Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,310
- 26,156
Habari hii nimeisikia asubuhi hii kupitia RFA magazeti, mwenye taarifa atujuze ni nani ukizingatia kuna yule mwandishi wa kanda ya ziwa anayedaiwa kuandika sakata la mkuu wa mkoa kukamatwa na polisi akiwa Musoma.
Kaimu Kamanda wa Jeshi wa polisi Kagera, Yusuph Daniel amethibitisha tukio hilo kutokea, ambapo mwili wa kijana huyo ulikutwa unaelea Juni 12 majira ya saa saba mchana na wavuvi waliofika eneo hilo kwaajili ya shughuli zao za uvuvi wa Samaki.
Kamanda Yusuph amesema uchunguzi unaendelea wa kubaini nini kimesababisha kifo cha kijana huyo na kuwatoa hofu baadhi ya wananchi wanaoamini kuwa kijana huyo kauliwa kuwa Jeshi la Polisi litahakikisha wale wote waliohusika bila kujali kama ni mtumishi wa Jeshi la Polisi au la watachukuliwa hatua stahiki endapo watathibitika kufanya mauaji hayo, na kuwaomba wananchi wawe watulivu wakati uchunguzi unaendelea.
========
Jeshi la polisi mkoani Kagera linaendelea kufanya uchunguzi wa kifo cha kijana Lucas Baraka (20), mkazi wa kisiwa cha Goziba wilayani Muleba mkoani Kagera aliyekuwa anafanya kazi ya kupakua dagaa kwenye mitumbwi baada ya mwili wake kukutwa unaelea katika Ziwa Victoria.