Anaomba ushauri: Alitembea na mume wa mtu, akamtumia mkewe picha za uchi

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,078
Nilifanya makosa ya kutembea na mume wa mtu, mke wake alijua na tukatukanana sana, huyo mwanaume alinidanganya kuwa atamuacha mke wake lakini baada ya kukaa miaka 7 naye nikaona umri unaenda hamuachi mke wake.

Mwisho nilimua kuachana na huyo mwanaume baada ya kumbebesha ujauzito dada yangu mtoto wa Mama yangu mdogo. Basi tukagombana na kila kitu kikaisha.

Hiyo ilikua ni mwaka juzi 2021 mwanzoni, nilisahau na nikaendelea na maisha yangu.

Lakini shida ni mke wake, pamoja na kuachana na mume wake lakini yeye bado hajaniacha, mwanaume bado ni malaya hivyo kama akifumania meseji huko ni kunitafuta na kunitukana.

Haiishii hapo, kuna mapicha mengi ya uchi na mavideo nilimtumia huyo mwanamke ili kumuumiza kuwa niko na mume wako. Kwa akili zangu za kipindi hicho nilikua naamini kama nikimtumia voideo niko kitandani nafanya mapenzi na mume wake basi ataondoka na kuniachia mwanaume.

Sasa anatumia hizo picha kuniharibia, kila nikipata mwanaume akishaona niko serious anamtafuta na kumwambia "ongea na mchumba wako aachane na mume wangu na kuacha kunitumia mapicha ya uchi"

Kaka mwanaume akishatumiwa picha zangu niko na huyo mzee hata nikijielezeaje hanisikilizi. Nilishapeleka nyumbani wanaume 3 lakini wote wameniacha kwasababu hiyo.

Nimejaribu kuongea na huyo dada, lakini haamini kama nishaachana na mume wake kwani bado mumewe anafanya umalaya, ananiambia kama nilivyomuumiza na kuharibu ndoa yake na mimi nitaumia hivyo hivyo!

Nimechoka na hii hali, naomba msaada wenu, nifanye nini ili huyu mwanamke aachane na maisha yangu.

Nina miaka 34 sasa, mwanaume kanipotezea muda wangu, Napata wanaume wazuri sana tena wananipenda lakini wakishatumiwa mapicha yangu wananiona kama kahaba nisaidieni nifanye nini Wana JF?
 
Sasa ipo hivi

Sisi wanaume hua hatutoi msamaha wa dhati linapokuja swala la usaliti wenye ushahidi. Hata kama ikitokea nimesema nimekusamehe basi ujue ni kinyume chake labda nimeamua kunyamaza tu kwasababu pengine bado nakupenda, sijapata mbadala, nakutumia ama kwasababu yeyote ile.

Wanaume tumeumbika tofauti kabisa na wanawake ambao hutoa msamaha wa dhati hata kama tumewasaliti, ingawa nyie hua mnasamehe kwadhati lakini mtaliongelea hilo jambo hata pale maisha yenu yanapo koma.
Kwahili lakukushauri ni.

Tafuta mtu yeyote alie na ukaribu na huyo mama kisha aichukue hiyo sim aidumbukize kwenye maji, then amwambie amlipe nyingine mpya na achukue ile akuletee uiharibu.

Hiyo mbinu inaweza ikakugharimu fedha ndefu lakini itakua imekutibu milele
 
Nilifanya makosa ya kutembea na mume wa mtu, mke wake alijua na tukatukanana sana, huyo mwanaume alinidanganya kuwa atamuacha mke wake lakini baada ya kukaa miaka 7 naye nikaona umri unaenda hamuachi mke wake...
Ulipata wapi ujasiri wa kutuma picha za ngono kwa huyo mwanamke? Kosa kubwa usirudie tena ujinga huo,hapo kaombe msamaha kwa hiyo familia wote mke na mme wenda akazifuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri hili kosa limefanywa na watu wengi sana, sema basi hawajulikani kwasababu hawajisemi.
Na miaka hiyo watu wengi hawakujua kama teknolojia ni kirusi cha hatari zaidi katika maisha ya mwanadamu
 
Nilifanya makosa ya kutembea na mume wa mtu, mke wake alijua na tukatukanana sana, huyo mwanaume alinidanganya kuwa atamuacha mke wake lakini baada ya kukaa miaka 7 naye nikaona umri unaenda hamuachi mke wake...
Njoo Pm tuongee binti mzuri mimi niko tayari kukuchumbia, epuka vibaka wa humu wengi wanaishi kwa wazaz wao.
 
Nilifanya makosa ya kutembea na mume wa mtu, mke wake alijua na tukatukanana sana, huyo mwanaume alinidanganya kuwa atamuacha mke wake lakini baada ya kukaa miaka 7 naye nikaona umri unaenda hamuachi mke wake.

Mwisho nilimua kuachana na huyo mwanaume baada ya kumbebesha ujauzito dada yangu mtoto wa Mama yangu mdogo. Basi tukagombana na kila kitu kikaisha.

Hiyo ilikua ni mwaka juzi 2021 mwanzoni, nilisahau na nikaendelea na maisha yangu.

Lakini shida ni mke wake, pamoja na kuachana na mume wake lakini yeye bado hajaniacha, mwanaume bado ni malaya hivyo kama akifumania meseji huko ni kunitafuta na kunitukana.

Haiishii hapo, kuna mapicha mengi ya uchi na mavideo nilimtumia huyo mwanamke ili kumuumiza kuwa niko na mume wako. Kwa akili zangu za kipindi hicho nilikua naamini kama nikimtumia voideo niko kitandani nafanya mapenzi na mume wake basi ataondoka na kuniachia mwanaume.

Sasa anatumia hizo picha kuniharibia, kila nikipata mwanaume akishaona niko serious anamtafuta na kumwambia "ongea na mchumba wako aachane na mume wangu na kuacha kunitumia mapicha ya uchi"

Kaka mwanaume akishatumiwa picha zangu niko na huyo mzee hata nikijielezeaje hanisikilizi. Nilishapeleka nyumbani wanaume 3 lakini wote wameniacha kwasababu hiyo.

Nimejaribu kuongea na huyo dada, lakini haamini kama nishaachana na mume wake kwani bado mumewe anafanya umalaya, ananiambia kama nilivyomuumiza na kuharibu ndoa yake na mimi nitaumia hivyo hivyo!

Nimechoka na hii hali, naomba msaada wenu, nifanye nini ili huyu mwanamke aachane na maisha yangu.

Nina miaka 34 sasa, mwanaume kanipotezea muda wangu, Napata wanaume wazuri sana tena wananipenda lakini wakishatumiwa mapicha yangu wananiona kama kahaba nisaidieni nifanye nini Wana JF?
Mshahara wa dhambi!
 
Back
Top Bottom