DOKEZO Arusha: Wananchi wadai kutozwa Sh. 2,000 ili wapite barabarani Arumeru, wawekewa kizuizi chenye misumari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,642
6,324
Watumiaji wa barabara iliyopo Kata ya Oldonyowasi, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, wamedai kuwa wakiwa wanapita na usafiri wa magari na pikipiki katika barabara hiyo wamekuwa wakitozwa shilingi elfu mbili (2,000) kwa kila siku ya jumamosi na kuelezwa kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya ukarabati wa barabara hiyo.

Inaelezwa kuwa siku ya jumamosi ni siku ya soko katika eneo hilo, hivyo wakusanyaji wamelenga kukusanya fedha hizo katika siku hiyo ili kupata fedha nyingi kulingana na idadi kubwa ya watu wanaoelekea sokoni.

Aidha, GADI TV imezungumza na wanaoratibu zoezi hilo, na wamedai kuwa zoezi la ukusanyaji wa fedha hizo ni jambo lakawaida licha ya kwamba hawatoi risiti.

Kadhalika, tumemtafuta Mkuu wa wilaya ya Arumeru ndugu Amiri Mkalipa ili tuweze kufahamu iwapo kama analifahamu zoezi hilo na haya hapa ndio yalikuwa mazungumzo yake....

Kwa upande wa Uongozi wa TARURA wilaya ya Arumeru umedai kushtushwa na tukio hilo na umesema hautambui chochote kuhusiana utozwaji wa fedha hizo

Hata hivyo, Diwani wa kata hiyo bwana Kijana Mollel amesema utaratibu huo niwa uongozi wa kijiji husika na hayupo tayari kuingilia jambo hilo kwakua hajaletewa malalamiko yeyote.

Chanzo: GADI TV
 
Hayo mambo vijijini ni common sana na ndio Ile utaona wananchi wamejenga zahanati au shule kwa nguvu zao
Na hiyo ndio nguvu zenyewe
 
Wazo ni zuri kwakuwa ni kweli barabara inatumika , ina haribika na inahitaji ukarabati.

Ila tatizo sasa ni uwazi kwenye matumizi ya hizo fedha.

Raia wamekuwa wakali kwakuwa labda wahusika wanazitumia kinyume na malengo.
 
Back
Top Bottom