Ajira za Ualimu 2020 Kwa mtazamo Chanya

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Mar 25, 2012
462
343
Wasalaam wanajukwaa

Ni dhahiri kwamba serikali imekwama kwa kipindi kirefu (tangu 2015 hadi wakati huu) kutoa ajira za ualimu kwa usawa (Sayansi&Arts) kama ambavyo imezoeleka katika taratibu za serikali za awamu zilizopita (hasa ya Mh. Jakaya.M.Kikwete) ambapo ajira Zilitolewa kwa wakati (Kila mwaka) na bila ubaguzi wowote kwa wote wenye sifa zinazotakiwa na kwa idadi kubwa (si chini ya ajira elfu ishiri na maelfu mengi) na kwa hivyo kila mhitimu wa fani ya ualimu alipata ajira kila anapohitimu.

Kwa kuwa hali ipo hivyo, serikali ni lazima ishirikiane na sekta binafsi kwa karibu sana katika kusaka suluhisho la kudumu la tatizo la ajira za ualimu nchini.

Ni kwa mazingira haya,serikali inapaswa kuiimarisha sekta binafsi katika huduma ya elimu ili kuipa uwezo wa kutoa ajira kwa maelfu ya wahitimu wa fani ya ualimu kwa tahasusi zote.

Serikali zilizopita ziliona umuhimu wa kuipanua sekta ya elimu ili kutoa wigo mpana wa upatianaji wa huduma ya elimu sambamba na ajira kwa vijana wanaohitimu fani ya ualimu nchini kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.

Kulipa hilo nguvu; Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi Stadi pamoja na Taasisi ya Elimu ya watu Wazima ikawakaribisha watu wenye uwezo wa kuwekeza na kuendesha Vituo vya Elimu ya Watu Wazima kwa njia ya masafa na ana kwa ana.

Hii ni hatua nzuri sana iliyopigwa pamoja na kwamba bado haitekelezwi na hailindwi na serikali na taasisi zake kama chanzo cha ajira za ualimu nchini.

Kupitia utaratibu huo,mamia ya vituo vya elimu ya watu wazima vimeanzishwa na kusajiliwa nchini na vituo hivi ikumbukwe tu kuwa ni walipakodi wakuaminika kwa serikali yetu tukufu.

Vituo hivi vinahitaji kuboreshewa mazingira ya kibiashara na serikali yetu ili viwe katika namna ya kujiendesha inayotoa faida kwa pande zote (watoa huduma na wapokea huduma) ili viweze kuajiri walimu wengi zaidi kulingana na kuboreka kwa mazingira na kuongezeka kwa wahitaji wa huduma.

Serikali na mamlaka zake zipige marufuku taasisi ambazo hazijasajiriwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI kutoa huduma za elimu - nje ya mfumo rasmi kama vile masomo ya ziada (tuition),QT(STG I,II&III), Reseating, Pre-Form One Courses, Pre-Form Five Courses, English Courses na Computer Courses.

Lakini pia vyombo hivi vinapaswa kuhakikisha kuwa vituo vinavyosajiliwa vinaajiri wahitimu wa fani ya ualimu kutoka vyuo vilivyosajiliwa na kutambuliwa na serikali kwa uwiano sahihi sawa na mwongozo wa utolewaji wa usajiri wa vituo vya kutolea elimu katika mfumo usio rasmi.

Serikali ipige marufuku walimu walioajiriwa serikalini kujihusisha na masuala ya kufundisha tuition,tempo na hata kutumika katika shule binafsi na vituo vya elimu ya watu wazima.

Serikali ipige marufuku shule za serikali zilizosajiri vituo vya mitihani (Qt&Pc) kuacha mara moja kutoa huduma ya masomo kwa watu wanaohitaji kusoma kupitia mfumo wa usio rasmi wa elimu nchini tofauti na sasa ambapo shule za serikali zimejiiingiza katika biashara ya kufundisha watu wanaotaka kusoma au kirudia masomo kwa mfumo usio rasmi.

Serikali ipige marufuku shule binafsi kuajiri watu wasio na sifa za fani ya ualimu kuanzia msingi (English Medium) hadi Sekondari na ninaomba UHAKIKI ufanyike Shule zote binafsi nchini kwa usimamizi mkali na wa haki kuliko ule uliofanywa kwa waajiriwa wa serikali wakati ule na shule hizi zifuate utaratibu wa wazi na haki na vigezo kuajiri walimu ikibidi zisimamiwe na Halmashauri zote nchini na wanapohitaji kuajiri wawape kazi hizo idara za elimu Halmashauri.

Serikali kupitia Taasisi ya Elimu kwa kushirikikana na ofisi za elimu wilaya zote nchini iwasadie wamiliki wa vituo vya kutolea huduma ya elimu nchini kudahili wanafunzi wanaoshindwa kuchaguliwa kujiunga na shule za sekondari za serikali katika halmashauri vilimo hapa nchini.

Serikali pia ipige marufuku shule binafsi kuajiri Wastaafu wa Ualimu kote nchini ngazi zote za elimu kote nchini.
Serikali ipige marufuku na iwakamate watu wote wasio na fani ya ualimu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali wanaojitangaza au kutangaza kutoa huduma ya elimu (Tuitio,pre-form one courses,Pre-form five courses,QT na Reseating,English Courses n.k) na iwafungulie mashitaka ya UHUJUMU UCHUMI, UTAPELI na KUGUSHI FANI ili wenye sifa stahiki wafanye hizo kazi kwa tija.Watu ambao hawajasomea fani ya ualimu wanashusha hadhi na thamani ya fani ya ualimu kwa kutoa huduma kwa bei zisizokidhi gharama halisi za huduma za elimu na ni dhuluma kwa wale waliosomea fani hiyo.


Mwisho kabisa, Serikali iurudishe ule Mswada wa Bodi ya Walimu 2016 pamoja na marekebesho yake bungeni ujadiliwe, Upitishwe na Rais ausaini uwe Sheria kamili na mamlaka zinazosimamia kufuatwa kwa sheria zifanye kazi zake.

Nina matumaini kabisa dhana ya ajira na kujiajiri kwa wahitimu wa fani ya ualimu nchini itafanikiwa ikiwa serikali itatilia maanani haya niliyoyaandika na kwa kiasi kikubwa hakuna mhitimu atakosa pa kujishikiza wakati serikali pia ikibakia kuwa MWAJIRI MKUU kwa kutoa ajira Makumi elfu manne, matano na hata elfu.

Cc:
Mh. Rais John P.J.Magufuli,
Mh. Waziri Joyce Ndarichako,
Mh. Waziri Selemani Jafo,
Wah. Maafisa Elimu Mkoa,
Wah. Maafisa Elimu Wilaya,
Wah. Waratibu wa Elimu Kata,
Wah. Watendaji Kata,
Wah. Wamiliki wa Vituo vya Elimu kwa Mfumo Usio Rasmi,
Wah. Wananchi na wadau wa Elimu.

Ahsante.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja kampeni zianze, utasikia TUTABORESHA NA KUONGEZA FURSA ZA AJIRA. Na bado tutawaamini


sijui huwa wanaturoga sisi wananchi

Kizibo
 
Nnaloliona mim hapa, serikali ipige marufuku watoto wote kwenda shule, maana elimu ya Tz ni non sense kwa sasa! Imagine mtu unamdahili mwenyewe akasome theoretical education alaf on collar based curriculum alaf akisha maliza unamwambia akajiajili!! Mtu kasomea mfano jinsi ya kufundisha wanafunzi huko vyuoni alaf unamwambia akajiajili je mtaji anatolea wapi!!? Kama ameshindwa hata kufinance elimu yake mpaka Heslb imemfadhiri je ndo atapata mtaji!!!?

Mi ninge shauli watoto tuwapeleke gereji, tuwapeleke kwenye collage za kilimo etc sio kupoteza mabilion kufinance hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajira mwezi huu zipo 16000 mkuu
 

Attachments

  • Screenshot_2020-02-10-09-53-46.png
    Screenshot_2020-02-10-09-53-46.png
    82.3 KB · Views: 1
  • Screenshot_2020-02-10-09-23-41.png
    Screenshot_2020-02-10-09-23-41.png
    147 KB · Views: 1
Poleni sana vijana. Ndio mjue siasa ni ajira mama. Siasa ni kama Katiba ya nchi ina nguvu sana kuhusu kesho ya mwananchi.

Siku nyingine msijekudharau hata mara moja kuhusu siasa. Ona sasa hivi wasomi wanamtegemea mwanasiasa afanye maamuzi kuhusu kesho yao.

Kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa kamili.

Badilikeni sasa vijana.
 
Vijana walikosea nini ili wajirekebeshe?
Poleni sana vijana. Ndio mjue siasa ni ajira mama. Siasa ni kama Katiba ya nchi ina nguvu sana kuhusu kesho ya mwananchi.

Siku nyingine msijekudharau hata mara moja kuhusu siasa. Ona sasa hivi wasomi wanamtegemea mwanasiasa afanye maamuzi kuhusu kesho yao.

Kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa kamili.

Badilikeni sasa vijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nnaloliona mim hapa, serikali ipige marufuku watoto wote kwenda shule, maana elimu ya Tz ni non sense kwa sasa! Imagine mtu unamdahili mwenyewe akasome theoretical education alaf on collar based curriculum alaf akisha maliza unamwambia akajiajili!! Mtu kasomea mfano jinsi ya kufundisha wanafunzi huko vyuoni alaf unamwambia akajiajili je mtaji anatolea wapi!!? Kama ameshindwa hata kufinance elimu yake mpaka Heslb imemfadhiri je ndo atapata mtaji!!!?

Mi ninge shauli watoto tuwapeleke gereji, tuwapeleke kwenye collage za kilimo etc sio kupoteza mabilion kufinance hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye college ya kilimo ndio hatoitaji Mtaji ?

Portfolio | 2020
 
Wasalaam wanajukwaa

Serikali ipige marufuku shule za serikali zilizosajiri vituo vya mitihani (Qt&Pc) kuacha mara moja kutoa huduma ya masomo kwa watu wanaohitaji kusoma kupitia mfumo wa usio rasmi wa elimu nchini tofauti na sasa ambapo shule za serikali zimejiiingiza katika biashara ya kufundisha watu wanaotaka kusoma au kirudia masomo kwa mfumo usio rasmi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa nini shule za serikali tu? Kwa nini hata shule binafsi zilizosajiliwa kutoa elimu kwa mfumo rasmi zisizuie kutoa elimu kwa mfumo usio rasmi QT na reseaters?
 
Back
Top Bottom