- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kuna utafiti unasambaa Mtandaoni ukionesha Asilimia 80 ya watanzania wanaishi na maambukizi ya VVU.
Ni kweli?
Ni kweli?
- Tunachokijua
- Kumekuwepo chapisho linaloitwa "Sexual Behaviors and HIV Status: A Population-Based Study among Youths and Adults in Tanzania" lililochapishwa na mhariri wa jarida la 'Journal of Infectious Disease and Epidemiology Volume 7 | Issue 8' DOI:10.23937/2474-3658/1510224 la mwaka 2021 linalosambazwa katika mitandao ya kijamii ambalo pamoja na mambo mengine limedai kuwa 80% ya watanzania wanaishi na Virusi vya UKIMWI.
Andiko halisi la Utafiti huu limehifadhiwa hapa.
Aidha, baadhi ya watu kwenye Mitandao ya kijamii wamechapisha utafiti huu wakijaribu pia kuonesha takwimu zilivyo kwa Tanzania. (Hapa)
Takwimu hizi zina Ukweli?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini takwimu hizi hazina ukweli.
Taarifa sahihi za kitafiti kwa kipindi tajwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu lilionyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kilikuwa asilimia 4.9 tu. Aidha, kiwango cha maambukizi kimeshukia zaidi hadi kufikia asilimia 4.4% mwaka 2022-2023. (hapa)
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakinzana pia na kile kilichochapishwa kwenye utafiti huu. Kwa mujibu wa WHO, takriban watanzania Milioni 1.7 pekee ndiyo wanaishi na VVU. Pia, takwimu za taasisi ya NACP zinaonesha maambukizi yapo kwa 4.7%.
Aidha, takwimu zingine za Taasisi ya USAID za Juni 2023 zinaonesha kiwango cha mamambukizi ya VVU nchini ni 4.5%.
Wizara ya Afya yatolea ufafanuzi
Kutokana na sintofahamu iliyozuka mtandaoni baada ya kusambaa kwa utafiti huu, Wizara ya Afya ilikanusha takwimu zilizotolewa, ambapo pamoja na mambo mengine Wizara ilichukua hatua kwa kuwaandikia na kuwataka waandaji wa chapisho hilo kufuta andiko hilo (article retraction) pamoja na kuwasiliana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya Connecticut, Marekani juu ya upotoshaji huu uliofanywa na mwanasayansi ambaye ni mwajiriwa wao. (Hapa)
Pia, Wizara ilisema Waandaaji wa chapisho hilo hawajawahi kufanya tafiti nchini Tanzania na wamekiuka miiko na taratibu za mawasilisho ya kisayansi, ambayo yanawalazimu kufanya ushirikishwaji wa wanasayansi wa nchi husika wanapoandaa na kuchapisha mawasilisho ya kisayansi.