Poleni mnaosuburi ajira ndiyo mifumo ya nchi yetu ilivyo humu mtandaoni mtapewa matumaini,lugha za kuwaudhi,na maneno ya shombo ila ukweli utakuja kujulikana baadae mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusiana na ajira za 2015/2016. Mwaka jana tulisikia mengi sana ila mwisho wa siku tukajua mchele upi na pumba zipi kumbukeni humu kwenye majukwaa wanapita watu wengi sana wengine wanaponda wanapoona mnazungumzia ajira wakati wao wamesota kitaa mpaka hakieleweki ila ninavyojua mimi ajira mtapata tu wiki mbili zilizopita tulikuwa tunaaandaa taarifa juu ya walimu shuleni ikiwa inasehemu tatu walimu waliopo shuleni,uhitaji,upungufu .Hivyo msiwe na presha suala ni kuvuta subira kweli kitaa kinachosha sana kama huna cha kufanya daily unanunua bundle kuingia mtandaooni kupata info juu ya ajira walengwa msiwe na jabza .