Arusha: Baba atafutwa na jeshi la polisi kwa kumlazimisha mwanafunzi amlawiti

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
9,398
16,463
Jeshi la polisi wilayani Arumeru, mkoa wa Arusha, linamsaka Baba mmoja ajulikanae Kwa jina la Steve, umri miaka 50 anaeishi katika kitongoji Cha olmareti katika Kijiji Cha kivulu, Kwa kosa la kumuomba mwanafunzi wa kiume wa kidato Cha tatu mwenye umri wa miaka 16 amuingile kinyume na maumbile.

Mwanafunzi huyo akieleza ilivokuwa anasema kuwa aliitwa na baba huyo wakati akipita njia ndipo alipomrubuni na kuingia nae ndani.

Anaendelea kuusema kuwa Baba huyo alimlazimisha kijana huyo amuingilie kinyume na maumbile na alifanya kitendo hicho usiku kucha kwani walianza saa nne ya usiku hadi saa kumi na Moja Asubuhi,

Mama mzazi wa kijana huyo aliyejitambulisha Kwa jina la Upendo Jackson anasema Kuna mama mmoja jirani alimuita na kumpeleka nyumbani kwa Baba huyo na kumkuta mtoto wake akiwa anatoka Bafuni ameshikilia mafuta ya kupaka huku akitembea Kwa shida ndipo alipoulizwa kulikoni ndipo baadae alieleza ukweli kuwa baba huyo alimlazimisha amuingilie kinyume na maumbile usiku kucha na kwamba sio yeye amefanyiwa Bali alikuwa anamfanyia baba huyo. Na alimtishia kuwa asikisema Kwa mtu yoyote yule basi atamkata shingo.

Mama mzazi wa kijana huyo Upendo Jackson anasema kuwa hakuamini kama mwanae hajaingiliwa na hivyo basi Kwa kushirikiana na Wamama wengine walimpeleka kijana huyo hospital kumpima kama aliingiliwa au lah ndipo majibu yalionyesha kuwa hajaingiliwa.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho anasema kuwa Baba huyo amekuwa akiishi mwenyewe na baada ya kutokea Kwa tukio hilo ametoroka na hajulikani alipo.
 
Back
Top Bottom