benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Mkazi wa Mtaa wa Kota, Kata ya Mlandege Mkoani Iringa, Goodluck Mgovano aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 33 anadaiwa kumuua Mtoto wake Alvini Mgovano mwenye umri wa miaka minne kwa kumnyonga na kamba ya viatu huku akijirekodi kwa simu yake ya mkononi wakati akimnyonga Mtoto na alipomaliza akapiga selfie na mwili wa Mtoto na kuacha ujumbe ulioelekeza wapi Mtoto huyo azikiwe.
@AyoTV_ imefika nyumbani kwa Familia ya Marehemu na kukuta hali ya simanzi kwa Ndugu na Majirani ambapo wamesema wakati Baba anamnyonga Mtoto, Mkewe hakuwepo nyumbani na aliporudi alipiga kelele ‘Mume wangu amempa Mtoto sumu’ ndipo Majirani waliingia ndani na kukuta Mtoto amelala kitandani, walimpa maziwa lakini yalikuwa hayapiti ndipo ikabainika amefariki.
Kwa mujibu wa taarifa za Majirani Goodluck alijifungia ndani na Mtoto wake na kumnyonga nyuma ya mlango kwa kutumia kamba ya viatu huku akirekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkononi na baada ya hapo alimlaza kitandani na kupiga nae tena picha (Selfie) na kutokomea kusikojulikana na bado anatafutwa “Simu yake yenye picha na video aliiacha hapohapo nyumbani na kwa sasa ipo mikononi mwa Polisi”
Mtuhumiwa aliacha ujumbe uliosema “Chanzo cha mauaji haya ni ugomvi uliotokea kati yangu Mimi na Mke wangu mnamo October 6 , 2023 na Mimi naenda kujiua na nataka Mimi na Mwanangu tuzikwe Kijiji cha Itendulinyi”
Diwani wa Kata ya Mlandege, Jackson Chaula amesema Mtuhumiwa alikuwa anafanya kazi ya ubebaji mizigo katika magari lakini hakuwa na shida yeyot, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa Alfred Mwakalebela amekiri kupokea mwili huo na kusema mwili huo ulikuwa na makovu ya shingoni.. @AyoTV_ inaendelea na jitihada za kumpata RPC Iringa ili kupata taarifa zaidi kutoka Polisi.
View: https://www.instagram.com/p/Cy8Lj94ijls/?img_index=1