Amps, Volts & Watts ni nini? Kwanini Simu Yako Haichaji?

HabariTech

Member
Sep 1, 2019
8
22
Iwe ni chaji iliyokuja pamoja na simu au ulinunua baada ya kupoteza au ya kwanza kufa, wengi huwa tunazingatia amps, volts, na watts kujua kama chaji hiyo ni fast charger na kama inafaa kwenye simu zetu. Wasiwasi wetu huwa unakuja tunapoona chaji ya uwezo mkubwa inauzwa bei ndogo. Huu wasiwasi huwa ni sahihi kuwa nao, ni heri uchukue tahadhari kuliko kuchoma nyumba yako.

Ukiangalia charger utaona kuna maneno na namba nyingi zimeandikwa pale, bahati mbaya kwa wale ambao hawakupata elimu ya uhandisi wa umeme, huwa hawaelewi huwa yana maana gani. Hapa nitajitahidi kutumia lugha rahisi ili uelewe zile namba zina uhusiano gani na uwezo wa chaji kuchaji simu yako.


Kuchaji Simu Yako kwa Usalama​

Watengenezaji wa simu na vifaa vya simu vya uhakika wanahangaika kuhakikisha vifaa vinakuwa katika ubora. Watengenezaji wa simu wanataka simu ziwe na uwezo mkubwa wa kutunza chaji na zikae na chaji muda mrefu. Kuna kundi la pili la watengenezaji ambao huwa wanatengeneza chaji za bei rahisi ambazo hutengezwa kwa material za hovyo, ili ziwahi kufa ununue nyingine.

Watu wengu wamekuwa wakinunua hizi chaji za hovyo kwa kuwa ni bei rahisi na zinafanya kazi vile wanataka, lakini baada ya miezi kadhaa mtu analazimika kununua chaji nyingine.

Kwanini?

Kwa sababu chaji hizi hupoteza uwezo wake wa kuchaji simu katika ubora wa hali ya juu. Shida na hizi chaji za bei rahisi huwa ziko hivi

  • Zinaweza zisitoe umeme wa kutosha au unaozidi kiasi ambacho simu yako inatakiwa kupokea. Kitu ambacho hupelekea simu kuchaji polepole sana au battery kupata joto la kuzidi na kupelekea kulipuka.
  • Zinaweza kuwa hatari kwako na mali zako nyumbani. Hatari za chaji za hivi inaweza kuwa uharibifu wa kifaa chako au kusabibisha moto wa umeme nyumbani.
  • Zinaweza kuungua polepole na kutoa moshi ambao huchanginyika na kemikali zisizo salama kwa mfumo wa upumuaji wa binadamu.
Kwa ufupi niseme kwamba hata kama chaji imethibitishwa na mamlaka husika kama CE, UL au ETL haina maana kwamba ni salama kutumika kwenye simu yako. Ukiona ni bei rahisi mno kwa hiyo kuwa chaji ya ubora, ni uhakika kwamba haifai kutumika. Kuna uwezekano imetengenezwa kuwa ya bei rahisi kwa kutumia vifaa vya bei rahisi ambavyo vina uwezekano mkubwa wa kushindwa kufanya kazi.

Watengenezaji wa hizi chaji hutoa chaji nzuri kwa ajili ya majaribio katika maabara za mamlaka husika. Baada ya kupita majaribio hawa watengenezaji hurudi kutumia vifaa vya ubora wa hali ya chini ili wasitumie gharama kubwa kufanya matengenezo na wapate faida kubwa.

Unachotakiwa kufahamu​

Haijalishi unatumia charging ya port moja ya chaji au yenye port nyingi za chaji. Kuna maswali kadhaa unatakiwa kujiuliza kuhusu hiyo chaji.

  • Je amps, volts na watts zilizoandikwa kwenye hiyo chaji zinaendana na simu unayotaka kuchaji?
  • Hii chaji itakuwa na uwezo wa kuchaji simu kwa usahihi, bila kuzidi au kupungua uwezo?
  • Ni salama kutumia hii chaji?
Sehemu inayofata nitajitahidi kujibu haya maswali kwa lugha rahisi.

Amps, Volts, & Watts na Uhusiano Wao Katika Uwezo wa Kuchaji​

Uwezo wa kuchaji na umeme ambao simu huwa zinatumia huwa unapimwa katika watts. Lakini vya muhimu kuzingatia katika mobile charging ni amps na volts.

Amps ni kipimo cha umeme kiasi gani unapita sehemu fulani ndani ya sekunde moja. Volts ni kama spidi ya huu umeme kupita sehemu fulani ndani ya sekunde moja.

Nitatumia mfano wa bomba ya maji inayojaza maji kwenye ndoo ya lita 20. Tukifungua bomba ya maji kwa usawa wa nusu, itachukua dakika moja kujaza lita moja kwenye ndoo.

Kwa usawa ule ule tuliofungua hii bomba ya maji, tutapunguza upana wa mdomo wa bomba ya maji, hapa pressure ya maji itaongezeka (volts) lakini bado itachukua dakika moja kujaza lita moja ya maji.

Pia tukisema tuongeze upana wa bomba, pressure ya maji itapungua, lakini bado itachukua dakika moja kujaza lita moja ya maji.

Kwa hiyo kupunguza au kuongeza upana wa bomba kuna athiri pressure/spidi (volts) ya maji, ila ujazo wa maji/volume (amps) utabaki vile vile.

Kwahiyo pressure ya maji ni volts na ujazo ni amps. Kwahiyo ili ndoo yetu ya maji ijae haraka tunahitaji kuwa na ujazo mkubwa au amps nyingi. Sasa chukulia kitu pekee unajua hapa ni kuhusu ujazo, sasa wewe unaamua badala ya kutumia bomba kujaza maji kwenye ndoo. Wewe unaenda kuchukua tenki ya lita 10,000 yenye mdomo mkubwa sana kisha unamwaga tu maji kwenye ile ndoo ili ijae haraka.

Ukifanya hivyo pia utakuwa umefanikisha lengo, lakini unaweza lipia gharama kubwa sana kwa kufanya hivyo. Chukulia ile ndoo ni simu yako. Umezidisha ujazo na pressure ya maji, kitu ambacho kinaweza pelekea ile ndoo kupasuka. Hiki ndicho kinaweza tokea hata kwenye simu ukizidisha kipimo cha umeme kinachotakiwa.

Pia haitakiwi umeme uwe mdogo sana kiasi kwamba chaji iliyopo kwenye battery inakuwa kama kizuizi kuruhusu simu iingie chaji nyingine. Kwa hiyo ni muhimu sana kuzingatia unachagua chaji yenye vipimo sahihi kulingana na uhitaji wa simu yako.

Kanuni ya Amps x Volts = Watts​

Kama nilivyosema mwanzo kwamba watts ni kipimo cha kiasi cha umeme unao tumika na vifaa vya umeme, hivyo usishangae kuona hiki ndicho kipimo kinachokuwepo kwenye matangazo ya vifaa vya umeme.

Mara nyingi utakuta kuna utofauti wa kiasi cha amps na volts zilizoandikwa kuwa ni uwezo wa chaji au simu. Ni kawaida kuona hizi namba zikitofautiana. Tunachotaka kuona kinabaki sawa mara zote ni kiasi cha watts.

Kwa pamoja amps na votls ndizo zinapelekea kujua uwezo ambao simu inahitaji ili kujaa kwa haraka na usahihi. Kwa lugha rahisi ni hivi ukichukua amps kuzidisha volts unapata watts.

Amps x Volts = Watts

Hivyo unaweza kuta kifaa chako kinatoa 10V (volts) na 2A (amps) jumla inatoa watts 20W. Chaji nyingine itakuwa na 6.67V na 3A na itakuwa na 20W pia itakuwa inafaa.

Chaji nyingine itakuwa na 5V kwa 2A hii itakuwa na 10W. kwa maana hiyo hii chaji ya 10W itakuwa pole pole ukilinganisha na ile ya 20W. Wakati chaji ya 20W inachukua dakika 60 kujaza simu kutoka 0% mpaka 100% chaji ya 10W itachukua dakika 120.

Mpaka hapa utakuwa umeelewa kwanini, simu yako inaweza kuwa inachaji haraka au pole pole. Cha kufanya, chukua chaji yako soma sehemu ya output uone inasoma ngapi. Namba za kwenye output ndizo zinaonyesha kiasi cha umeme kinachoingia kwenye simu yako.

Hesabu hizi hizi pia zinatumika kwenye chaji za PC na vitu vingine vyote. Kitu kingine cha muhimu kuzingatia ni amps. Kumbuka amps ndiyo ujazo unaotakiwa kuingia kwenye simu. Kama simu yako inahitaji chaji iwe na 2A au zaidi wewe ukatumia chaji yenye 1.5A au yoyote chini ya 2A ujue kabisa hiyo chaji haitakuwa na uwezo wa kujaza chaji kwenye simu yako.

Hivyo ni muhimu pia kuzingatia/kujua simu yako inahitaji umeme kiasi gani ili iweze ingia chaji.
 
Shida ni kwamba hatufahmu hizi simu zetu znahtaji chaja yenye amp au volts ngapi
 
Nimesoma aya chache baada ya kuona unachanganya sana haya maneno, chaji na chaja!
 
Nyongeza kwa nini simu hazicharge
1. Kutumia USB cable ilyo mbovu au adaptor mbovu
2. Poor flex cables and connectors kama matatizo meng ya galaxy a series
3. Betri kuwa Na moto kidogo sana (matatzo ya iphone 6s kushuka chini)
4. Njia za umeme kuwa shorted kabla umeme haujafika kwenye PMIC
Fault trigs/trister kwenye upande wa iphone
5.kuanguka hupelekea flex cables kudetach hivyo simu hushindwa kucharge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom