Alianza kusoma BSc In Mechanical Engineering aka-drop out baada ya kuumwa. Je, kuna ofisi private zinazoweza kumpa kazi?

Candela

JF-Expert Member
Aug 12, 2021
811
2,126
Kuna kijana hapa alisoma BSc In mechanical Engineering, mwaka wa 3 semister ya 2 akaugua sana akashindwa kuendelea akaomba kuahirisha, mwaka uliofuata akaahirisha tena akae sawa kabisa.

Alipotaka kurudi aendelee na masomo chuo walimpokea lakini bodi ya mikopo wakasema hana sifa kuendelea kupata mkopo(kwao kuahirisha ni mwaka mmoja pekee).

Hali ikawa tete kijana aka drop out. Sasa akapambana sana arejee asome tena lakini uchumi umekuwa mgumu sana kwa wakati huu anapambana anapata hela ya kula tu.

Anaomba ushauri kama kuna ofisi private zinazoweza kumpa kazi mtu kama yeye. Kwani kama ni utaalamu dogo anajua sana yaani ni wale watu alisomea anachokipenda na anakiweza, practical yupo vizuri sana kuanzia Mechanical yenyewe, electronics, sijui mambo ya IoT ndio utampenda ukimpa programming ndio utadata, yani ni full package.

Ukija kwenye embedded systems ni kisanga. Kuna sehemu alikuwa anafanya kama freelancing ila ndio hivyo sio uhakika.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom