Anguko huduma za afya :Ushauri kwa Wizara ya Afya

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,535
Huduma za afya katika nchi yetu zimeanguka rasmi, hakuna ubishi kwa hili.
Kinachoniogopesha kwa sasa nimeshuhudia hata watumishi wazalendo, na wanaojituma wamekata tamaa, wamejaa na hofu, kujiamini kwao kumeshuka kwa kiasi kikubwa.

Nimetoka kupeleka mgonjwa wangu hospitali moja apa mjini,kwa kweli mgonjwa wangu katibiwa, ila katibiwa na watoa huduma waliojaa na hofu na kukata tamaa. Mhudumu wa afya anavyotoa huduma katika hali ya hofu uwezekano wa makosa ya kimatibabu huongezeka Maradufu.

Kati ya mambo /jambo ambalo wanasiasa wamefanikiwa (lakini limekuwa na mafanikio hasi) ni kujenga hofu kwa watumishi,matokeo yake huduma zimezorota zaidi hadi anguko rasmi la sekta hii.

Tukubaliane ya kwamba ni wajibu wa viongozi kuchukua hatua pale mtumishi anapokosea, ni vyema pia tukubaliane Kuna uwezakano mkubwa njia zilizotumika/zinazotumika sio sahihi.Yaani uwezekano wa kufa kwa mtanzania umeongezeka zaidi ya mara 10,,kulinganisha na mwaka1999.
Ushauri wangu kwa wizara ya afya.

1.kwa dhati kabisa ikubali kuna anguko kubwa la huduma za afya apa nchini

2.itoe tamko la kuonya kwa mwananchi yeyote kumshambulia mtoa huduma.

3.kuhakikisha watoa huduma wanaokikuka taratibu za kazi wanachukuliwa hatua kwa mjibu wa taratibu za kazi.

4.kutoa mafunzo maalumu kwa wanasiasa(madiwani, wabunge, mawaziri, rc, dc) kuhusu mfumo mzima wa huduma za afya apa nchini

5.kufanikisha mikutano kati ya vituo vya kutolea huduma na wananchi (kuanza vijijini, wilaya, mikoani)

6.kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba. Bajeti ya afya iongezwe maradufu.

7.Kusomesha watumishi wengi wa afya kuanzia ngazi ya cheti adi ubingwa. watumishi wengi hawaendelezwi ata nafasi za kwenda kusoma wanapewa watumishi wa mijini,, watumishi wengi wa vijijini wamesaulika na hawakumbukwi kuendelezwa kimasomo.

8.Vituo vyote viwe na namba ya simu na iwe wazi mda wote, pia wizara iwe na namba ya huduma kwa mteja iwe wazi mda wote.

9.Wizara ihakikishe makundi ya msamaha yanapata huduma stahiki.

10.wizara kumkemea(kupitia vyombo vya habari tv etc) kiongozi yeyote atakayetumia vibaya madaraka yake kumnyanyasa mtoa huduma.
 

wizara ya afya chonde chonde, mshughilikir jambo hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…