Akiri kuahidiwa kiasi cha euro 50000 ( zaidi ya milioni 124 za tz) na ufaransa ili kufanya vitendo vya ugaidi nchini Niger

Strong ladg

Senior Member
Jul 15, 2021
128
335
Katika hali iliyoshtua wengi, raia wa Algeria aitwaye Mohammed Amine Aissaoui mwenye umri wa miaka 35, amekiri kwamba aliahidiwa kiasi cha Euro 50000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 124 za Tz ili akafanye vitendo vya ugaidi nchini Niger.

Mohammed ambaye miongoni mwa raia wa Algeria waliohusika na vitendo mbalimbali vya uhalifu nchini Algeria,anadai kuwa mwaka 2022 alikutana na wawakilishi wa shirika lisilo la serikali la Ufaransa waliomuunganisha na mwanadiplomasia wa Ufaransa anayefanya kazi kwenye ubalozi wa Ufaransa mjini Algiers.

Mohammed anadai kwamba baadae aligundua kwamba mwanadiplomasia huyo ni jasusi wa shirika la ujasusi la Ufaransa la DGSE.

Mohammed anasema kwamba mwanadiplomasia huyo alimuahidi malipo ya Euro 50000 endapo Mohammed angekubali kwenda kuungana na magaidi wengine waliopo nchini Niger ili kufanya vitendo vya ugaidi nchini Niger mnamo mwaka 2023.

Hata hivyo ,Mohammed anadai mapinduzi ya Niger ya mwaka 2023 yalivuruga mipango yote ambayo tayari walikuwa wamepanga.

Haya yanakuja ikiwa imepita siku moja tangu serikali ya Algeria iituhumu Ufaransa kwa kupanga mipango ya kufanya ugaidi nchini Algeria. Serikali ya Algeria ilimuita balozi wa Ufaransa nchini humo ili atoe maelezo kuhusu tuhuma hizo.

Pia inakuja ikiwa imepita takribani mwezi mmoja tangu serikali ya Niger itangaze kumkamata jasusi wa DGSE mara baada ya jasusi huyo kutua katika mojawapo ya viwanja vya ndege vya nchini Niger.

Itakumbukwa pia kuwa mwaka 2022, serikali ya kijeshi ya Mali iliishitaki nchi ya Ufaransa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za kufadhili vitendo vya ugaidi nchini Mali kwa kutoa silaha, mafunzo pamoja na taarifa za kiintelejensia zilizowezesha magaidi kutekeleza vitendo vyao nchini Mali.

Source: AES INFO.

Sahel Info TV


View: https://x.com/AESinfos/status/1868754710263484444?t=0ePuj33KEkqUldjyp6H62Q&s=19

"Mali accuses France of allegedly supporting terrorists" Mali accuses France of allegedly supporting terrorists


View: https://youtu.be/15eMFZ-sQpk?si=N_nrNU2Jok3cpXDa
 
Kila siku nasema, Mabeberu ndo wafadhili WA magaidi duniani.

Hata juzi kiongoz wa mapinduz aliempindua Assad Ni gaidi la al Qaeda ,

Sahv wanajifanya kumsafisha Kiana na Yuko bega Kwa bega na serikali za mabeberu ili kuunda serikali mpya ya Syria.
 
Marekani kila anapo sema kuna ugaidi jeshi lake lipo nchini hapo, ila hayupo kwa kuondoa ugaidi yupo kwenye rasilimali za hio nchi na kuipeleka nchini kwake.
 
Watu walishajua ukitaka ugaidi ufanikiwe tenda wape kina mwamed.
Si ndio Majinga ya Kuyashika Masikio wewe badala Utafute Pesa kwa njia Salama na Yenye Amani unataka Uuwe watu ili upate hela alafu ukisha ua Unakimbia na kuanza Kuishi kwa Tabu kujificha ficha Sijui hizo Pesa utatumia zipi Sasa
 
Back
Top Bottom