'Alan Alda' Muigazaji wa Marekani aliwahi kutolea Mfano Tanzania kama moja ya nchi inayotoza kodi za juu Afrika

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
4,720
6,956
Ilikuwa ni mwaka 2015 katika kipindi cha Television huko USA kiitwacho "The west Wing". Alan Alda akawa anaigiza kama Rais wa Marekani akiizungumzia Afrika na changamoto zake za kiuchumi.

Kilichonivutia hadi kuandika uzi huu ni kumsikiliza Alan Alda akiitolea Tanzania mfano wa nchi inayoongoza kwa utitiri wa kodi za hovyo kabisa barani Africa.

Sijapenda Tanzania nchi yangu kutolewa mfano wa hovyo kama huo (ingawa ni maigizo lakini kuna ukweli mchungu ndani yake na, ukweli mchungu huwa unauma).

I wish Mwigulu Nchemba au viongozi wetu wangemsikiliza huyu jamaa, kuna kitu wangejifunza hasa hasa baada ya migomo ya wafanyabiashara wetu.

Hebu msikilize; 👇

Kwa tafsiri isiyo rasmi, jamaa anasema;
"Kwa Tanzania, kwa kila mapato ya dola za Kimarekani 475 kuna kiwango cha asilimia 30% ya kodi, na kwa kuongezea wanaweka asilimia 20% ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), fikiria hiyo ni kwa kila kitu utakacho nunua.

Hivyo viwango vya juu vya kodi vinapelekea isiwe rahisi kufanya uwekezaji wa mitaji mikubwa katika hizo nchi. Hivyo hakuna kitakachojengwa, hakuna biashara, wala viwanda, wala ukuaji wa uchumi, hakuna.

Nchi maskini za Kiafrica zina malipo ya chini kabisa kwa wafanyakazi hapa duniani. Licha ya hivyo, kampuni kama NIKE kwa mfano, haiwezi kujenga kiwanda katika mojawapo ya nchi kama hizo kwa sababu ya viwango vya juu vya kodi kandamizi.

Kodi zimeua uwezekano wa kuwa na maendeleo ya kiuchumi, zimeua matumaini yote ya hizi nchi kuweza kujitegemea zenyewe.

Na hiyo imewaweka moja kwa moja kwenye kutegemea huruma ya misaada na mikopo; na hapo ndipo penye kitu kibaya kuliko vyote, unajua ni kwanini hizo nchi zina viwango vya juu kabisa vya kodi?

Ni kwa sababu yetu sisi; wanataka kutuonesha sisi kuwa wanaweza kukusanya pesa za kutosha ili walipie mikopo yao. Lakini, kodi haiwezi kukusanya pesa yeyote kama kodi hiyo inaua uchumi.

Hivyo basi kinachotokea ni madhara ya kuhuzunisha yasiyotarajiwa ya nia yetu njema kabisa kwa bara la Afrika; wema wetu kwao ni kama tumezihimiza hizo nchi kujifungia ndani ya anguko la kiuchumi lililo baya na la kutisha.

Kama hatutozihimiza hizo nchi kupunguza viwango vyao vya kodi, kamwe hawataweza kukuza uchumi wao. Wananchi wao wataishi maisha yao yote bila ya kuwa na ajira, magonjwa yataongezeka, umaskini utakuwa ni endelevu, na watoto wao watakosa chakula; na misaada yetu kwao kamwe haitawatosheleza, kamwe!".
 
Kwa sasa siwezi kusema za Juu kabisa ila nina uhakika ni nchi yenye kodi za kipuuzi dunioani zisizoendana na uhalisia na kipato cha mlipa kodi...

Hivyo kupelekea wakwepa kodi kila wanapopata upenyo...., Vilevile hakuna value for money kwa kodi tunazolipa
 
Yaan wanaoimba na kusifu awajiulizi kwann ukwepaji kodi ni mkubwa kiasi hiki kumbe tatizo liko nao wenyewe wameoza na awaisikii harufu ya uozo Kwa ajili ya kukosa maono na kusikiliza Leo migomo every where guess what is next.
 
Ilikuwa ni mwaka 2015 katika kipindi cha Television huko USA kiitwacho "The west Wing". Alan Alda akawa anaigiza kama Rais wa Marekani akiizungumzia Afrika na changamoto zake za kiuchumi.

Kilichonivutia hadi kuandika uzi huu ni kumsikiliza Alan Alda akiitolea Tanzania mfano wa nchi inayoongoza kwa utitiri wa kodi za hovyo kabisa barani Africa.

Sijapenda Tanzania nchi yangu kutolewa mfano wa hovyo kama huo (ingawa ni maigizo lakini kuna ukweli mchungu ndani yake na, ukweli mchungu huwa unauma).

I wish Mwigulu Nchemba au viongozi wetu wangemsikiliza huyu jamaa, kuna kitu wangejifunza hasa hasa baada ya migomo ya wafanyabiashara wetu.

Hebu msikilize; 👇
View attachment 3027809
Kwa tafsiri isiyo rasmi, jamaa anasema;
"Kwa Tanzania, kwa kila mapato ya dola za Kimarekani 475 kuna kiwango cha asilimia 30% ya kodi, na kwa kuongezea wanaweka asilimia 20% ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT), fikiria hiyo ni kwa kila kitu utakacho nunua.

Hivyo viwango vya juu vya kodi vinapelekea isiwe rahisi kufanya uwekezaji wa mitaji mikubwa katika hizo nchi. Hivyo hakuna kitakachojengwa, hakuna biashara, wala viwanda, wala ukuaji wa uchumi, hakuna.

Nchi maskini za Kiafrica zina malipo ya chini kabisa kwa wafanyakazi hapa duniani. Licha ya hivyo, kampuni kama NIKE kwa mfano, haiwezi kujenga kiwanda katika mojawapo ya nchi kama hizo kwa sababu ya viwango vya juu vya kodi kandamizi.

Kodi zimeua uwezekano wa kuwa na maendeleo ya kiuchumi, zimeua matumaini yote ya hizi nchi kuweza kujitegemea zenyewe.

Na hiyo imewaweka moja kwa moja kwenye kutegemea huruma ya misaada na mikopo; na hapo ndipo penye kitu kibaya kuliko vyote, unajua ni kwanini hizo nchi zina viwango vya juu kabisa vya kodi?

Ni kwa sababu yetu sisi; wanataka kutuonesha sisi kuwa wanaweza kukusanya pesa za kutosha ili walipie mikopo yao. Lakini, kodi haiwezi kukusanya pesa yeyote kama kodi hiyo inaua uchumi.

Hivyo basi kinachotokea ni madhara ya kuhuzunisha yasiyotarajiwa ya nia yetu njema kabisa kwa bara la Afrika; wema wetu kwao ni kama tumezihimiza hizo nchi kujifungia ndani ya anguko la kiuchumi lililo baya na la kutisha.

Kama hatutozihimiza hizo nchi kupunguza viwango vyao vya kodi, kamwe hawataweza kukuza uchumi wao. Wananchi wao wataishi maisha yao yote bila ya kuwa na ajira, magonjwa yataongezeka, umaskini utakuwa ni endelevu, na watoto wao watakosa chakula; na misaada yetu kwao kamwe haitawatosheleza, kamwe!".
Dure
 
Back
Top Bottom