kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Serikali ya CCM tuliipa nchi yetu tangu 1961 tulipopata Uhuru. Tumewapa Kodi na rasilimali zetu zote ili watupatie huduma kwa miaka yote hiyo. Bila shaka wamefanya mengi yanayoonekana kwa macho ya nyama na yarohoni. Wana hofu gani inayosababisha kuwaogopa na kuwakamata akina Mbowe?
Tanzania ilishaingia kwenye vitabu vya nchi za kidemokrasia miaka 3 iliyopita, vipi Tena?
Wacheni Kila mtu atumie akili, macho na masikio yake kuzipima kazi zenu kuona value of money kati ya huduma mnazowapatia dhidi ya Kodi na rasilimali zao walizowapa kwa miaka 60+, wacheni woga usiojulikana chanzo chake. Kazi ya serikali ingekuwa kuwapa ulinzi na kuwasikiliza wanachotaka kusema na kuona wanachotaka kufanya na kuvipima na kuchukua hatua.
kuwakamata ni sawa na kuwapa mileage kitaifa na kimataifa.
Soma: John Mrema: Wanachama na Viongozi wa CHADEMA waliokamatwa hadi sasa ni 427