Anayoyaeleza John Mnyika kuhusu CCM kupaka rangi ofisi ya mtaa wa Saranga na kuigeuza ofisi ya chama yana ukweli? Tumefikishwaje hapa?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,037
4,752
Kuna habari nyingine siwezi kuziamini hadi nipate ufafanuzi kutoka upande wa pili. Nimeona clip inasambaa ikieleza kwamba katika jimbo la Ubungo chama cha mapinduzi kimebadili matumizi ya ofsi ya mtaa na kuipaka rangi cha chama kisha kuifanya ofisi ya chama.

Anadai TAKUKURU wameambiwa wakakaa kimya, mkurugenzi kimya na chama nacho kimekaa kimya. Kinachonisikitisha ni ukubwa wa ofisi ikilinganishwa na ukubwa wa chama.

Je, kweli CCM inaweza kupora vyumba viwili vya ofisi na kuvipika rangi? Kama wamefanya hivyo ni msimamo wa chama au kuna mtu au kikundi cha watu kimeamua kukichafua chama? Kubadili ofisi ya serikali kuwa ofisi za chama ni tuhuma za ubadhirifu wa mali za umma. Ikumbukwe mali za umma siyo mali za chama.

Niombe suala ili dogo lipatiwe ufafanuzi wa haraka lisitumike vibaya huko ubungo. Mhe. Kitila Mkumbo hizi karata usipozichanga vyema hawa jamaa watakupokonya jimbo mchana kweupe. Wameanza kupata wafuasi nahoja zimeanza kumiminika.
 
Back
Top Bottom