Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,444
- 40,538
Julius Malema wakati wa harakati zake za kisiasa na wakati wa Kampeni za mwaka huu, alijiegemeza Sana kwenye kukishambulia chama cha siasa cha pili kwa ukubwa nchini Afrika ya Kusini.
Malema alikuwa anaonesha kuwa tatizo la Afrika ya kusini ni "wazungu" wanaobebwa na ANC kuwepo kwake madarakani.
Akajenga hoja kuwa ili Afrika ya Kusini ikombolewe kiuchumi na kijamii, ni lazima kwanza ANC itoke madarakani ili chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) kiweze kupambana na wazungu kikiwa madarakani.
Ghafla aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, akaunda chama na kukipa jina la uMkhonto we Sizwe (MK) ambacho kina mfanano kifalsafa na kisera na ANC isipokuwa kwenye sera ya utaifishaji migodi ya dhahabu na Platinum.
EFF ikapoteza uungwaji mkono na MK ikachukua zaidi ya Viti 58 huku Democratic Alliance (DA) iliyokuwa inapigwa vita na EFF ikijiongezea Viti 5 na EFF yenyewe ikipoteza Viti 5 vya ubunge.
Leo hii DA iliyokuwa inashambuliwa na EFF ndiyo Iko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuunda serikali ya mseto na ANC kuliko ilivyo Kwa EFF ya Julius Malema.
Hapa Tanzania ACT wako bize kupambana na CHADEMA badala ya kujijenga yenyewe. Mwisho wa siku CHADEMA ama itaongoza nchi au itakuwa chama kikuu Cha upinzani wakati huo ACT itakuwa haina nguvu za kisiasa Zanzibar.