mwanyaluke
JF-Expert Member
- Jan 22, 2015
- 697
- 2,421
Nimekuwa mkulima wa parachichi kwa miaka mingi, lakini sijawahi kuona pesa inayosemekana ipo kwenye zao hili. Kila mwaka nakutana na sababu zile zile za changamoto za soko.
Baada ya kutafakari kwa muda mrefu, nimeamua rasmi kufyeka parachichi na kubadilisha mwelekeo wa kilimo changu. Nitatumia ardhi hiyo kufuga ng’ombe na mbuzi, huku nikibaki na kilimo cha viazi ambacho kimekuwa na faida kwangu.
Kwa wasiojua, nimewekeza sana kwenye kilimo cha parachichi. Shamba langu lipo vizuri, nimetumia mbolea za asili na chumvi, nimefanya installation ya mfumo wa umwagiliaji, na kutumia madawa kama boron na copper, pamoja na booster zinazotumika hata na wakulima wa Afrika Kusini. Pamoja na juhudi hizo zote, bado sijapata mafanikio niliyotarajia.
Nimeangalia pia maisha ya wakulima wenzangu—labda wao wananufaika, lakini kwangu hali ni tofauti. Naamini tatizo kubwa lipo kwenye soko la parachichi nchini Tanzania. Serikali imeweka tozo nyingi ambazo zinadhoofisha biashara hii, na wanaofaidika zaidi ni madalali kutoka Kenya.