Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
683
1,343
Serikali yakabidhi mfano wa hundi ya shilingi bilioni 688.6 kwa kampuni ya Arab Contractor kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rufiji.

Mkandarasi ujenzi Mradi wa Maporomoko ya Mto Rufiji Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri imekabidhiwa hundi ya Bilioni 688.651 kama malipo ya awali kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Hundi hiyo imekabidhiwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James.

Akikabidhi hundi hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kwa hivi sasa nchi inajumla ya Mw 1602, hivyo kukamilika kwa mradi wa Rufiji kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Aliongeza mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja.

"Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla yake itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla" alisema Bw. James.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyimvua alisema malipo hayo ya awali ni sawa na asilimia 15.

Aliongeza, malipo yamegawanyika sehemu sehemu mbili asilimia 70 ya fedha za kigeni ambazo Amelia na asilimia 30 atalipwa baada ya kukamilisha shughuli za kimkataba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa niaba ya TANESCO ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo.

Hafla hiyo ilihudhuliwa pia na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadilifu Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka, Wakandarasi na baadhi ya wasimamizi wa Mradi wa Rufiji.

FB_IMG_1556103837938.jpeg

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA

HISTORIA
 
Miradi hii tutakuja kuichunguza maana ripoti za CAG awamu hii zinaashiria mengi yasiyofaa.

Na huu mradi tunasubiri uhamishiwe ofisi ile ambayo matumizi yake hayakaguliwa ila hii ni kinga ya muda tu.
kama hata huu hadi unaupinga sio bure kuna kitu.
 
Sijui nani katuroga.
Wengine tunawaza t. 1.5 na t.4 zimetumika vipi, wengine wanasifia t. 0.688, 06?
Safari hii ni viva wajinga, mnaonekana sana kwa awamu hii. Yaani awamu hii umetufanya tuwadharau hata wenye bonge na cheti cha elimu.
 
Back
Top Bottom