Kuna mambo mengi sana hapo ya kuyaangalia kabla ya kufanya maamuzi, kwanza hongera zake kwa kujikwamua na fedheha za kupanga.
Pili, kama ameweza kuvumilia kadhia za usafiri hadi sasa hivi hadi amehamia kwenye nyumba yake ndogo sio mbaya akiendelea kuvumilia ili aezeke nyumba kubwa. Kama nyumba ipo maeneo mazuri, akiiezeka anaweza kuipangisha ikawa kama kitega uchumi ikaingiza pesa ambazo baade taratibu atanunua gari huku nyumba ikiwa imeezekwa.
Gari ukishalinunua lina gharama zake za matunzo, mafuta, service n.k hapo hatujaongelea mambo ya ajali, Mungu aepushie mbali.
Bora angeezeka nyumba kwanza kisha mambo ya gari yafuatie baadae.