Huyu meneja katika huu mgawo wa umeme anabagua maeneo kulingana na hali ya watu wanaoishi eneo husika.
Anaongozwa na wenye hela anapewa rushwa. Unakuta eneo linakatwa kwa wiki nzima jioni, kwa mfano kuanzia Usa-River mpaka King'ori ni wiki sasa umeme unakatwa kila ikifika saa 12 jioni.
Jioni kuna mambo mengi ya kufanya ikuwepo kupata taarifa za habari kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na kwingineko duniani.
Kwanini ugawaji usiwe fair, kwamba leo ukikata asubuhi, kesho unakata jioni. Hakuna ambacho hamuelewi ila mnakula rushwa.