Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,444
- 3,627
Kada wa Chadema aliyeuwawa na wasiojulikana atazikwa leo na Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi atakuwepo.
Inna lillah waina illah rajiuun
-----
Mwili wa aliyekuwa Kada wa Chadema, Ali Kibao unatarajiwa kuzikwa leo Jijini Tanga, kata ya Tongoni katika kijiji cha Tarugube, baada ya mwili huo kuwasili majira ya Saa 6 ya usiku ukitokea Jijini Dar es Salaam
Akizungumza nyumbani kwa Familia ya Marehemu Kibao, Naibu Katibu Wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Singo Benson Kigaila amesema msiba huo unatarajiwa kuhuduriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni
Viongozi wengine ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Buruani, mkuu wa wilaya ya Tanga mjini Japhary Kubecha, Viongozi wa vyama mbalimbali, dini pamoja na wananchi
Kibao ambaye ni mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema inadaiwa jioni ya Septemba 6, 2024 maeneo ya Kibo Complex Tegeta jijini Dar es Salaam, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga na basi la Tashrif alishushwa kwenye basi hilo na kuchukuliwa na watu wasiojulikana majina yao wala walipotokea.
Pia, soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana