Anayejua identity ya mziki wa bongo aje

Mr.Wenger

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
2,558
6,091
Siku za karibuni kumezuka stories kuwa wabongo wameacha kupiga miziki ya kwao na kuwaiga wanaigeria. Mfano wa ngoma zinazotajwa kuiga ladha ya Nigeria ni kama Kokoro, Shikorobo, Mugacherere, na nyingine nyingi. Sasa nataka wataalam wanaojua identity ya mziki wa bongo waje watujuze. Binafsi nimesikia style nyingi sana hapa bongo kama mnanda, mchiriku, dansi, taarab, mduara, zhouk, rnb, singeli, takeu,hip hop, traditional music ( kama anaofanya Saida karoli)na nyingine nyingi. Sasa mziki upi unaidentify bongo fleva? Ni vyema anayefahamu akaja na mfano wa msanii na wimbo/nyimbo ambazo hizi tutasema ni wa asili ya bongo na ndo identify yetu kimataifa.
Wadau mnakaribishwa kuchangia
 
Asili ya mziki wa Tanzania ni Mchiriku tu.....sema kwa kuwa haukuwai kupewa sana promo na wengi wao wanaouimba ni masela kwa sana,mchiriku unaonekana ni mziki wa wahuni,ila asili ya mziki wetu ni mchiriku.
 
Asili ya mziki wa Tanzania ni Mchiriku tu.....sema kwa kuwa haukuwai kupewa sana promo na wengi wao wanaouimba ni masela kwa sana,mchiriku unaonekana ni mziki wa wahuni,ila asili ya mziki wetu ni mchiriku.
Sasa kwanini sasa hivi ndo wanasema tunaiga wakati kuiga tumeanza tangu enzi na enzi?
 
Wenzetu nje ya Tanzania sasa wakisikilizia Muziki wetu tu wanasema hii ni Bongo fleva to Tanzania, Kama mfuatiliaji wa Muziki wetu utagundua muziki wetu sasa Una touch flani zinafanana kwenye nyimbo nyingi, Na touch hizo hazikuwepo kipindi cha nyuma enzi Bongo fleva inaanza!

Nakumbuka siku moja nipo na Producer mmoja maarufu kipindi hicho sasa ni Marehemu, akiitwa Roy toka G Record, alinambia "Kama Producer tunahangaika kutafuta Muziki flani ambao utakua Uniform hapa Bongo, ila siku sio nyingi Muziki wa Bongo fleva kwa the way unavyo sound, mtu akiusikia popote atasema huu Muziki ni kutoka Tanzania"
 
Asili ya mziki wa Tanzania ni Mchiriku tu.....sema kwa kuwa haukuwai kupewa sana promo na wengi wao wanaouimba ni masela kwa sana,mchiriku unaonekana ni mziki wa wahuni,ila asili ya mziki wetu ni mchiriku.

Ni taarabu


Kula aina ya muziki una historia yake na umepitia kwenye mabadiliko ya muda mrefu. Sawa na taarabu na mchiriku. Ukifuatilia historia utagundua mchiriku ulianza zamani ulikuwa ukiitwa chakacha au maarufu kama msambwe. Kama taarabu vionjo na sound za kibantu viliwekwa baadae Sana kadiri miaka ilivyokwenda. Lakini zamani aina hizi za muziki zilikuwa hazina tofauti Sana na muziki wa waarabu. Taarabu ilitumia ala nyingi na Mara nyingi kulikuwa na mchanganyiko wa wasanii wa kike na wakiume, wakati chakacha wanaume Tu na kulikuwa na kundi kubwa la wasenge wanaofuata msambwe kila unakopigwa. Wengine walitandikiwa virago chini kuonyesha uhodari wa kukatika.
 
Its true, hatuna ID ya muziki wetu tunaiga mara kwaito sijui mara naigeria na hiyo inatufanya tushindwa kujitambulisha kimataifa ingawa Diamond anajituma sana lakini hata yeye ukimfuatilia sana copy melody zake kwa wanaigeria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…