cha kazi ni uwanja mdogo wa Ndege wa Kisongo walipewa kiasi hicho cha fedha na wafanya biashara hao kwa makubaliano ya kuachiwa dawa hizo za kulevya.

Taarifa zaidi za ndani kutoka katika jeshi hilo zilisema kuwa mara baada ya kupokea kiasi hicho cha pesa askari hao waliwageuka wafanyabiashara hao na kusema kuwa mzigo wote wa dawa hizi za kulevya utakuwa chini yao na waliwaamuru kutoweka haraka vinginevyo na wao watakamatwa na kuswekwa rumande.

Habari ziliendea kusema kuwa hatua hiyo haikuwafurahisha wafanyabiashara hao na kuamua kutoa taarifa kwa viongozi wa juu wa polisi Arusha{majina tunayo} ambao ni washirika wa wafanyabiashara hao na kuwekwa mtego wa kuwakamata.

Vyanzo ndani ya Polisi Arusha vilisema kuwa mtego huo uliwanasa askari hao februali 4 saa 4 asubuhi walikamatwa wakiwa na mzigo katika gari na kupelekwa moja kwa moja katika kituo Kikuu cha Polisi Arusha ambapo waliwekwa mahabusu na hadi leo bado wanasota humo.

Taarifa iliendea kusema kuwa jalada la uchunguzi dhidi ya askari hao lilifunguliwa na linachunguzwa na ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Arusha{OC CID} kupitia makachero wa Ofisi hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Arusha,Justin Msejo alipoulizwa juu ya hilo alidai hana taarifa ila akizipata atatoa taarifa.

Matukio ya askari kujihusisha na utovu wa nidhamu jijini Arusha na baadaye askari hao kuachwa waendelee na kazi ni jambo ambalo limekuwa likiwakera baadhi ya askari ndani ya jeshi hilo ambao wamekuwa wakilalamika kuwa RPC Arusha anawakumbatia na baadhi yao anawafukuza hasa wanaoshindwa kumwona kikubwa.

Mmoja ya askari hao jina linahifadhiwa,alidai kuwa miongoni mwa askari waliokamatwa kwa kosa la kumbambikiza meno feki ya Tembo, Profesa Justin Maeda mkazi wa Usa River na kumpora sh,milioni 100 waliachiwa na baadhi yao walifukuzwa kazi na wengine walirejeshwa kazini na kupandishwa cheo jambo ambalo alidai ni upendeleo umetumika.

"Unajua RPC wetu ameanza kutumika vibaya kuna askari wakubwa anakula nao hasa wapofanya matukio ya kihalifu lakini sisi wadogo ndio tunafukuzwa kila siku hii haikubaliki lazima IGP alione hili maana kuna taarifa hata hawa waliopo Lokapu wanaweza wasifukuzwe kazi "

Hata hivyo matukio ya rushwa kwa askari polisi Arusha yamekuwa yakiendelea kushika kasi lakini jeshi hilo Arusha limekuwa likishindwa kutoa taarifa kwa wakati na kufikia hatua baadhi ya wananchi kuona kuwa jeshi hilo limekuwa likilindana na kufichiana maovu dhidi askari wakware.

images.jpg
 
Back
Top Bottom