Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 38
- 94
Wananchi wa Mtaa wa Murieti, Kata ya Murieti, jijini Arusha wamefunga barabara ya kuelekea Intel kwa zaidi ya saa tatu siku ya Jumatatu Desemba 16, 2024, wakishinikiza serikali kutengeneza barabara ya Kimara Mwisho hadi Kwa Patel ambayo imeharibika vibaya na kujaa mashimo yenye maji machafu.
Wananchi hao wamesema hali hiyo imewafanya washindwe kupita kwa urahisi kwenda kutafuta riziki yao ya kila siku, huku wakilalamikia athari za kiafya na kiuchumi zinazotokana na miundombinu hiyo duni.
Katika hali ya taharuki, Diwani wa Kata ya Murieti, Mariety Mbise, pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa walifika eneo hilo kutuliza wananchi. Hata hivyo, wananchi hao waliwakaribisha viongozi hao kwa kuwashinikiza wapite kwenye madimbwi hayo ya maji machafu ili kushuhudia changamoto wanazopitia.
Wananchi wa Murieti wamesema kuwa wamekuwa wakitoa kilio kwa muda mrefu kuhusu hali ya barabara hiyo bila mafanikio, na hatua ya hivi karibuni ni kuonesha kukata tamaa kwao na kushinikiza hatua za dharura zichukuliwe.
Diwani Mariety Mbise ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha barabara hiyo inafanyiwa matengenezo ya haraka ili kurejesha hali ya kawaida.