Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 970
- 2,559
Wakati taifa likiwa linaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi Novemba, Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo amemuahidi Rais Samia kutumia viongozi watakaochaguliwa na wananchi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kama Jeshi la kumtetea Samia kwenye uchaguzi mkuu.
Soma pia: Ruvuma: Rais Samia asema wananchi wasifanye makosa Uchaguzi Serikali za Mitaa, rangi za kuchagua ni Njano na Kijani
Akiwa anazungumza na Rais Samia kwa njia ya simu wakati wa mkutano, Gambo alimshukuru Rais Samia kwa kazi yake kubwa aliyoifanya katika mkoa huo na kuongeza kuwa wataenda kuilinda mitaa yote ili wenyeviti watakapopatikana watumike kama jeshi lake kwenye uchaguzi mkuu wa 2025
"Mheshimiwa Rais tukuhakikishie kwamb sisi tuko na wewe leo mpaka mwaka 2030. Na namna ya kukuonesha kwamba tunakuunga mkono kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka huu 2024"
"Tutakwenda kuilinda mitaa yote ili wenyeviti wa mitaa watakaopatikana wawe ni jeshi lako kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025"
Source: Jambo TV Youtube