Arusha: Genge la ulipuaji mabomu na umwagiaji watu tindikali lanaswa na Polisi

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,973
9,572
Wakuu,

Arusha imekuwa katika hali ya kutatanisha katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya ajabu hasa milipuko ya mabomu ya hivi karibuni.

Habari njema leo ni kwamba jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni Kijana mmoja ambaye ni mkazi mgeni katika mtaa wa Osunyai kata ya Sombetini leo, amekutwa na mabomu 7 na tindikali, mapanga, majambia, risasi na silaha nyinginezo. Amekamatwa na yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi. Wanaendelea kumpekua nyumbani kwake.

Tutaendelea kuwajuza kila kinachojiri.

========
UPDATE:

JESHI la Polisi jijini Arusha limewakamata watu 16 akiwemo Imam wa Msikiti wa Al Quba uliopo mkoani Arusha, Jafar Lema na mfanyabiashara 1 wote wakihusishwa na matukio ya ulipuaji wa mabomu jijini Arusha.

Bunduki-Risasi-Mabomu-Arusha-Shoka.jpg

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai nchini (DCI), Issaya Mungulu, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Arusha leo, Jumanne Julai 22, 2014 imedaiwa kuwa Julai 21, 2014 saa 20.00 usiku katika maeneo ya Sombetini, Jeshi hilo limewakamata Yusufu Ally (30) na mkewe Sumaiya Juma (19) wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono Saba (7), risasi sita za bunduki aina ya shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja.

Mungulu amenukuliwa na FikraPevu akisema kuwa Yusufu ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha na kuwa mahojiano juu ya mtuhumiwa bado yanaendelea dhidi yake.

Aidha, amesema uchunguzi wa shauri hilo pamoja na matukio mengine ya milipuko yanaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa polisi na kuwakamata watakaobainika kuhusika na matukio hayo.

Mtuhumiwa mwingine wa milipuko nchini asakwa na Polisi

Hata hivyo, Jeshi hilo limesema linamtafuta, Yahya Hella (33) mkazi wa Mianzini mkoani humo, mwenyeji wa Chemchemu, Kondoa – Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini.

"Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu na pia nipende kuwashukuru sana wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa jeshi letu hapa nchini" alisema Mungulu.

Watuhumiwa wengine kufikishwa mahakamani

Amesema kufuatia tukio la mlipuko wa bomu Julai 7, 2014 saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa vibaya, Jeshi hilo limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi na kuwa kati yao watu sita watafikishwa Mahakamani mapema iwezakanavyo.

Amewataja watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo kuwa ni pamoja na Shaaban Mmasa (26) ambaye ni mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo, Athuman Mmasa (38) na Mohamed Nuru (30), wote walinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la Gymkhana jirani na eneo la tukio.

Wengine ni Sheikh Jaffar Lema (38) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet katika wilaya ya Arumeru, pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha ambaye ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo balimbali nchini, Abdul Salim (31), wakala wa Mabasi Stendi Arusha, na Said Temba(42), mfanyabiashara wa Arusha.

Soma zaidi: Arusha: Genge la ulipuaji mabomu na umwagiaji watu tindikali lanaswa | FikraPevu
 
Wakuu,
Arusha imekuwa katika hali ya kutatanisha katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya ajabu hasa milipuko ya mabomu ya hivi karibuni.
Habari njema leo ni kwamba jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni Kijana YUSUPH ALLY ambaye ni mkazi mgeni katika mtaa wa Osunyai kata ya Sombetini leo, amekutwa na mabomu 7 na tindikali, mapanga, majambia, risasi na silaha nyinginezo. Amekamatwa na yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi. Wanaendelea kumpekua nyumbani kwake.

Tutaendelea kuwajuza kila kinachojiri.
Mungi, waweza kufafanua hapo kwenye 'mkazi mgeni'..?
 
Mkuu kuta ni ya mkenya wa muvi ya kwa kova.

Sina hakika kama diye mhusika
 
Kumekuwa na taarifa kwamba kuna vijana wanasafirishwa kwenda somalia kujifunza ugaidi na Alshabab, RPC na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama watuambie kuhusi intelijensia yao kutokana na hizi taarifa pamoja na milipuko ya mabomu.

IGP aliwahi kusema kuwa FBI walifika Arusha, mpaka leo hatujasikia ripoti yao.

Suala sasa la kujiuliza kama mtanzania ni je, haya mabomu yanapitia wapi? Rada yetu ipo? Inafanya kazi?

Usalama wa nchi ufanye majukumu yake iache siasa nchi iko hatarini
 
Wakuu,
Arusha imekuwa katika hali ya kutatanisha katika kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya ajabu hasa milipuko ya mabomu ya hivi karibuni.
Habari njema leo ni kwamba jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni Kijana YUSUPH ALLY ambaye ni mkazi mgeni katika mtaa wa Osunyai kata ya Sombetini leo, amekutwa na mabomu 7 na tindikali, mapanga, majambia, risasi na silaha nyinginezo. Amekamatwa na yuko chini ya ulinzi wa jeshi la polisi. Wanaendelea kumpekua nyumbani kwake.

Tutaendelea kuwajuza kila kinachojiri.

Hatimaye akili imeanza kurudi polisi. ee Mungu tulelee mtoto huyu wa ardhi yetu tunayoipenda sana; mpe mtoto huyu maisha marefu, mpe hekima, busara na ufahamu utokao kwako tu wewe Mungu wetu muumba wa ardhi na vyote vilivyopo humo.
DCIMNGULU.jpg
 
Usije kukuta huu ni mchezo wa kuigiza kwamba huyo ameandaliwa ili akamatwe na hivyo vitu na baadae itangazwe kwamba ametumwa na anamiliki hivyo vitu kwa niaba ya CHADEMA. Msianze kuisifia mvua kabla haijawanyea.

Stay tuned.

Tiba

Uko sahihi mkuu............. hapa ndipo usalama utakapojiweka kwenye aibu na kujivua nguo, kwakuwa wanaolinda mipaka ya nchi yetu ni usalama wa taifa, chadema haina serikali. Kama inaweza kuingiza vitu vya hatari namna hii basi ccm iondoke tu madarakani kabla hata ya uchaguzi.
 
Kumekuwa na taarifa kwamba kuna vijana wanasafirishwa kwenda somalia kujifunza ugaidi na Alshabab, RPC na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama watuambie kuhusi intelijensia yao kutokana na hizi taarifa pamoja na milipuko ya mabomu.

IGP aliwahi kusema kuwa FBI walifika Arusha, mpaka leo hatujasikia ripoti yao.

Suala sasa la kujiuliza kama mtanzania ni je, haya mabomu yanapitia wapi? Rada yetu ipo? Inafanya kazi?

Usalama wa nchi ufanye majukumu yake iache siasa nchi iko hatarini

Hapo kwenye red si Chenge ali make vijisenti?
 
Kama kweli kuna ugaidi basi umezalishwa na mbinu za CCM kupambana na CHADEMA Arusha na maeneo mengine.

Kwamba magaidi hao wametengenezwa na CCM kwa namna mbili.

1. Mbinu za CCM kupambana na upinzani hasa CHADEMA huku Serikali chini ya Kikwete ikishindwa kuchukua hatua. Watu sasa wenye nia mbaya wameamua kutumia upenyo huo huo.

Hivi unawezaje kumwelezea mtu makini kuwa hadi leo polisi hawajawahi hata kutoa preliminary report on Soweto incident?

2. Kazi ya system kufanya terror kwa malengo fulani ya kisiasa ambayo implications na complications zake ni hasi kwa wananchi na uchumi.
 
Kumekuwa na taarifa kwamba kuna vijana wanasafirishwa kwenda somalia kujifunza ugaidi na Alshabab, RPC na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama watuambie kuhusi intelijensia yao kutokana na hizi taarifa pamoja na milipuko ya mabomu.

IGP aliwahi kusema kuwa FBI walifika Arusha, mpaka leo hatujasikia ripoti yao.

Suala sasa la kujiuliza kama mtanzania ni je, haya mabomu yanapitia wapi? Rada yetu ipo? Inafanya kazi?

Usalama wa nchi ufanye majukumu yake iache siasa nchi iko hatarini

rada haiwezi kuona bomu mangi.
 
Back
Top Bottom