Anthony Joshua apoteza pambano lake dhidi ya Usyk

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,509
68,207
Hii ni baada ya kupokea kipigo cha pointi toka kwa mpinzani wake huyo katika pambano lao lililomalizika muda mchache uliopita.

Usyk toka Ukraine ameshinda kwa pointi 117-112, 116-112, na 115-113, hivyo kuondoa uwezekano wa Joshua kupambana na Tyson Fury kwa pambano la kuunganisha mikanda yote mikubwa ya uzito wa juu.

AJ anatarajiwa kutumia kipengele cha pambano la marudiano kati yake na Usyk ili kujaribu kuirudisha mikanda yake aliyoipoteza kwa bondia huyo toka Ukraine.
 
A.J alicheza kwa wakati mgumu Sana maana timing yake ni kuingia ndani.

Ila Usky hakumpa nafasi kuingia Wala kutawala, amechezea nyingi za uso na alikuwa anamhofia kabla ya pambano na upepo ulikata kama kwa Andy Ruiz Junior The Destroyer.
 
A.J alicheza kwa wakati mgumu Sana maana timing yake ni kuingia ndani.

Ila Usky hakumpa nafasi kuingia Wala kutawala, amechezea nyingi za uso na alikuwa anamhofia kabla ya pambano na upepo ulikata Kama kwa Andy Ruiz Junior The Destroyer.
Tusubiri pambano la marudiano tuone kama atarudia alichofanya kwa Ruiz, japo binafsi namuona this time ana wakati mgumu sana.
 
Nipige this time halafu nitaomba kurudiana tuta make pesa kuliko hii, hawa jamaa siku hizi siwaamini hizi game za marudio ndio target zao game ya kwanza kama promotion na kweli kama WWE lakini bora WWE wao hata jina lao ni entertainment sawa tu ila boxing siku hizi hakuna kitu. Tyson aliondoka na ngumi zake....
 
Ngumi walipigana kina Evander Hollyfied, Tyson, Bowe, Lenox, Razor Rudock, Mohamed Ally, Ken Norton, Foreman nk. Hawa wa sasa hakuna ngumi kabisa.

Angalia hilo pambano la Bowe na the real deal highlights kisha angalia la Joshua, unaweza kulia.
 
Nipige this time halafu nitaomba kurudiana tuta make pesa kuliko hii, hawa jamaa siku hizi siwaamini hizi game za marudio ndio target zao game ya kwanza kama promotion na kweli kama WWE lakini bora WWE wao hata jina lao ni entertainment sawa tu ila boxing siku hizi hakuna kitu. Tyson aliondoka na ngumi zake....
True..
 
Niliwahi cheki movie ya Creed

Pale mtoto wa apolo creed anamuuliza mwalimu ilikuwaje alimpiga baba yake kwenye pambano maana babaye anasifika kuwa alikuwa bondia hatari Sana

Jamaa akamjibu "it was time " his time was over "

Muda ukifika utapoteza tu no matter what

AJ era is fineshed kuanzia Sasa ataanza kupigana mapambano ya bonanza
 
Afadhali Fury kuliko Wilder,

Fury is more technician,
Wilder is the deadliest Killer!

Joshua hana chin, hana pumzi
 
Kwa Mfano Fury alitumia techniques kumpiga Wilder,

Hivi hivi huwezi kumpiga Wilder,

Mkono wake wa kulia ukitua kwenye Kichwa unakuwa umeshamaliza kazi!

Ana mkono wenye nguvu kwenye ndondi Duniani,

Kama ulivyo mkono wa Ngannou kwenye UFC
 
AJ siku hizi anapenda biashara kuliko heshima, hapo anatafuta hela ndefu kwenye pambano la marudiano.

Huyo jamaa atachakazwa na AJ kwenye pambano la marudiano hamtaamini.
Mimi ni mshabiki mkubwa wa AJ, hebu tuache kujifariji uongo.

Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mapambano ya AJ utagundua alianza kushuka kiwango tangu 2018 baada ya kumpiga Klitschko.

-Miguu haina balance
-Pumzi inakata mapema
-Right hook nyingi zinakuwa off target, hii ni kwasababu anaogopa kumkaribia mpinzani maana anajua akipigwa combination lazima aende chini. Kwa ushahidi zaidi angalia raundi ya 12 Usyk alivompiga combinations ila kengele ikamuokoa.

Tukubali tu AJ enzi yake ndo imeisha hivo kimasihara.

Akirudiana na Usyk anastaafishwa rasmi kwa KO.
 
AJ yupo katika kuandaa mafao yake ya kutosha ili akae nje ya ulingo ili aendelee kula maisha, yamebaki mapambano 4 kama alivyopanga ratiba zake
 
Back
Top Bottom