Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 232
- 1,119
Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.
Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.
Mwananchi ilipomtafuta Dk Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.
Pia soma: Pre GE2025 - Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025