Folk Part II

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
412
486
Habari wana jamvi?

Kama kichwa kinavyojieleza nimeanzisha thread hii ili itusaidie sisi kujua je hizi ndoto zinatofautiana au sawa kwa watu sawa au wanaoishi maeneo tofauti lakini zinakuwa na maana moja au ni tofauti?

Andika ndoto yako ya usiku wa leo hata siku zijazo utakazoota hii itasaidia pia kutunza ndoto zako na utaweza kutafusiriwa zilikuwa na maana gani katika maisha yako?

Ni mimi hapa
Folk Part II
Naandika nikiwa hoi kitandani.
 
Kuota mwanamke unayemfahamu anakuomba hela unamnyima anaamua kuondoka kwa bodaboda kabla hata hajaondoka hata hatua kumi pikipiki inapata ajali na mwanamke kufa palepale, halafu mimi nafuatwa na staff member mwenzangu na kuondoka kwa pikipiki..
Upo unasafiri kwa pikipiki umebebwa na ndugu yako mkiwa njiani mnakaribia sehemu watu wamekusanyika kwa msiba mnapata ajali mnamgonga mwendesha baiskeli wa kike na kufa palepale
Kuota upo kwenye kitu kirefu kama jengo halafu baadae hicho kitu kikapata hiitlafu na kuanza kubomoka lakini kabla sijaanguka nikapata kamba nikashuka nayo salama, halafu mwenzangu aliye kuwa jinsia ya ke... Akajirusha akafa palepale.
Kwa vyovyote utakua una mawazo negative sana dhidi ya wanawake.
 
Nimeota wadada wawili tunaishi nao karibu. Mmoja kanishika akiwa kavaa khanga nusu uchi akanishika sehemu za siri kwa nguvu, ananiambia atakuja kwangu leo usiku, wakati anamaliza kuniambia nikamuona mwenzake anatokea akawa ananionya kuwa amemsikia huyo alichoniambia cha ajabu na yeye yuko kifua wazi na ananiangalia kwa matamanio.
Hawa nimewakwepa kwa mikwepo yote mwaka mzima na kuna uwezekano ndani ya siku tatu zijazo nisiwe nao karibu tena maana wataondika eneo lililokuwa linaniweka karibu nao.

Nimejiuliza maana yake nini. Nimeamua kupotezea tu, japo asubuhi tumeonana na kusalimiana.

Mtaalam, karibu. Hata mimi ni expert wa mambo ya ndoto za kiroho ila hili limenishangaza maana ninao kila siku lakini sijawahi kuwafikiria hadi kuwaota.
 
Ukiota mkeo anagegedwa na bestie wake wa kiume ina maana gani kindoto/kiroho?
Kiroho inamaanisha kwamba.......

viumbe wameumbwa na hisia za tendo la ndoa kila penye viumbe wawili wa jinsia tofauti lazima hizo hisia zitakuwepo ambapo kwa wanyama wengine ukiachana na binadamu watafanya bila kujali undugu lakini kwa binadamu huzuiliwa na sheria za kijamii kama maadili ya jamii, heshima kwa mfano huyu ni mama, mke wa ndugu yangu au mke wa mtu au ni ndugu yangu na hii inatuaminisha kwamba hakuna urafiki wa karibu sana kwa jinsia mbili ambazo hazina undugu wowote na kama ni ndugu usizidi mipaka

Kimazingira na Kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba.......

Binadamu huwa hatuamini kabisa urafiki wa ukaribu wa mwanaume na mwanamke ambao hawana undugu kama unaweza kuwa wa kawaida usihusishe mapenzi na wewe hili lipo kichwani mwako (imani). kama huwaziagi kwa mke wako na bestie zake bas umeona kwa mke wa ndugu/rafiki zako akiwa na mazoea yanayoashiria mahusiano au tayari ushawaona wake za watu wakichukuliwa na watu wengine au wewe mwenyewe ndo maana imekuja ndotoni
 
Kuota upo kwenye kitu kirefu kama jengo halafu baadae hicho kitu kikapata hiitlafu na kuanza kubomoka lakini kabla sijaanguka nikapata kamba nikashuka nayo salama, halafu mwenzangu aliye kuwa jinsia ya ke... Akajirusha akafa palepale.
Kiroho inamaanisha kwamba...

Hii ndoto ilikuwa inakukumbusha ufanye vitu vyako kwa tahadhari ili viweze kwenda sawa,

kwenye ndoto tahadhari yako ilikuwa ni hiyo kamba ambayo ilikuokoa na huyo mwanamke aliekufa kwenye ndoto alikosa tahadhari na kupoteza uhai. huyo mwanamke katumika kama funzo kwako

Kimazingira na kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba.....

Unajua kazi ya kamba, umewahi kufikilia kitu kikibomoka, umewahi kuona au kufikiria jengo lefu likibomoka na unaweza ukajiokoa vipi, unajua kati ya mwanaume na mwanamke nani anaweza kujiokoa kirahisi huu muunganiko ukakupa ndoto hii
 
Upo unasafiri kwa pikipiki umebebwa na ndugu yako mkiwa njiani mnakaribia sehemu watu wamekusanyika kwa msiba mnapata ajali mnamgonga mwendesha baiskeli wa kike na kufa palepale
Kiroho inamaanisha kwamba.....

Binadamu huwa hamwamini binadamu mwezake alieishikilia roho yake.

Kimazingira na kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba....

Kila binadamu awepo safarini au mwenye safari huwazia ajali na wewe kwako huwa unafikiria hili na ndo ukapata ndoto hii na ndo mana utaskia ajali ikitokea mtu anasema roho yangu ilikuwa inasita sana kusafiri leo kiukwel hakuna ambaye huwa hawazii hii kitu
 
Kuota mwanamke unayemfahamu anakuomba hela unamnyima anaamua kuondoka kwa bodaboda kabla hata hajaondoka hata hatua kumi pikipiki inapata ajali na mwanamke kufa palepale, halafu mimi nafuatwa na staff member mwenzangu na kuondoka kwa pikipiki..
Kiroho inamaanisha kwamba....

Binadamu kaumbwa na roho ya chuki ambayo hii roho imejaa wivu, na ubaya ndani yake na hii ndoto inakuonyesha kwamba kila umchukiae au akuchukiae lazima akuombee/umuombee baya limkute
Inakuonyesha kwamba ni watu ambao inatakiwa kukaa nawo mbali sana

Kimazingira na kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba.....

katika maisha yako ya kawaida mwanamke amekuwa ni chukizo kubwa sana na unamfikiria kwa ubaya sana mwanamke imefika hatua kila mwanamke unamchukulia ndo walewale
 
Nimeota wadada wawili tunaishi nao karibu. Mmoja kanishika akiwa kavaa khanga nusu uchi akanishika sehemu za siri kwa nguvu, ananiambia atakuja kwangu leo usiku, wakati anamaliza kuniambia nikamuona mwenzake anatokea akawa ananionya kuwa amemsikia huyo alichoniambia cha ajabu na yeye yuko kifua wazi na ananiangalia kwa matamanio.
Hawa nimewakwepa kwa mikwepo yote mwaka mzima na kuna uwezekano ndani ya siku tatu zijazo nisiwe nao karibu tena maana wataondika eneo lililokuwa linaniweka karibu nao.

Nimejiuliza maana yake nini. Nimeamua kupotezea tu, japo asubuhi tumeonana na kusalimiana.

Mtaalam, karibu. Hata mimi ni expert wa mambo ya ndoto za kiroho ila hili limenishangaza maana ninao kila siku lakini sijawahi kuwafikiria hadi kuwaota.
Kiroho inamaanisha kwamba.....

(Nguvu ya Roho ya pendo kwa jinsia mbili tofauti)
Roho yako inaamini katika kupendwa na kuvutiwa na wanawake

Kimazingira na kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba.......

Katika maisha yako kuna sehemu umekutana na wanawake ambao wamekuonyesha kukupenda/kuvutiwa na wewe tofauti na hao uliowaota ndotoni na hua unawafikiria hao wanawake, kifua ulichokiona kwa mwanamke wa ndotoni ni kifua ulichokionaga kwa mtu uliemuonaga akiwa tupu au huwa unakifikiria kichwani mwako kifua kama icho kuwa ndo chenye mvuto au cha ovyo, sura ilizoziona ni zao ila haimanishi ni wao ndo walikuja ndotoni huo ni mtindo wa mfumo wa fahamu kuunganisha vitu tofauti na kuwa kitu kimoja usije shangaa unamuota mwanamke sura yake na unafanya nae mapenzi na kuona K yake wakati kiuharisia haujawahi kuiona ile huwa ni ile ambayo umewahi kuiona sehemu fulani kwa mtu halisi au picha au kwa kuifikilia ilivyo. Hao wanawake hauna haja ya kuwakwepa hicho kitu hawajui kama umewaota labuda mpaka uwambie na ndoto haithibitishi kama wao wanakupenda ila wewe hapo wapo unaoamini wanakupenda na sio hao mana umesema huwa huwafikirii
 
Nimeota nimefumaniwa na sina mume, hapo vipi sheikh Yahya
Kiroho inamaanisha kwamba.....

Ndoto hii inakuonyesha kwamba haujatulia na mpenzi mmoja na inakuonya nini madhara ya kuwa hivo

kimazingira na kimaisha ya kawaida inamaanisha kwamba.....

Unawaza ukiwa na wapenzi wengi huku ukihofia kufumaniwa. Pia wewe ni mchepuko wa mme wa mtu huwa unawaza kufumaniwa
 
dah! Sema nini bro ukikaza utawapiga maboya wengi, nimecheka balaa
 
Mtaalam Folk Part II , nakusalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nina ndoto nyingi sana nilizoota
1. Niliota nipo maeneo ya soko la samaki la Ferry kona ya kwenda Ikulu nimesimama na mwenzangu akapita Mheshimiwa Jakaya Kikwete raisi mstaafu anaendesha gari Escudo nyekundu akatuita huku anatabasamu Vijana twendeni tukapanda gari tukaondoka. Hii ina maana gani ?

2. Niliota ndoto nyingine kumhusu Msichana fulani ambaye tunatoka Wilaya moja na wote ni kabila moja na tumefanana kwa vitu vingi sana, ikiwemo Siku ya kuzaliwa japo nimempita karibia miaka mitano na miezi mitano na siku kama 9 hivi. Ananipa Sufuria ndogo nyeupe mpya kabisa huku akipiga goti na anatabasamu hii ina maana gani ?. Hizi ndoto kumhusu huyu binti nimeota zaidi ya ndoto saba ambazo ni kama series kabisa :):)

3. Ndoto nyingine niliota tupo kwenye mazoezi kama ya wale Vijana wa JKT tumesurubika sana, tukawa tumekaa chini tukiwa tumechafuka sana na tumenyoa vipara yaani ni kama mazoezi ya Kijeshi. Sasa akatokea Dada ambaye ni kama Secretary wa Boss akaanza kusema " Mwenye nidhamu na aliyefaulu mafunzo yetu ni ( .....................) Akamtaja jamaa mmoja ambaye ni mshikaji wangu tulisoma wote Shule ya Msingi na Secondary lakini tukaja kutengana baada ya Mimi kuhama ile Shule, Sasa yule Secretary wa Boss alivyomtaja yule Jamaa akatokea Boss akasema hakuna wewe kaa chini , njoo MANYANZA, sasa wakati nainuka nataka kwenda kwa boss huku nakimbia yule jamaa akanishika Tshirt ili nianguke lakini nilimpiga ngumi nzito na akaniachia huku akivuja damu puani na mdomoni, nilivyoinuka nikawa namkimbilia Boss nilipofika kwa Boss akaninyanyua juu huku akinipongeza. Na huyu jamaa ambaye niliyempiga ngumi kafariki mwaka huu kwa ajali ya gari hapa hapa Dar es Salaam na nilikuwa naenda sana kumtembelea na kumsafisha wakati mwingine. Je hii ndoto ina maana gani ?

4. Nimeandika ndoto ya kwanza kumhusu huyo Binti, Kuna siku nilimuota Mama yake Mzazi, wapo kwenye Kibasi kidogo hiace mbuga za Wanyama yeye na Wakina Mama wengine, Kile Ki Hiace kikaharibika ghafla na wale wakina wote wakamkimbia na Yeye akawa anahuzunika na akaonekana kama ana umwa ugonjwa wa tumbo na Mimi nilikuwa juu ya mti nikashuka nikaenda kumpa pole huku nimemshika begani akaanza kutabasamu na furaha ikamrudia tena. Je hii ndoto nayo ina maana gani ?

Zipo ndoto nyingi sana nisaidie maana ya hizo ndoto. Kiimani na Kiuhalisia wa maisha yetu Sisi Binadamu
 
Back
Top Bottom