Ally Kamwe, Shabiki Simba maarufu kama ‘Dokta Moo’ wapigwa faini ya shilingi milioni tano, Ahmed Ally aponea chupuchupu

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,141
1,944
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemkuta na hatia shabiki wa Simba Mohamed Khamis Mohamed maarufu kama ‘Dokta Moo’ aliyeshtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.

Baada ya kamati hiyo kukutana kwa ajili ya kupitia na kutolea uamuzi shauri hilo mbele yake, ilitoa hukumu hii.

“Mohamed Khamis Mohamed, Mwanachama wa klabu ya Simba, alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021”.

“Baada ya Kamati kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, imemtia hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na kumpa adhabu ya kulipa faini ya sh. 5,000,000 (milioni tano) na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili. Adhabu hiyo inaanza tarehe 16/04/2025”.

Aidha Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, alishtakiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.

Baada ya kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, Kamati imemtia hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na kumpa adhabu ya kulipa faini ya sh. 5,000,000 (milioni tano) na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili. Adhabu hiyo inaanza tarehe 16/04/2025.
1745050440789.png
1745050686847.png
1745050930350.png
 
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemkuta na hatia shaniki w Simba Mohamed Khamis Mohamed maarufu kama ‘Dokta Moo’ aliyeshtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021.

Baada ya kamati hiyo kukutana kwa ajili ya kupitia na kutolea uamuzi shauri hilo mbele yake, ilitoa hukumu hii.

“Mohamed Khamis Mohamed, Mwanachama wa klabu ya Simba, alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF akituhumiwa kwa kosa la kuchochea umma kwa ujumla kinyume na Kanuni 73(4) ya Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la Mwaka 2021”.

“Baada ya Kamati kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake, imemtia hatiani kwa kosa aliloshtakiwa nalo na kumpa adhabu ya kulipa faini ya sh. 5,000,000 (milioni tano) na onyo la kutofanya kosa la kimaadili ndani ya kipindi cha miaka miwili. Adhabu hiyo inaanza tarehe 16/04/2025”.
ajabu kosa hujalisema!
 
Back
Top Bottom