Akipatikana Mzanzibari mmoja tu mwenye akili, atawaunganisha Wazanzibari

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
hivi katika zanzibar kumekosekana mtu mmoja tu mwenye akili ? yeyote anayekumbatia kundi dogo na kuendeleza kuwagawa wanzibari sijui kama anawafaa wazanzibari.

fikirieni mbele kodi za wazanzibari zinatakiwa kutumika kuboresha maisha waliyonayo wazanzibari leo na sio kudhibiti migogoro maisha yatarudi nyuma.
 
nahisi bado na sizan kama atapatikana hao migogoro tu ndo wanaweza wengine hapana
 
we ndio huna akili wazanzibzr wapo makini tena timamu na wanajitambua
 


Yaani baada ya kupindua haki ya wazanzibar kupata viongozi wanaowataka hamjatosheka mmeamua kuwatukana kabisa kuwa hawana akili, lakini hao unaowaona wana akili wamefanya nini kwa muda wa miaka 42?
 
mtu mwenye akili haishii kuangalia kwenye kiganja chake tu na haoni mbele huko aendako bali mwenye akili huona mbali ya upeo wa kiganja chake na kujaribu kujiepusha na njia inayomuelekeza kwenye matatizo na kufuata njia salama.

kama singidadodoma ungekuwa miongoni mwa wale wenye upeo wa kuona mbali ya viganja vyao vya mikono ungekubaliana na mimi kuwa wazanzibari kugawanyika katika makundi ni njia isiyo sahihi.

na mtu mwenye akili ni yule ambaye angewaunganisha wazanzibari kuwa kitu kimoja.

lakini kama kila mmoja anajiona upande wake yuko sahihi bila lakini wazanzibari wakaendelea kugawanyika hujanishawishi bado na huo umakini wa wazanzibari labda unaungalia kwa upeo wako huo huo.

binafsi natamani sana wazanzibari hawa waniprove wrong on ground lakini si kujitetea kwa maneno huko wakifanya tofauti.

we ndio huna akili wazanzibzr wapo makini tena timamu na wanajitambua
 
unafaidika nini muungano ukivunjika? mtoa mada declare your interest
 
unafaidika nini muungano ukivunjika? mtoa mada declare your interest
Nafikiri umemuelewa vibaya mleta mada yeye hazungumzii Muugano kuvunjika ila amewaza tu endapo atapatikaa mmoja ambaye ataweza kuwauganisha ili waondoe hii hali ya sisi wapemba wale waunguja...nafikiri amewaza sahihi ila viongozi huandaliwa ni wakati sasa watu wetu wa usalama muandae mtu wa aina hii lakini mkiwa na tahadhari kamwe asije kuuvunja Muungano wetu adhimu
 
miaka 42 iliyopita mafanikio mliyoyapata ni mchango wa wazanzibari wote.

yawezekana baadhi ya yale unayoyabeza yamefanywa na wale unaowaunga mkono ingawa leo hii wamebadili mashati na kuvaa ya rangi tofauti.

hivyo wazanzibari ifike wakati mjiulize hivi tunakoelekea kwa wanasiasa kuanza kutugawanya ndio tunapiga hatua kuelekea mbele au tunarudi nyuma?

je yeyote anayewagawanya ninyi kweli anataka kuwapeleka mbele au ndio atawarudisha nyuma zaidi?

hakuna mtu wa nje ya zanzibari atakuja kujenga zanzibari yenu isipokuwa ninyi wenyewe na njia ya kwanza ni kuepuka migogoro.

yawezekana miaka 42 iliyopita mmefanya kidogo lakini sasa ni wakati wa kupima wanaokuja na misema kama hii je wanaelekea kweli kufanya mfanye makubwa?

"there is no second chance in life" haya unayoishi leo ndio maisha yako, mkiyachezea msije kutafuta mchawi.

wazanzibari kuwa kitu kimoja ndio hatua ya kwanza katika njia yeyote ya kimaendeleo mtayoichukua na mkiichezea hiyo hamtapiga hatua zinazofuata.

Yaani baada ya kupindua haki ya wazanzibar kupata viongozi wanaowataka hamjatosheka mmeamua kuwatukana kabisa kuwa hawana akili, lakini hao unaowaona wana akili wamefanya nini kwa muda wa miaka 42?
 
nadhani hujaelewa

leo wazanzibari wanafanya uchaguzi lakini kuna wazanzibari wanasapoti uchaguzi na kuna wazanzibari wametangaza kususia uchaguzi. hii ni moja kwa moja siasa taratibu zinawagawa wazanzibari katika makundi na sio jambo jema kuiacha jamii inaendelea kutofautiana taratibu tubaki kimya kwa maana kwangu mimi wanasema nyumba ya jirani ikifanya nini kwako pia sijui kuna nini.

tofauti kama hizi zikiachiwa inakuwa ni mitaji inayotumiwa na wendawazimu. mtu aliyejengewa chuki kichwani anakuwa hawazi vizuri anaweza kujitia hasara kwa kudhani aqnamkomoa mwingine kumbe anajikomoa mwenye lakini hata anayewaza vizuri anaweza kupata hasara kutokana na mmoja tu asiyewaza kwenye kundi.

huwezi kuungana na watu ambao wao wenyewe wamrgawanyika katika viapnde ukapata faida au wau wakapata faida au muungano ukawa na maana hivyo wazanzibari kutokuwa kitu kimoja kunahatarisha muungano zaidi.

ni wakati sasa watanzania tujenge tabia ya kuambiana kuwa jamani mambo yanavyoelekea hapo mbona hakuna anayejaribu kuona mbali.

tukiwaacha wazanzibari wakabaki kubishana siku wakitoka kwenye ubishi na kuona pengine sehemu nyingine ya muungano imepiga hatua hawataona kuwa walijirudisha nyuma kwa kubishana bali watalaumu upande mwingine.

tunataka Tanzania yote tujielekeze katika kujenga uchumi wetu. tuna rasilimali nyingi sote tujielekeze katika kuzielekeza serikali zetu kutumia rasilimali hizo kutupeleka mbele na sio kuzielekeza serikali katika kushughulikia migogoro.



unafaidika nini muungano ukivunjika? mtoa mada declare your interest
 
Yeye aliyeweka mipaka ya visiwa na Mabara aliiweka Pemba karibu na Tanga kuliko unguja. Kwa tamaa za watu fulani Tanga wakaikataa wakidai wao ni waomani.
 
we unaona kuna mwenye akili zanzibar? wakti inatawaliwa na bara na wao ukiwaambia kuwa huru hawataki kabisa kusikia habari hizo. unadhan wangekuwa makini wangeendelea kuburuzwa kama tunavyowaburuza? acha si tujikamatie koloni miaka hii ni ngumu kuwa na koloni ila bara tumeweza kuwa na koloni letu.

 
hizo akili za mtungi kulowesha ulipokaa ukidhani unamkomoa mwingine.

ukiona china leo inapaa kiuchumi ni kutokana na mambo mengi lakini mojawapo ni population. ukiwa na watu wengi ni rahisi kuanzisha jambo lolote ndani ya nchi kwa maana ya kupata mtaji na soko.

kuungana kuna faida nyingi kiuchumi na vipofu wa maendeleo ndio pekee wanawaza kugawanya jamii katika vikundi vidogo kama kwao wataona ni raisi kupata madaraka katika vikundi vidogo kuliko ndani ya muungano bila kujali ugumu wa maisha unaotokana na jamii ndogo kutokujitosheleza.

zanzibari ikiwa imekaa kama zanzibari hebu angalia soko la viwanda, huwezi kuanzisha kiwanda kikubwa kwa kutegemea soko la ndani tu lakini kama kiwanda kikianzishwa zanzibari kina soko la tanzania nzima unafuu unakuwepo.

kuwabeza kama ulivyowaita ni kuwachochea wazidi kuchukia muungano.

 
Nilichokiona Leo huko Zanzibar, kinapokuja kitu Kwa nahusu Zanzibar, basi wazanzibar ni wamoja.
 
Kama angepatikana japo kiongozi mmoja tu mwenye hekima ambaye yupo madarakani, nina hakika utengano ungekwisha na maendeleo yangepatikana. Bahati mbaya tunao hawa ambao tunao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…