Aliyekatwa mikono kwa utasa sasa ni mjamzito

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411


Mwanamke ambaye alishambuliwa na mmewe na kukatwa mikono nchini Kenya, baada ya ndoa yao kuvunjika kwa kishindwa kuzaa mtoto, sasa anaripotiwa kuwa mjamzito.

Muda mfupi baada ya kushambuliwa, Jackline Mwende alisema kuwa madaktari walikuwa wamewajulisha kuwa yeye alikuwa na uwezo wa kushika mimba, lakini mmewe Stephen Ngila, hakuwa na uwezo wa kuzaa.

Kwenye mahojiano na gazeti na Daily Nation, Mwende amesema kuwa hali hii ilichangia aanze uhusiano mwingine.

Anasema alikuwa na haja ya kuwa na watoto ndipo akaanza uhusiano na mwanamume mwingine ili kuokoa ndoa yake, lakini mumewe ambaye sasa anakabiliwa na kesi ya kutaka kuua akagundua.

"Nilikuwa ninataka mtoto. Nilikuwa na haja ya mtoto...na pia ibilisi alisababisha mimi kutembea nje ya ndoa yangu. Haikuwa vizuri kufanya hivyo, ninajua watu watanihukumu vikali kwa sababu ya hilo. Kwa vile niko hai na nitajifungua mtoto hivi karibuni, nini matumaini licha ya kupitia taabu." Alisema mwende.

Chanzo: BBC
 
Yaani haya mambo ya ndoa hayana mtaalam, inabidi kumwomba Mungu. Wengi tutahukumu na kuongea mengi lakini kati ya mume na mke wenyewe ndio wanajua kulikoni baina yao. Binafsi nahisi hasira sana kuona alichofanyiwa huyu mwanamke, kwa kweli ningekua karibu na huyo jamaa lazima pangechimbika.

Lakini pia ni rahisi kuongea mengi kwenye keyboard ya computer, subiri hadi yakukute, kwamba unaishi na mwanamke na umeshindwa kumpa mimba halafu aanze kugegedwa na mwanaume mwengine ili azae....... uzingatie kwamba wewe ni mwanaume wa kijijini, kule ambapo watu huwa na viburi vya ovyo na itikadi za kiajabu ajabu.

Nimefanya kazi ya asasi fulani ya kijamii ambapo tulizunguka vijijini sehemu nyingi, niliwakuta watu wapo nyuma sana kiakili. Kwengine unakuta mume anamuambukiza mkewe ukimwi halafu anamfukuza na kumtukana matusi makubwa, mke akirudi kwao wanamwona malaya kwamba yeye kamuambukiza mumewe ukimwi halafu sasa amerudi kwao nyumbani kuwaambukiza na wao pia. Tulitumia nguvu nyingi sana kutoa elimu.
 
Hivi wewe ni mkenya au mtanzania.kiswahili chako ni kama mtanzania vile. Xorry kwa kuwa nje ya maada
 
kichwa cha habari kingebadilishwa, kionekane "aliyekatwa mkono kwa uzinifu ashika mimba"...huyo hakukatwa mkono kwasababu hazai, bali kwasababu anafuata mbegu nje. alistahili hiyo adhabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…