Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,366
3,787
Wakuu,

Hawa ndio wahuni waliotajwa kupachikwa CHADEMA kufanya hujuma Uchaguzi Serikali za Mitaa!

Kaka anapayuka kwelikweli kumbe sio siyo mgombea aloyekutana na kashkash za kukatwa majina🤣🤣😂😂 sasa analalamika kuonewa wapi? :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Angalia video hapo ucheke na wewe.

Mpo salama wanajukwaa?

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha wamejikuta wakiingia kwenye mgogoro mkubwa uliosababisha kurushiana maneno makali na hata ngumi, muda mfupi baada ya mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama hicho Benson Kigaila na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Rose, Novemba 13, 2024.

Mashuhuda wameripoti kuwa vurugu hizo zilianza majira ya saa 12:30 jioni na ziliendelea kwa takribani saa moja. Wanachama hao walionekana wakirushiana lawama huku wakidai kuwa walishambuliwa na vijana wa hamasa wa chama hicho.

"Tumeshambuliwa na vijana wa hamasa bila sababu yoyote ya msingi," ameeleza mmoja wa wanachama, ambaye alisisitiza kuwa tukio hilo limeleta mgawanyiko ndani ya chama.

Mbali na malalamiko ya kupigwa, baadhi ya wanachama hao walimtupia lawama nyingi Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, wakimtuhumu kuwa na mienendo inayowakatisha tamaa ndani ya chama. Wamesema kuwa mienendo hiyo imekuwa chanzo cha migogoro na kutokuelewana miongoni mwa wanachama.

Pia soma: Wanachama wa CHADEMA Katavi wachapana makonde, Mbowe ashutumiwa kugawa pesa kwa wajumbe

Chanzo: Jambo TV
 
View attachment 3151765

Chanzo: Jambo TV
Chadema ni Gen - Z.
Hayo ni mambo ya kawaida .
 
..

..Chadema wako imara, na wana uchungu na chama chao, ndio maana ngumu zinatembea.

..Na siku Polisi wakiacha kuwalinda Ccm lazima watachezea kichapo toka kwa Chadema.
Nyumbu hovyo sana, wanaparuana wenyewe kwa wenyewe ila wakiambiwa kuandamana kila mmoja anajifanya siyo mwànachadema.
 
Back
Top Bottom