Albert Chalamila: Sijaridhishwa na hiki mlichofanya DAWASA, pia wanaoiba Mita za Maji washughulikiwe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,661
6,395

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kuja na mkakati wa kudhibiti wizi wa Mita za Maji baada ya kueleza kuwa kumekuwa na matukio mengi ya wizi wa Mita hizo.

Amesema wezi wa Mita wapo Mtaani hawatakiwi kuchekewa, amesema DAWASA ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kutokomeza tabia hiyo, ametoa maelekezo hayo alipofanya ziara kukagua Mradi wa Maji maeneo ya Malamba Mawili, Mbezi.

Pia soma:
~ Wizi wa mita za maji Mbezi Mtaa wa Luis (Upendo)
~ Wizi wa mita za maji washamiri Mbweni Teta, DAWASA wapo kimya
~ Wizi wa mita za maji, mita hizi zinapelekwa wapi?

Dar: Emmanuel Kalungwana kortini kwa wizi wa Mita za DAWASA
 
Back
Top Bottom