Anthony Mtaka mbona kwa Ummy Mwalimu umenywea? Ulisema utasimamia unachokiamini

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,982
Mtaka ulitokea hadharani kupinga, kumshutumu na kumuaibisha waziri wa elimu Prof.Ndalichako kwa sababu ya kuzuia makambi.

Ukaenda mbali kwa kusema unapuuza maagizo yake na utafanya vile mkoa wa Dodoma mnataka kufanya.

Sasa hivi kauli ya Ndalichako imetolewa na Ummy Mwalimu, na kapiga marufuku hayo makambi na masomo wakati wa likizo.

Vipi mbona kimya? Unahofia nini ikiwa ulisema utasimama kutetea Jambo hilo la makambi na masomo ya ziada wakati wa likizo?
Tuseme unamhofia na kumuogopa Ummy Mwalimu?

Ule umwamba ulioonyesha wakati ule na kuwaambia wazazi wasimsikilize waziri kwa kuwa Watoto wake wanasoma shule za ada mil 10, mbona Sasa haupo?

Screenshot_20211207-132834_1.jpg
 
Sawa watoto wa mabosi mnasoma shule za international, waacheni wa shule za kayumba nao wafanikiwe,,

Watafanikiwa tu, hata mkiwawekea vizingiti
 
Tatizo anasumbuliwa na nature ya kabila lake la Wajita,amejaa majivuno sana anadhani akiwa Mkuu wa Mkoa basi yeye ndio kila kitu. Pale Magufuli alipo msifia basi anajiona yeye ndio mwenye akili kuliko watu wote.
 
Kama kuna kipindi Mtaka alichemka na kushusha heshima aliyojenga ni kipindi kile.

Kwanza alitumia lugha mbovu isiyo ya kiustaarabu

Pili alimdharau Waziri mwenye dhamana ya sera ya elimu, kwa lugha nyingine alidharau mamlaka ya juu na vyombo(establishment) vilivyo mpa mamlaka ya kusimamia sera ya elimu

Tatu alikosa busara ya kuelewa hata mazingira ugonjwa wa UVIKO aliouongelea Waziri

Nne alivunja maadili ya viongozi wa umma, alitakiwa awasiliane naye au kutoa ushauri kwa platforms zinazokubalika kiserikali badala ya kwenda public au angejiuzuru kama anaona sera ya serikali inawalakini
 
MTU Mwenye Busara na Hekima huomba msamaha.

Ndio maana baada ya kutambua kosa lake, aliomba Radhia sio tu kwa Waziri, Bali kwa Wananchi.
 
Tatizo anasumbuliwa na nature ya kabila lake la Wajita,amejaa majivuno sana anadhani akiwa Mkuu wa Mkoa basi yeye ndio kila kitu. Pale Magufuli alipo msifia basi anajiona yeye ndio mwenye akili kuliko watu wote.
Mzee mbona uko negative sana mzee...dah...mantik ya mtaka kwenye swala hilo lina makosa gani

Kama unaweza pinga hoja za mtaka kwa maandish hapa naomba ufanye hvyo na sio kumshutumu wakat hoja zake hamjajibu...naomba majibu tafadhal
 
Jamaa alijitutumua sana nikikumbuka mpaka anavua barakoa anauliza hivi mnanisikia vizuri?

Vipi hana barakoa nyingine aivue au ndio Corona imeisha?!
 
Sikio haliwez kulizd sikio bwashee
Mtaka ulitokea hadharani kupinga, kumshutumu na kumuaibisha waziri wa elimu Prof.Ndalichako kwa sababu ya kuzuia makambi.

Ukaenda mbali kwa kusema unapuuza maagizo yake na utafanya vile mkoa wa Dodoma mnataka kufanya..
 
Hivi mnachomkandia huyo RC ni nini? Kwamba ana nia ovu na agenda yake? Agenda yake haina faida kwa watoto wa walalahoi wanaosoma Kayumba?
 
Tatizo anasumbuliwa na nature ya kabila lake la Wajita,amejaa majivuno sana anadhani akiwa Mkuu wa Mkoa basi yeye ndio kila kitu. Pale Magufuli alipo msifia basi anajiona yeye ndio mwenye akili kuliko watu wote.
Mtaka ni hopelss kabisa
 
Mzee mbona uko negative sana mzee...dah...mantik ya mtaka kwenye swala hilo lina makosa gani

Kama unaweza pinga hoja za mtaka kwa maandish hapa naomba ufanye hvyo na sio kumshutumu wakat hoja zake hamjajibu...naomba majibu tafadhal
Ana hoja zipi? Haya ummy mwalimu kapiga marufuku mbona yupo kimya?
 
Hivi mnachomkandia huyo RC ni nini? Kwamba ana nia ovu na agenda yake? Agenda yake haina faida kwa watoto wa walalahoi wanaosoma Kayumba?
Sijui nia yake, Ila Mimi nimehoji tu mbona kwa Ummy Mwalimu kakaa kimya? Anamuogopa?
 
Back
Top Bottom