Alikiba: Kalamu ya wino wa dhahabu

Super Charged

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
937
1,687
Msanii Ali saleh Kiba Alimaarufu Kama Alikiba Kutoka Kigoma Anasifika Kwa Uwaandishi Mzuri licha Ya mara nyingi Kutofuata Urari wa Vina Na Mizani katika mashairi Yake.

Mnamo Mwaka 2006 aliachia album Yake Inayojulikana Kwa jina la CINDERELLA ikawashirikisha wasanii Kama
Hakeem 5,Queen darleen, Taqwa, Dullysykes, Ranny, Zaharan, Kalama p na Kjt

Kwa hakika wino Alioutumia Kuandika Hii album sio wino wa Kawaida licha Ya Kuwa imeshapita Miaka Mingi tangu Album iachiliwe lakini bado Nyimbo hizo Zinavutia Masikio Ya Wasikilizaji Rika zote,Nyimbo zenye Mafundisho na Maudhui Mazuri Kama Mac Muga Ikielezea Kijana alizamia south Afrika starehe zikamhadaa Akarudi Mikono mitupu Tanzania huku akiwa hajui Wapi pa kuanzia.

ALIKIBA Great of All time Ikiwa ana Miaka takribani 20 Kwenye Game Lakini Bado Anang'ara Mawinguni Kaweza Kulinda nafasi yake Kwenye Kiwanda cha mziki. Tumeshuhudia Anguko La wasanii wengi Waliovuma kwa kasi kipindi cha nyuma kidogo wasanii kama Belle 9,Dullyskyes,Marehemu Sam wa Ukweli,Marlow Na wengine Baadhi.

Binafsi nyimbo Hizi za Alikiba Haziwezi toka masikioni Kwangu hata nikikuta sehemu zinapigwa nitasimama kuzisikiliza, Nyimbo Kama:-
1. Hadithi
2. Mac muga
3. Nakshi nakshi
4. Mapenzi yana run Dunia
5. Mwana
6. Single Boy
7. Cinderella

Inatosha Kusema Alikiba Ana Miliki Kalamu yenye Wino wa Dhahabu
Kwa Kumalizia simshabikii yoyote yule Nashabikia Mziki mzuri,Mziki Uliobeba Burudani Na Mafunzo Ndani Yake.
 
Hujui maana ya mwanamuziki na mchangamshaji
Wanaomwita mondi mchangamshaji wanatafuta chaka la kujificha tu. Wote ni wana mziki na mmoja kati ya hao muziki wake umemnufaisha sana na unapendwa na walio wengi.

Unaweza kukatiza mitaa karibia 15 unasikia nyimbo za mwanamziki mmoja tu ambaye hata wewe unamjua
 
Wanaomwita mondi mchangamshaji wanatafuta chaka la kujificha tu. Wote ni wana mziki na mmoja kati ya hao muziki wake umemnufaisha sana na unapendwa na walio wengi.

Unaweza kukatiza mitaa karibia 15 unasikia nyimbo za mwanamziki mmoja tu ambaye hata wewe unamjua
Naona mada imewapita kushoto, kaongelewa AliKiba na ndie King of Bongo Fleva hata Mondi anajua hilo, mziki wa AliKiba unaishi milele kama vile leo tunavyosikiliza miziki ya kina Kenny Rodgers, Bob Marley, Michael Jackson, Phil Collins, Cliff Richard, Dolly Parton,n.k na tunaburudika utadhani tulikuwepo enzi zao, hao ndio Wanamuziki, wanasikilizika kwa rika lote na kizazi chote,

Mziki wa Mondi hauishi ni mchangamshaji ila hana nyimbo za kufanya zije zisikilizwe miaka 100 ijayo na kizazi kingine,

Natumaini umeelewa point yangu.
 
Mac Muga bya kiba & Ntarejea by mondi…..hzi zitaishi sana zinamafunzo adi miaka 50 ijayo

Ila siku hzi wote wanaonyesha six pack zao wanaimba matusi hasa hasa mondi….Nahisi ni laana hzoo
 
Mziki wa Mondi hauishi ni mchangamshaji ila hana nyimbo za kufanya zije zisikilizwe miaka 100 ijayo na kizazi kingine,
Zipo nyimbo ambazo nahisi aliandikiwa ambazo kimsingi zina maisha marefu ingawa 96% ni fujo za matusi yanayokifaa kizazi husika

Mac Muga bya kiba & Ntarejea by mondi…..hzi zitaishi sana zinamafunzo adi miaka 50 ijayo
Yeeees, Nitarejea, hii itakuwa aliandikiwa; hana akili ya kuandika hii nyimbo.

Uandishi wa Kiba au kama anaandikiwa, basi anatumia hisia halisi na sio mihemko

Diamond ana Ufalme Gani kwa Kuimba Yesa yesa Na Kucopy Idea za Kina Asake
Hili suala la kukopi limevuma sana kipindi fulani. Hakuna nyimbo ambayo Kiba naye anatuhumiwa kukopi?
 
Back
Top Bottom