Application za mikopo onine: Wapinzani tupieni macho hili jambo, huenda ni biashara ya vigogo serikalini na inaweza kuja kuwa kashfa kubwa

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
48,967
151,060
Wapinzani, nawashauri mfanye uchunguz kuhusu hizi App hasa kujua wamiliki wa hizi applicatio za mikopo. ya online ambazo zinatumika kutoza riba kubwa ndani ya muda mfupi tena wakitumia ligha za vitisho na hata kudhalilisha wateja wao wanapochelewa kulipa kwa wakati.

Katika hii biashara, kuna uwezekano wa kuibua kashifa kubwa tu kwa vigogo wa nchi hii kwani hiwezekani watu wana-operate biashara hii kwa kutumia makampuni ya simiu ya humu nchini halafu mamlaka husika zikashindwa kuwabaini. Hii haiwzekani na haingii akilini kabisa unless kuna watu wakubwa humu nchini wanawalinda,

Maswali yakujuliza:
1. Wanaweza kutumia mitandao ya simu kufanya hii biashara pasipo kusajiliwa?

2.Wanaweza kusajiliwa kutumia menu za mitandao ya simu bila kuwa na leseni ya biashara, address ya makazi, n.k?

3. Line za simu wanazotumia hazijasajiliwa?

4. Watu hawa wanapata wapi viburi vya kusambaza sms za vitisho kwa watu bila woga?

5. Kwa maswali haya machache, hakuna uwezekano wa watu hawa kuwa wanalindwa na watu ndani ya serikali?

6. Kama serikali imeshindwa kudhibiti hizi application, je tuko salama kiasi gani kama nchi?
 
Hakuna eneo wananchi wanapigwa kama hili, mobile loan ni tatizo kubwa Tanzania na halina weledi kabisa .. Imagine mtu anakopewa pesa kiduchu riba lundo ! Wakopaji wanafedheheshwa, wanazalilishwa, wananyanyasika .. Serikali ikomeshe huu wizi, sauti zaidi zipazwe. USTAWI LOANS Mr. Finance wanaongoza kuzalilisha watanzania kupitia hii mikopo haramu.
 
Hakuna eneo wananchi wanapigwa kama hili, mobile loan ni tatizo kubwa Tanzania na halina weledi kabisa .. Imagine mtu anakopewa pesa kiduchu riba lundo ! Wakopaji wanafedheheshwa, wanazalilishwa, wananyanyasika .. Serikali ikomeshe huu wizi, sauti zaidi zipazwe. USTAWI LOANS Mr. Finance wanaongoza kuzalilisha watanzania kupitia hii mikopo haramu.
Aise,hivi wanalazimishwa kukopa au

Ova
 
Siku moja sina hili wala lile nashangaa niko kwenye group Jipya alafu lina maneno mazito ya kumkashifu mmoja ya mtu nae juaana nae kuwa NI TAPELI NA JAMBAZI HIVYO MUWE MAKINI NAE.
Ndani lina picha za jamaa na maneno makali ya kumueleza jamaa... Pia moja ya picha ni mkopo alochukua ambao alipewa wiki mbili kuurejesha.
Kilichonishangaza ni kwamba alikopa 50k wakampa 32 alafu anatakiwa kurejesha 54 ,eti hiyo 18 ni kwenye makoto alafu riba yao ni 4 tuu .. Kwa vile Watz Wengi akili zakijinga wakisikia riba ni asilimia mbili yee anaona ndogo hatizami makato.
 
Back
Top Bottom