taharuki imetoka katika mtaa wa ngusero kata ya osunyai mkoani arusha baada ya vijana zaidi ya tisa wenye mapanga kudaiwa kuvamia sherehe ya ubarikio uliokuwa ukifanyika na kumkata mkono na sikio baba wa mtoto aliyekuwa akifanyiwa ubarikio.
Inadaiwa chanzo cha tukio ni dereva wa pikipiki aliebeba dawa za kulevya aina ya mirungi kuendesha kwa kasi na nusura kumgonga mtoto, baada ya kukaripiwa ndipo alipoenda na kurudi na wenzake