NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,577
- 13,415
Nimekua nikifuatilia sana hili sakata la Feitoto kwa pande zote mbili, lakini nimegundua bwana mdogo kuna mtu nyuma yake akimrubuni na kumvimbisha kichwa bwana mdogo Feisal Salum.
Ukitazama clip aliyozungumza mama yake vyema, basi utagundua kuna mengi yaliyojificha nyuma ya pazia.
Ndiyo, kuna wajinga wapo nyuma ya hili sakata wakijitahidi kusuka mambo ili tu Feisal aondoke pasipo na mpangilio maalum ndani ya Yanga.
Lakini hao manjangu waliopo nyuma ya Feisal Salum wanachokifanya hawaoni kabisa kuwa wanaua kipaji cha bwana mdogo, kijana kinda kabisa ndani ya taifa letu hili lakini tu siyo kwamba taifa linamtegemea bali wanapoteza ndoto zake zinakwenda kufifia gizani hii ni hatari sana.
Nyie mliopo nyuma ya Feisal pamoja na wapiga kelele au wagonga ulimbo wachambuzi wa mchongo mnaopiga kelele juu ya Feisal na muangalie nyuma na mtambue kuwa huyu bwana mdogo kipaji chake kinazama gizani. Sasa sijui akipotea mtakuja tena kusema Yanga imempoteza Feisal?
NB: Feisal kula ugali kwa sukari ni propaganda tu zilizosetiwa na kikundi cha wapumbavu wasiopenda maendeleo ya football ndani ya nchi yetu, hakika mama yake na Feisal katumika vibaya.