Back to Kayumba Schools Campaign (Making Kayumba Schools Great Again) MAKASGA Camapign

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,673
31,370
Elimu bora ina fanya mambo matatu:

1. It will help you to acquire power.

2. It will help you to maintain power

3. It will help you to protect power.

Kwa bahati mbaya sana mfumo wa elimu yetu ya Tanzania hau guarantee hayo mambo matatu.

As a matter of fact juu ya sayari ya dunia kuna kikundi cha watu wasio pungua elfu 20 ambao ndio wana access na elimu yenye qualities hizo 3 nilizo zitaja hapo juu.

Hawa ndio wanao itawala dunia..

The rest of the world tuna access na elimu ambayo inatusaidia kusurvive.

BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN ( MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN )

Kwa sisi tulio pata elimu ya Msingi miaka ya tisini. Kaka zetu walio soma elimu ya Msingi miaka ya themanini pamoja na wadogo zetu walio soma elimu ya Msingi mwanzoni mwa miaka ya 2000 wengi wetu tulisoma katika shule zinazo fundisha mtaala wa NECTA kwa lugha ya kiswahili. Shule hizo ndio zilikuja baadae kubatizwa jina na kuitwa Shule za Kayumba.

Shule zenye kufundisha mtaala wa NECTA kwa lugha ya kiingereza zilikuwa chache, Mfano OLYMPIO ( dsm) ARUSHA SCHOOL ( Arusha) na NYAKAHOJA PRIMARY( MWANZA)

Almost watoto wote nchi nzima walisoma kwa lugha ya kiswahili..

KUCHIPUKA KWA SHULE BINAFSI ZA KIINGEREZA ( ENGLISH MEDIUMS)

Kulitokea mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili. Kwa maoni yangu nasema kulichagizwa zaidi na shule za ST.MARYS zilizo kuwa chini ya Mama Rwakatare( R.I.P)

Baada ya shule za St.Marys kufanya vizuri sokoni, Wafanya biashara wengi waliona fursa kwenye biashara ya elimu hivyo waka invest kwenye shule za kiingereza.

Taratibu kuibuka kwa shule za kiingereza kukaanza kutengeneza unyanyapaa dhidi ya shule za kiswahili.

Cha kushangaza zaidi hata wale watu ambao walilelewa kwenye shule hizo zinazo Itwa za Kayumba nao pia wakaingia kwenye mkumbo wa kuzinyanya paa shule za Kayumba.

WE HAVE TO MAKE KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN.

Msomi wa kweli ni yule anae tatua mambo ambayo anayaona ni changamoto kwenye jamii yake na sio kuyakimbia.

Badala ya kuzinyanya Paa shule za Kayumba kwanini tisiziboreshe? Ni kazi ya serikali? Serikali ni mimi na wewe.

Fanya chochote unacho weza kuboresha shule ya Msingi uliyo soma.

Butterfly effect is real. Kitu kidogo kimoja utakacho kifanya kinaweza kuleta impact kubwa kuliko unavyo weza kufikiria..

NILIICHO FANYA HADI SASA KWENYE SHULE NILIYO SOMA.

1. Nimepaka rangi shule nzima ( niliwashawishi alumni wenzangu tukachanga pesa tukapaka rangi shule nzima)

2. Tumepanda miti na maua kwenye shule hiyo.

3. Mwaka jana tuliajiri vijana watatu wahitimu wa kipato cha sita na mmoja mhitimu wa chuo kikuu kuwapiga msasa wanafunzi wa darasa la saba kwenye shule hiyo na matokeo yalikuwa mazuri wanafunzi wote walifaulu kwa wastani mzuri..

4. Tulichangisha michango sisi kama alumni plus kuwashawishi wana mtaa kuchanga pesa kwa ajili ya kujenga matundu mapya ya vyoo na sasa hivi watoto wanajisaidia kwenye vyoo visafi.

Sisi kama alumni wa shule yetu bado tuna mipango mingi sana kwa ajili ya kuboresha shule yetu kimiundombinu na kitaaluma.

Ewe mtanzania mwenzangu popote pale ulipo, fanya unacho weza kufanya kwa ajili ya shule ya kayumba/uliyo soma...Shule hizo ndio urithi wa vizazi vyetu. Hivyo ni jukumu letu kuziboresha .

My vision: Ni kuona shule zote za Msingi NCHINI Tanzania zinazo Itwa shule za Kayumba zinarudi katika hadhi yake ya awali.

1. Ziwe na mazingira mazuri.

2. Ziwe na miundo mbinu bora ya kusomea.

3. Ziwe na maendeleo mazuri kitaaluma.

BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN ( make Kayumba Schools Great AGAIN) ni kampeni ambayo itakuja kuchukiwa sana na wamiliki wa shule za English Medium kwa sababu moja kati ya malengo yake ni pamoja na watoto wanao soma katika shule za Kayumba, mbali na kulelewa kimaadili ya kitanzania lakini pia wanapata uelewa mzuri wa somo la kiingereza ili wanapo fika sekondari wasipate tabu kwenye masomo yao... ( kampeni hii itarejesha hadhi ya shule za Kayumba jambo ambalo wamiliki wa Shule za English Medium hawataki kulisikia)

Kampeni itaanzia hapa hapa Jf itakwenda instagram na am sure as heavens baada ya muda itaenea nchi nzima na hadhi ya shule za Kayumba itarudi tena..

Just keep in touch.

Sijawahi kufeli kwenye mission yoyote ile . Infact I am specialised in doing the things that seems to be impossible to other people.

I LOVE YOU TANZANIA.

God bless

====

Waliofata ushari wa kurudisha watoto Kayumba mpaka sasa

Ni braza moja kati ya wasomi wa kitaani kwetu. He was born in 1980. He is 5 years older than me. Darasani alikuwa very smart. Ni wale the cream wa Azania wa Enzi hizo.

To cut story short. Jamaa alikuwa mtumwa mwaminifu wa Shule za Ems. Amepunwa ile kinoma Noma. Kwanza Watoto wawili wa kwanza . Hawa aliendelea kupunwa hadi seco kawapeleka shule wanalipa ada tu milioni 6. Dogo wa kiume kamaliza form four kagoma kwenda Advance kasema anataka kwenda college. Kozi Aliyo ichagua sasa " PROCUREMENT ". Ule utoto aliokuwa anamwambia baba ake alipokuwa primary " Daddy I want to be a pilot, lawyer, Doctor or Engineer blah blah blah" ukawa ume evaporate.

Jamaa alikuwa so much dis appointed . Nakumbuka wakati wa Corona aliwahi niuzia kiwanja kwa bei ya Chanika halafu hela yote akaenda kulipa ada shuleni. Sehemu yenyewe aliyoniuzia kiwanja ni very potential area. Japo kiwanja sio chake ni cha urithi but aliniuzia kwa bei ya chini.

Mwaka mmoja baadae akataka nimtafutie mteja amuuzie kiwanja chake kingine alipe ada za watoto.

Nikamkalisha chini nikampa somo kuhusu shule za Kayumba. Nikamwambia warudishe wanao Kayumba. Watoto watatu sio poa. Mapacha wawili wa kike plus mdogo wa mwisho, kwa kipato chako sio kweli bro. Hata hivyo hakuna umuhimu wowote wa wewe kulipa hela yote hiyo kwa ajili ya Elimu ya msingi ya mtoto.

Toa watoto wako Em walete Kayumba. Mbona Mimi nimewatoa na wako poa tu.

Jamaa akawa inspired na ushauri wangu. Akawatoa watoto wake wote watatu Ems akawaleta Kayumba. Hao mapacha wawili ndio wamefaulu wamepata A zote na mdogo wao anafanya vizuri sana shuleni.

Jamaa kuandika gazeti refu sana ananishukuru mdogo wake kwa ushauri ambao pia umemsaidia kusave pesa na kuinvest kwenye mambo mengine.

Comments za wadau sasa. Kuna comments za watu kama sita ambao nao pia waliwatoa watoto wao Ems wakawaleta Kayumba. Wadau hao wanasema walikuwa inspired na Mimi. Baada ya kuona hadi Mimi nimewarudisha watoto wangu Kayumba. ( Aina ya maisha ninayo ishi na vitu ninavyo vimiliki ambavyo watu wa mtaani kwetu wanavijua, wanaona watoto wangu hawastahili kusoma Kayumba. Mimi kuwapeleka watoto wangu Kayumba ni jambo linalo tengeneza sentensi " kama Likud kawatoa watoto wake Kayumba Mimi nani)

Wengi walio watoa watoto wao Ems na kuwaleta Kayumba wanashukuru sana na wanajilaumu kwanini hawakufanya hivyo mapema.

Hata wewe mzazi unae jistress kulipia mamilioni kwenye shule za Ems wacha mara moja. Haraka sana kimbia kawatoe watoto wako EMS walete Kayumba. Huna sababu yoyote ile ya kujistress kulipa mamilioni huko EMs . N real sense,Shule za Ems hazina umuhimu wala UPEKEE wa aina yoyote ile. Umuhimu na upekee huo umetengenezwa na Wamiliki wa shule za Ems ili waendelee kukupuna.

Mtu muhimu kuliko wote kwenye shule hizo ni wewe mzazi kwa sababu wewe ndo unaelipa ada na ndio sababu kuu kwanini mmimiki kaanzisha shule hiyo.

Kilaza atasema " Likud huna hela "

Situmii hela hovyo kwa sababu ninazo.

Enyi wazazi ambao watoto wenu wamefanya vizuri kwenye shule za Kayumba enyi wazazi ambao mliwatoa watoto wenu Ems na kuwaleta Kayumba na wamefanya vizuri,acheni ubinafsi. Hakikisheni mnashare hizo information kwa watu wengi iwezekanavyo ili kuwatoa usingizini wazazi ambao bado wamelala. Wazazi ambao wana jistress kulipa mamilioni kwenye shule za Ems

====

Nilifuata ushauri wa Likud Nina watoa watoto wangu shule ya English Mediums.

Niliwatoa mwaka jana katikati. So mwaka huu mzima watoto wangu wamesoma Kayumba.

1. Kwa mwaka huu mzima pamoja na kumalizia kibanda changu na kununua kiwanja kingine,nimeweza kuhifadhi shilingi milioni 8 na uchafu.

2. Hili limewezekana kwa sababu nimewatoa watoto wangu shule ya English Medium.

Nilikuwa nasomesha watoto wa3. Mtoto mmoja kwa mwaka ada tu ni milioni mbili, bado hajaweka usafiri na vikorokocho vingine tuseme ukihesabu na hivyo inakuwa milioni 3 na ushee.

So kwa watoto watatu maana yake ningekuwa nimetoa milioni kumi halafu pia nisingekuwa na akiba yani sasa hivi ningekuwa naumiza kichwa ntapata wapi hela za kuwalia wanangu.

But :

1. Nimehamia kwangu. Watoto wangu wanaishi nyumbani kwababa yao. Nisinge wahamisha hadi muda huu ningekuwa sijajenga wala nisinge kuwa na kiwanja cha ziada wala hiyo milioni nane.

2. Nina kimilioni nane changu ambacho kufikia mwakani mwezi wa kumi na.mbili kwa mipango niliyo iweka itakuwa imezalisha mara kumi yake.

3. Watoto wangu wanasoma shule kifalme. Wanaenda kwa miguu umbali wa kama dakika kumi. Wanakula vizuri, wanalala pazuri, wanavaa vizuri, shuleni wana sare pea tano tano viatu pea tano tano mabegi pea 3 tatu kila mmoja.

Nawasimamia vizuri.

Wanafanya vizuri darasani.

Nimewawekea programme za kitaaluma : home tuition; English, Hesabu na Sayansi plus programme za kitaaluma kupitia kwenye Tv ya nchi 40+ ambayo pengine nisinge weza kuinunua kama wangesoma shule ya Em coz hela yote ingeishia kwenye ada.

Asante sana Likud.

Watanzania wenzangu wenye kipato cha kawaida fikirieni mara mbili. Wacheni kujistress na ada kwenye shule za EM wakati uwezo wenu ni wa kuunga unga.

Kusomea EM at least uwe na networth ya kuanzia walau milioni 150 plus.
 
Elimu bora ina fanya mambo matatu:

1. It will help you to acquire power.

2. It will help you to maintain power

3. It will help you to protect power.

Kwa bahati mbaya sana mfumo wa elimu yetu ya Tanzania hau guarantee hayo mambo matatu.

As a matter of fact juu ya sayari ya dunia kuna kikundi cha watu wasio pungua elfu 20 ambao ndio wana access na elimu yenye qualities hizo 3 nilizo zitaja hapo juu.

Hawa ndio wanao itawala dunia..

The rest of the world tuna access na elimu ambayo inatusaidia kusurvive.

BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN ( MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN )

Kwa sisi tulio pata elimu ya Msingi miaka ya tisini. Kaka zetu walio soma elimu ya Msingi miaka ya themanini pamoja na wadogo zetu walio soma elimu ya Msingi mwanzoni mwa miaka ya 2000 wengi wetu tulisoma katika shule zinazo fundisha mtaala wa NECTA kwa lugha ya kiswahili. Shule hizo ndio zilikuja baadae kubatizwa jina na kuitwa Shule za Kayumba.

Shule zenye kufundisha mtaala wa NECTA kwa lugha ya kiingereza zilikuwa chache, Mfano OLYMPIO ( dsm) ARUSHA SCHOOL ( Arusha) na NYAKAHOJA PRIMARY( MWANZA)

Almost watoto wote nchi nzima walisoma kwa lugha ya kiswahili..

KUCHIPUKA KWA SHULE BINAFSI ZA KIINGEREZA ( ENGLISH MEDIUMS)

Kulitokea mwishoni mwa miaka ya tisini na mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili. Kwa maoni yangu nasema kulichagizwa zaidi na shule za ST.MARYS zilizo kuwa chini ya Mama Rwakatare( R.I.P)

Baada ya shule za St.Marys kufanya vizuri sokoni, Wafanya biashara wengi waliona fursa kwenye biashara ya elimu hivyo waka invest kwenye shule za kiingereza.

Taratibu kuibuka kwa shule za kiingereza kukaanza kutengeneza unyanyapaa dhidi ya shule za kiswahili ambazo zilibatizwa jina la Kayumba.

Cha kushangaza zaidi hata wale watu ambao walilelewa kwenye shule hizo zinazo Itwa za Kayumba nao pia wana zinyanyapaa..

WE HAVE TO MAKE KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN.

Msomi wa kweli ni yule anae tatua mambo ambayo anayaona ni changamoto kwenye jamii yake na sio kuyakimbia.

Badala ya kuzinyanya Paa shule za Kayumba kwanini tisiziboreshe? Ni kazi ya serikali? Serikali ni mimi na wewe.

Fanya chochote unacho weza kuboresha shule ya Msingi uliyo soma.

Butterfly effect is real. Kitu kidogo kimoja utakacho kifanya kinaweza kuleta impact kubwa kuliko unavyo weza kufikiria..

NILIICHO FANYA HADI SASA KWENYE SHULE NILIYO SOMA.

1. Nimepaka rangi shule nzima ( niliwashawishi alumni wenzangu tukachanga pesa tukapaka rangi shule nzima)

2. Tumepanda miti na maua kwenye shule hiyo.

3. Mwaka jana tuliajiri vijana watatu wahitimu wa kipato cha sita na mmoja mhitimu wa chuo kikuu kuwapiga msasa wanafunzi wa darasa la saba kwenye shule hiyo na matokeo yalikuwa mazuri wanafunzi wote walifaulu kwa wastani mzuri..

4. Tulichangisha michango sisi kama alumni plus kuwashawishi wana mtaa kuchanga pesa kwa ajili ya kujenga matundu mapya ya vyoo na sasa hivi watoto wanajisaidia kwenye vyoo visafi.

Sisi kama alumni wa shule yetu bado tuna mipango mingi sana kwa ajili ya kuboresha shule yetu kimiundombinu na kitaaluma.

Ewe mtanzania mwenzangu popote pale ulipo fanya unacho weza kufanya kwa ajili ya shule ya kayumba/uliyo soma...

My vision: Ni kuona shule zote za Msingi NCHINI Tanzania zinazo Itwa shule za Kayumba zinarudi katika hadhi yake ya awali.

1. Ziwe na mazingira mazuri.

2. Ziwe na miundo mbinu bora us kusomea.

3. Ziwe na maendeleo mazuri kitaaluma.

BACK TO KAYUMBA SCHOOLS CAMPAIGN ( make Kayumba Schools Great AGAIN) ni kampeni ambayo utakuja kuchukiwa sana na wamiliki wa shule za English Medium kwa sababu moja kati ya malengo yake ni pamoja na watoto wanao soma katika shule za Kayumba, mbali na kulelewa kimaadili ya kitanzania lakini pia wanapata uelewa mzuri wa somo la kiingereza ili wanapo fika sekondari wasipate tabu kwenye masomo yao...

Kampeni itaanzia hapa hapa Jf itakwenda instagram na am sure as heavens baada ya muda itaenea nchi nzima na hadhi ya shule za Kayumba utarudi tena..

Just keep in touch. Sijawahi kufeli kwenye mission yoyote ile . Infact I am specialised in doing the things that seems to be impossible to other people.

God bless
Mpaka pale ccm itakavo tenganisha siasa na elimu, ndo ubora wa elimu utakapo onekana.
 
Mpaka pale ccm itakavo tenganisha siasa na elimu, ndo ubora wa elimu utakapo onekana.
WE don't have to wait on that. Hata kwenye Biblia imeandikwa " Hapo Mwanzo dunia ilikuwa imejaa giza, utupu na ukiwa, lakini Mungu aliziumba mbingu na nchi"

Maana yake nini? Giza halikumzuia Mungu kufanya kazi ya uumbaji.

kumbe basi hata sisi wanadamu ambao tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hatupaswi kuruhusu changamoto zituzuie kufanya kazi ya kujenga.
 
Jidanganye uliza Magufulu na kiherehere chake cha kubadili nchi alishia wapi?
 
Nothing you can do than help ur kids with good and quality education.

St kayumba sio shule inayoweza Mfanya Mtu akakomaa kimaarifa.do it for own risk.
 
Ni kampeni nzuri ya kizalendo ila imekosa shabaha na ni mtihani mgumu kutekeleza kampeni hii kwa vitendo. Serikali ina hela kupeleka halmashauri shule zake ziwe bora. Mimi tu kama mwalimu hainilipi vizuri mshahara, hakuna extra time allowance, naishi kwenye gofu la shule liliochoka, huo moyo wa kujitolea kukarabati madarasa na vyoo vya wanafunzi kwa mshahara wangu nautoa wapi ikiwa kufundisha nakatishwa tamaa? Mshahara wangu wa mwezi ndio pensheni yangu full stop. But kayumba school will remain the best at all times. Huko kwingine kwa wafanya biashara ya elimu ni kubovu ila wazazi hawajui wanafuata mkumbo ili waonekane wanasomesha watoto shule bora english medium. Walimu wenyewe wa kuokoteza mitaani, ndugu wa wamiliki wa shule na hawana mafunzo ya ualimu, ni wababaishaji wa masomo huku hawajui kuongea lugha ya kiingereza kwa ufasaha, wanafunzi wao ndio kabisa wanaongea english vapour. Ni vituko vitupu
 
Hamna huwezi kuwa na hela mwanao akaenda kula vumbi.
Hiyo elimu inayo tolewa English Mediums ina quality 3 nilizo zitaja hapo juu?
To enable a person :
1. To acquire power

2. To maintain power and

3. To protect power?
 
Tatizo ni umasikini
Yes upo sahihi bwana tajiri, ndio maana tunapiga kampeni hii kuwasaidia watoto wa masikini ambao hawana uwezo wa kulipa mamilioni kusomesha watoto wao kiingereza
 
1. Kwanza wazo lako ni wazo zuri sana (nakupongeza kwa hili)
2. Mtanzania wa kawaida hawezi akafanya lolote kuibadilisha elimu ya Tanzania zaidi ya serikali.
3. Bado kuna watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu bata michango ama mahitaji ya watoto wao kwenda shule za kawaida.
4. Kama serikali haifanyi, mimi ninani nitaweza na nitaweza kwa pesa gani wakati hata mshahara wenyewe haunitoshi hata kubakiza kidogo nimsaidie mama yangu kule kijijini?
5. Lakinipia wanaume hua tukuishiwa tunapenda kutafuta utetezi na justifications ili tu kutetea kile kilicho tushinda kionekane ni kibaya.
 
Sawa
 
Back
Top Bottom