BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,803
Mahakama Kuu ya Tanzania, imemwachia huru mzee wa miaka 78 ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa madai ya kumbaka mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 na kumwambukiza virusi vya Ukimwi (VVU) kati ya 2022 na 2023.
Mbali na Mahakama ya Wilaya ya Iringa kumuhukumu kifungo cha maisha Oktoba 20, 2023, Mahakama ilikuwa pia ilimwamuru kumlipa mtoto huyo, fidia ya Sh30 milioni, kulipa faini ya Sh5 milioni na kuchapwa viboko 11.
Mzee huyo alikuwa ametiwa hatiani kwa makosa matatu, moja la kubaka mtoto mwenye umri chini ya miaka 18, kumwambukiza virusi vya Ukimwi (VVU) kwa makusudi na kosa la tatu likiwa ni kufanya jaribio la kumbaka mtoto huyo.
Hukumu ya kubatilisha na kufutwa adhabu hizo, imetolewa Juni 28, 2024 na Jaji Eliamin Laltaika wa Mahakama Kuu kanda ya Iringa, akisema upande wa Jamhuri haukuweza kuthibitisha kesi hiyo kwa viwango vinavyokubalika kisheria.
Kubatilisha kwa hukumu hiyo na hatimaye kuachiwa huru kwa mzee huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili, kulitokana na rufaa aliyoikata Mahakama Kuu kanda ya Iringa, akiegemea sababu tano kupinga hukumu hiyo.
Miongoni mwa hoja hizo ni, Hakimu aliyemhukumu alikosea kisheria kumtia hatiani na kumpa adhabu hizo kwa kuegemea ushahidi dhaifu wa mwathirika (mtoto), aliyeshindwa kutaja tarehe halisi ambazo mshitakiwa alimbaka.
MWANANCHI
Pia Soma
- Iringa: Jela maisha kwa kubaka na kumpa mtoto Ukimwi