Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Anna Mghwira

R I P
Mar 9, 2012
206
362
Ninaikumbuka vema kauli ya mama Salma Kikwete kuwa nanukuu: " Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako." Leo watoto wa wenzetu wameingia tatizo la kukosa mikopo ya elimu ya juu; tuwasaidie kama watoto wetu.

Ninapenda kuwaomba akina mama wote nikianza na Mhe mama Salma Kikwete aliyeasisi usemi na hatua hii, tushirikiane kunusuru maisha ya elimu ya watoto walioko vyuoni wenye sifa ya kuwa na mikopo lakini hawakufanikiwa kupata mkopo. Tuwahamasishe vijana waliobakia mitaani na majumbani kujiunga na vyuo vikuu kuanua akili zao changa kukidhi ushindani wa sasa kimaisha.

Naomba akina mama wote viongozi, wazazi, walezi, wafanya bishara, waajiriwa, wanaharakati bila kujali itikadi zetu za aina yoyote tusimame kama wanawake wazazi wenye nia kuejnga taifa la watu walioelimika tuunde mfuko wa kuwasiadia watoto wetu wafanikiwe kumaliza masomo yao kwa ujenzi wa taifa letu.

Nikitoka na mama Kikwete ninaomba wake za marais wote waliopita kuanzia na mama Karume (mzee marehemu na Rais aliyemaliza mda wake) mpaka mama Janet Magufuli anayenivutia sana kwa kuonesha moyo wa amani sana kwa taifa letu.

Baada ya hao nimuombe mama Anna Makinda na wabunge wanawake wote waliopo na waliomaliza tangu uhuru wa nchi yetu tuungane kumsaidia kila mtoto wa Tanzania mwenye uwezo wa kusoma asome.

Kisha kwa niaba ya wanawake wafanya bishara niombe kitengo cha wanawake cha TCCIA, Baraza la Biashara la wanawake...tukubali wito huu: Tuungane kama wazazi na walezi chini ya kauli mbiu: Mtoto wa mwenzio ni mtoto wako...tuunde mfuko wa elimu kwa ajili ya vijana wetu.

Niombe vyama vya wana-taaaluma: waalimu, madaktari, wahandisi, watumishi wa umma, mabenki, makampuni yote ya ndani na ya kigeni, asasi za kiraia za ndni na za kimataifa, balozi zetu zote, tuungane kuunda chombo hiki kuwasaidia vijana wetu.

Nimeguswa sana na mahangaiko ya vijana wa vyuo vikuu. Ninawashukuru wachache waliofika kwangu kueleza changamoto zao. Mmenihamasisha kuchangia kidogo elimu yenu lakini ninaomba hili liwe suala la kitaifa.

Ninaomba wanawake wenzangu popote tulipo tuwasiliane tuunde umoja huu kuwaimarisha na kuwapa tumaini vijana na janga la kukosa elimu ya juu kama wana sifa za kuipata.

Tuweke kando siasa, dini, kabila, ukanda ama aina yoyote ya kigezo kufanikisha jambo hili. Ninawashukru sana. Kesho kuna wanafunzi watashindwa kufanya mitihani kwa kukosa ada kidogo tu ya laki kuanzia 5-8. Mfuko wa mama Salma, Mfuko wa mama Mkapa wa Fursa sawa kwa wote, Taasisi ya Benjamini mkapa, Taasisi ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mwalimu Nyerere, na zingine, tusaidiane kukamilisha azima hii. Na mimi nimeanzisha Taasisi ya Mama Anna Mghwira kwa ajili ya kushughulikia masuala ya aina hii.

Nitawashukuru sana kwa niaba ya vijana wetu, tuenzi elimu yao kwa kuunganisha nguvu zetu hivi. Mnisamehe kwa kuandika mtandaoni. Nimejaribu njia za kawaida za simu sikufanikiwa sana. Hapa ninajua kila moja atapata taarifa. Mapungufu yangu yasizuie jambo hili kutendeka. Jinsi tulivyo changia madawati, sasatuchangie elimu ya juu.

Niombe wizara na Bodi ya mikopo ya wanafunzi kutoa ushirikiano tutakapouhitaji utaalamu muwe nasi bega kwa bega.

Mungu atubariki wote, aibariki Tanzania.

Asanteni tena, ni mimi mama Anna Mghwira
 
Kweli tungepata viongozi wa aina hii katika nchi hii sijui tungefika wapi.

Tungekuwa mbaaali mno na pengine tungehama kutoka dunia hii ya tatu kwa kweli

Wengine nao wapo tu kujinufaisha wao katika ngazi zao

Jamani akina mama bila kujali itikadi yoyote ya vyama vyenu au chochote unganeni kulikomboa taifa,

Kuna shamba na kuna mbegu lakini mpandaji kakosa
Miaka ijayo tutakosa mavunobya wataalam na wajuvi mbalimbali hapo ndipo tutaanza kutafutana wapi tumekosea.

Leo vijana wengi wapo mtaani na si hivyo wwngine hawajui hatma yao aseee ungeni mkono hilo
 
Hili ni wazo zuri sana mama.

Huu ni wakati muafaka kwa kila mtanzania kuachana mara moja na utamaduni wa kuchangia harusi na sherehe nyingine zisizokuwa na tija kwa taifa na kuhamia kwenye kuchangia elimu kwa Mtanzania kwa manufaa ya Tanzania ya baadae.

Hakika wazo hili kama likipata msukumo unaostahili, tunaweza tusije kuzungumza tena hapa juu ya watoto wenye ufaulu wanaoshindwa kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu.

Pesa hii ikishakuwepo, itatolewa kwa walengwa on academic merits. Kulingana na kiasi kitakachokuwepo, itasetiwa cut-off point ya mtoto atakaekuwa eligible kupata hiyo scholarship.
 
Nina wasiwasi na serikali hii kama kweli ina dhamira ya dhati kuinua elimu na kuwasaidia watoto wa masikini.

Nakumbuka kwenye kampeni mjini Tabora mjomba alisema hakuna mtoto atakayekosa mkopo. Sasa sijui kma mjomba anakumbuka.

Kwenye majukwaa wanasema hii ni serikali ya wanyonge na maskini, Lkn kwenye utekelezaji ni tofauti kabisa. Huu umaskini wetu ndo viongozi wanajivunia.
 
Mama Anna;

Umetoa wazo zuri sana! Umetoa mwelekeo..!

Humu najua watu wataliunga mkono kwa maneno tuu na pongezi kwa wazo zuri..

Nilifikiri huu wito ungefanya event kabisa ili uliadress vizuri..either uitishe Press au kitu kama fundraising na kuwaalika watu wote walengwa..

Humu kuna members kama 400,000 hivi...bado tunataka ifike kwa watu zaidi hata watu 24milion ambao ni nusu ya Population yetu...

Ikiwezekana zihusishwe Taasisi tuu, watu binafsi na NGOs ! Serikali ikae pembeni manake wataleta siasa..! Hili suala wameshindwa kwa sababu watu wako after political gain..

Leo tukishindwa kusomesha hiki kizazi..miaka 50 ijayo hili taifa litapotea kabisa..

[HASHTAG]#Elimukwanza[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Uzalendokwanza[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Mikopo[/HASHTAG] elimu ya juu
 
Mama yangu umetoa wazo zuri, nachelea kusema watu wanaweza kuchukulia unataka kujijenga kisiasa na kumbuka ulikuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Kumbuka serikali iliyopo madarakani ilisema watapewa mikopo wale tu waliosoma shule za serikali kwa maana ya kuwa waliosoma private wazazi wao wana uwezo!!!???

Uangalie usije kuwa unataka kuichonganisha serikali na wananchi wake maana tunatofautiana uelewa.

Ili kutoingia kwenye mgogoro,ningeshauri uanzie huko huko serikalini kwa kuwaomba wakukubarie wazo lako.

Naamini, watanzania wengi watakuunga mkono na si wanawake tu kama uluvyoainisha.
Watoto wamebaguliwa, kuna watoto wa watanzania na walipa kodi ndo wanafaidi kodi za wazazi wao!!!!

Hili huwa linatia hasira kama sio kusikitisha....

Hongera mama kwa kuja na hili wazo,simama nali,komaa nalo mpaka uone matunda yake.
 
Akhsante sana mama, hoja ya msingi kabisa. Mimi niliwahi kupata wazo kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wetu.

Kama serikali inashindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili,basi tuweke taratibu,sheria au kanuni ambazo zitalazimisha halmashauri husika ambapo mwanafunzi anatoka kuhakikisha mwanafunzi huyo anasomeshwa nao.

Na hili kuna Halmashauri wanafanya tayari. Pia kama tunaweza kuchangia sherehe mbalimbali (mpaka arobaini ya mtoto) na kupatikana mamilioni,kwa nini tusichangishane kwa hawa watoto ambao wamekosa mikopo?

Utengenezwe utaratibu tu hata wa kutoa asimilia fulani za michango ya sherehe kwa ajili ya kusaidia hawa vijana. Hili kimsingi ni jukumu la serikali,lakini kama pamoja na kelele zote zilizokwisha pigwa kuhusu wanafunzi wote wenye sifa za kupewa mikopo wapewe,bado wahusika hawaonyeshi kujali.

Sasa tuache kuwasaidia vijana wetu kusoma kisa tu si jukumu letu ni la serikali au tuwasaidie ili kujenga Tanzania bora ya kesho.
 
Wazo zuri sana Mama Mghwira. Ila angalizo, kuna wale ma-plagiarists wazoefu ataibuka RC mmoja (safari hii anaweza kuwa mwingine); ataliteka wazo; litaenezwa kwa propaganda kali halafu mwisho wataliharibu na kujisifia chama cha wanyonge kimejaribu!

Kuweni makini na hawa majamaa japo manasema maendeleo hayana itikadi au vyama lakini wao ni mabingwa wa kutafuta sifa kupitia migongo ya wengie japo wazoefu wa kuharibu.
 
Nilihuzunika sana baada ya wanafunzi wenzangu wa mwaka wa kwanza kuondolewa kwenye chumba cha mitihani kwa kushindwa kulipa ada...chuo ni cha serikali..pamoja na kusoma kozi zenye kipaumbele (sayansi) bado mikopo tunaisikia kwenye bomba....ambapo ilikuwa vigumu kukosa mkopo kipindi cha jk kama unasoma masomo ya sayansi...

Tulitembea sana bale bodi ya mikopo bila kupata msaada wowote mpaka Dada mmoja miongoni mwa ofisi pale mapokezi aliposema mliambiwa elimu bure hadi chuo kikuu nyie mkachagua had I form 4. Niliondoka pale nikawapigia simu wazazi/walezi nikawaambia sasa ndio mwisho wangu wa elimu nimekosa mkopo naomba nirudi nyumban....
Wakajichanga wakapata ada wakaniambia wewe ni mtoto wa kiume hiyo ada matumizi mengine tutakuapatia Mungu akipenda....

Cha kusikitisha zaidi ni bodi pamoja na serikali yaani wizara kushindwa kusema ukweli juu ya mikopo...idadi kubwa ya wanafunzi tumekosa na wengi wamerudi majumbani kwa kushindwa kumudu gharama za masomo....
 
Back
Top Bottom