Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia askari wa jeshi la wananchi Tanzania, (JWTZ), wilayani Monduli kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mfugaji, Laisi Lemomo(26)Mkazi wa Kijiji Cha Lashaine wilayani Humo.
Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi Mkoani hapa, Justine Masejo alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi Julai 12 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji hicho.
Alisema kuwa chanzo Cha tukio hilo bado kinachunguzwa baada kikosi Cha askari wa upelelezi kutoka makao makuu ya jeshi hilo Mkoani Arusha kutumwa eneo la tukio na kwamba taarifa zaidi juu ya tukio hilo zitatolewa hapo baadaye.
Wakati huo huo jeshi la polisi Mkoani hapa linamshikilia mganga wa kienyeji, (jina lina hifadhiwa) Mkazi wa Sombetini jijini Arusha anayedaiwa kumshawishi mtuhumiwa wa mauji ya Mtoto mwenye umri was miaka minne ambaye Julai Sita mwaka huu mwili wa Mtoto huyo ulikutwa kwenye shamba la Mikahawa eneo Burka jijini hapa ukiwa umetelekezwa.
Kamanda Masejo, alifafanua kwamba mwili wa marehemu wenye jinsia ya kiume ulikutwa na majeraha ya kipigo na kuzibwa mdomo na majani ya miti huku mtuhumiwa wa ukatili huo (jina linahifadhiwa) akidaiwa ni baba wa kufikia wa marehemu ambaye alikuwa akiishi naye.
Alisema kwamba mtuhumiwa huyo Mara baada ya kukamatwa na kuhojiwa alikiri kutenda unyama huo na kumtaja mganga huyo wa kienyeji kuwa ndiye aliyemshawishi kutenda tukio hilo kwa lengo la kumaliza kesi zake zinazomkabili mahakamani pamoja na kunyosha mambo yake ya kibiashara.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Mara baada ya upelelezi was jeshi la polisi kukamilika.
Ends...